Utangulizi.

Saturday 13 January 2007
Wasomaji,

Baada ya muda kupita tangu kufanyika kwa mkutano wa blogu Tanzania, kamati ya muda imeamua kufungua blogu hii ili kutoa nafasi kwa kila mtu kuchangia mawazo yake juu ya yale tuliyokubaliana kuyafanyia kazi.

Katika mkutano huo tulikubaliana kuyafanyia kazi masuala makuu yafuatayo:-

1. Uundaji wa jumuiya ya wanablogu Tanzania.

2. Jina la jumuiya na aina ya muundo wake.

3. Kikusanya habari na jina lake.

4. Ujenzi wa tovuti ya jumuiya.

5. Tuzo na mfumo wa utolewaji wake.

6. Siku ya blogu Tanzania.

Ili kuweza kupata mawazo ya kina, kamati ya muda imepanga kwamba iwe ikijadiliwa mada mojamoja katika kipindi cha juma zima, na baada ya hapo tunahitimisha mada kwa kuchagua mapendekezo ya wengi kuwa jibu la mada.

Kwa kuanza, tunaanza kwa kupendekeza JINA la Jumuiya ya blogu Tanzania.
Wewe mwanablogu ungependa Jumuiya iitweje? Kumbuka mada hii itakuwa hewani hadi Ijumaa, Jumapili litapatikana jibu na jumatatu itatangazwa mada inayofuatia.
 
© Blogu Tanzania | Tarehe: 1/13/2007 |

Maoni: 15

  Tarehe: 15 January 2007 at 15:23 Anonymous Anonymous Anasema:
Napendekeza jina la blogu ya watanzania iitwe;
JUMUIYA YA BARUATANDO TANZANIA(JUBATA).Nimependekeza jina kwa kugha ya kiswahili ili kuienzi lugha yetu adhimu.
  Tarehe: 15 January 2007 at 22:07 Anonymous Anonymous Anasema:
Napendekeza Wanablogu Tanzania.
  Tarehe: 16 January 2007 at 09:23 Anonymous Anonymous Anasema:
napendekeza
1.Bongo Blogu
2.Bongo Syndicate
3.Blogu Bongo
4.Bongo Unleashed
5.Blogu TZ
6.Blogu Tanzania
  Tarehe: 16 January 2007 at 15:00 Anonymous Anonymous Anasema:
Wakati ukitoa maoni yako, iwapo kuna jina limependekwezwa ambalo umelipenda, ni vizuri kutamka kuwa unaliunga mkono. Hivi ndivyo tutajua jina gani linaungwa mkono na wengi.
  Tarehe: 16 January 2007 at 15:02 Anonymous Anonymous Anasema:
Isibingo,
Nadhani maneno kama BongoSyndicate, BongoUnleashed, n.k. yatafaa kuingizwa kwenye mapendekezo ya majina ya kikusanya habari (aggregator) badala ya jina la jumuiya yenyewe. Unasemaje?
Jumuiya ya wanablogu Tanzania
  Tarehe: 17 January 2007 at 16:03 Anonymous Anonymous Anasema:
Wanablogu Wa Tanzania
  Tarehe: 18 January 2007 at 14:51 Anonymous Anonymous Anasema:
Jumuiya ya Wanablogu wa Tanzania
Nimependa haya majina mawili:
1. Jumuiya ya wanablogu Tanzania
2. jumuiya ya wanablogu wa tanzania
napendekeza

1. bongoblogu

2. blogubongo
  Tarehe: 19 January 2007 at 21:46 Anonymous Anonymous Anasema:
Kwa mawazo yangu naona bongoblogu au blogubongo ni jina zuri kwa ajili ya kikusanya habari (aggregator). Lakini pia tunaweza kutumia maneno haya kwenye anuani ya tovuti (URL) iwapo neno litakalochaguliwa litakuwa refu sana kiasi cha kutofaa kuwepo kwenye URL.

Naelekea kupenda Jumuiya ya Wanablogu Tanzania (bila kuwepo kwa neno "wa" kabla ya neno Tanzania) kama alivyopendekeza Nambiza.

Wengine ambao wana mapendekezo ila hawajatoa inabidi watoe maana mjadala ndio unakaribia kufungwa.
Nadhani jina la jumuiya linapaswa kuwakilisha jumuiya hiyo bila utata kabisa. Vyama vya siasa, mawizara, asaasi za kiraia mara nyingi zina majina yaliyo wazi. kwa mfano: "wizara ya ardhi" ni jina linawakilisha katika maana halisi. Kwa maana wizara hiyo ni nini.

pengine tatizo linaweza kuja tunapotaka kupata jina linalowakilisha jumuiya ambalo ni jina 'cool' au la mtindo unaovutia.

nasisitiza kuungana na Kitururu na Macha hapo juu.
Napendekeza jina Jumuiya ya wanablogu Tanzania.Sellassi I.
Jumuiya ya blogu Tanzania
  Tarehe: 2 February 2007 at 00:50 Anonymous Anonymous Anasema:
Uhuru wa vyombo vya habari tulionao hivi sasa ungo njiani kutoweka kama sheria ya kudhibiti uhuru wa kupata habari na kuziandika/kuzitangaza itapitishwa na Bunge letu "huru". Kama hilo litatokea njia pekee kwa waTanzania kupata habari huru na za kweli ni kupita blogu HURU. Napendekeza jina: BloguHurutz