Mada ya juma hili: KATIBA.

Monday 12 February 2007
Juma lingine linaanza na mada mpya inaingia. Wasomaji bado tuko katika mada ya Muundo wa Jumuiya na katika juma hili tutajadili juu ya kuwa au kutokuwa na KATIBA ya Jumuiya.

Mada hii inaweza ikawa inaonekana fupi na rahisi kuijadili, lakini tunaomba tusiichukulie juu juu, tuchukue muda na kujiuliza kwanza juu ya umuhimu wa katiba, na kwa nini tunadhani jumuiya yetu inahitaji au haihitaji Katiba.

Karibuni katika mjadala. JE TUNAHITAJI KATIBA?
 
© Blogu Tanzania | Tarehe: 2/12/2007 |

Maoni: 22

Tunahitaji katiba ya kulinda jumuiya.
naunga mkono,tunahitaji katiba.
Naunga mkono kuwa na katiba.
Tunahitaji katiba. Hii itarahisisha vile vile kutenganisha haki za wanajumuiya wenye blogu na wale wasio nazo.
  Tarehe: 13 February 2007 at 21:50 Anonymous Anonymous Anasema:
Naunga mkono kuwepo kwa katiba. Katiba itatuwezesha kujua majukumu, kazi, na wajibu wa viongozi. Namna ya kuchagua viongozi, muda wa uongozi, taratibu za kuwatoa viongozi madarakani iwapo kutakuwa na ulazima, wajibu wa wanachama na haki zao (pia kama alivyosema Simon: tofauti za wajibu, haki, na majukumu ya wanachama wenye blogu na wasio na blogu [iwapo tutakubaliana kuwa wasio na blogu nao wawe wanachama]) na mengine mengi. Bila katiba hatutakuwa na mwongozo imara na unaoeleweka.
Muhimu tuwe na katiba kwa sababu zote mlizotaja hapo juu.
Simoni aliandika nanukuu,"Lakini sioni kwanini mchangiaji asiye na blogu ajulikanaye kama mwanajumuiya atengwe"
Na akaandika nanukuu "Hii itarahisisha vile vile kutenganisha haki za wanajumuiya wenye blogu na wale wasio nazo."
Na Ndesanjo akaandika,"...(pia kama alivyosema Simon: tofauti za wajibu, haki, na majukumu ya wanachama wenye blogu na wasio na blogu [iwapo tutakubaliana kuwa wasio na blogu nao wawe wanachama]"
Mmmm....NAONA HAPO NDIO MMEANZA KUWATENGA WASIO NA BLOGU!
(First class and second class citizen enhe?)
Ni sawa na kumkaribisha mgeni nyumbani kwako aishi kama wewe ila unapokula chakula yeye inabidi aliye jikoni wewe sebuleni. Ndio maana mimi mtizamo wangu ni wa kuwa na KATIBA ya wanachama wenye blogu. Ukiangalia kwa upande Mkubwa wachangiaji wa mjadala huu ni wenye blogu kwa hiyo ikiwa hivyo haya majukumu yatapangwa na wenye blogu kwa ajili ya wasio na blogu? (mambo hayo ya IMF, WORDBANK-Economic restructuring programmes sio?) Kuna misemo miwili hapa naiambatanisha.
Wema usizidi uwezo na unajikuna unapofikia. Na toa hoja
@Ndabuli:ambao hawanablogu ni chaguo lao kutokuwa na blogu na kwa hilo wanajua kabisa ni mambo gani wanayakosa.Sioni kuwa tunana watenga kwa sababu ni uamuzi wao kuwa katika kona hiyo.Kumtenga mtu ni pale tu atakavyo kuwa kama sisi halafu tukamkatalia.Naamini pia kuna watu hawanablogu sasa hivi lakini ni muhimu sana katika jumuiya hii yetu.
  Tarehe: 14 February 2007 at 15:25 Anonymous Anonymous Anasema:
Ndabuli: kutenga huku sio sawa na jinsi ulivyochukulia. Kitendo cha kuwa na viongozi na waongozwa tunaweza kusema pia tumetenga. Daraja A ndio hao viongozi wenye majukumu na nafasi kubwa kuliko wanaoongozwa, na daraja B ndio hao wanaoongozwa.

Hata tukichukulia hoja yako kuwa jumuiya iundwe tu na wale wenye blogu, tunaweza kuuliza kwanini tuwatenge wasio na blogu lakini wanashirikiana nasi?

Kutakuwa na wajibu ambao utatofautiana kati ya Mti Mkubwa au Zemarcopolo ambao wanashirikiana nasi bega kwa bega ila hawana blogu na mtu mwenye blogu. Mfano mmoja: katiba inaweza kusema kuwa kila mwanachama mwenye blogu lazima aweke nembo ya jumuiya katika blogu yake. Wajibu huu utakuwa ni kwa wale tu wenye blogu. Kipengele hiki hakitawagusa wasio na blogu.

Hili ndio jambo tulilogusia hapo juu kuhusu kuweka bayana tofauti za majukumu na wajibu kwa wana jumuiya wenye blogu na wasio na blogu.
Huu mjadala unanivutia sana.
@1.Simoni nakubali unaposema.."Kumtenga mtu ni pale tu atakavyo kuwa kama sisi halafu tukamkatalia." Asiye na blogu hajakuwa kama aliye na blogu kwa msemo wako huo basi hajatengwa.
2...unaposema...Naamini pia kuna watu hawanablogu sasa hivi lakini ni muhimu sana katika JUMUIYA HII YETU. Jumuiya ipi sasa unayozungumzia si ndio tuko kwenye utaratibu wa kuunda jumuiya (au kuna jumuiya nyingine?)(naona kwa mbali unaanza kuvutiwa na hoja zangu maana hii sentensi vilebile inaonyesha hiyo jumuiya unayozungumzia ni ya wenye blogu...hehe!)
@Ndesanjo...."Mfano mmoja: katiba inaweza kusema kuwa kila mwanachama mwenye blogu lazima aweke nembo ya jumuiya katika blogu yake". Huu Nadhani ni utambulisho mzuri wa kuwa mwanachama, asiye na blogu hataweza kujitambulisha kwa hili.. atajitambulisha kwa vipi? ..tukisema basi kuna sehemu unaweza kuona wanachama lakini utamu wa kiunganishi(link)kwa asiye na blogu unaupata vipi, nataka nimfikishie ujumbe asiye na blogu ningojee aje kwenye blogu yangu ndio ausome au nimtafutie wapi? Kwenye anuani pepe? mbona utamu wa kuacha ujumbe kwenye blogu unapotea(Najua utasema si anaweza mwenye blogu kuufuta..(lakini si utaonekana ameufuta kwenye blogu maarufu) ameupata)
Namalizia kwa kusema WENGI WAPE. Basi mtizamo wa wengi nitakubaliana nao.
Hadithi maana yake tuangalie zaidi kwenye utendaji wake(practicalities)
Ndabuli kidogo unaanza kunishawishi. Niko katika upande wa majukumu, naanza kujiuliza itakuwaje pale mwanajumuiya asiye na blogu atakapopewa jukumu fulani halafu akapotea tutampata wapi? au ndiyo tutaanza kubandika tangazo la WANTED katika kila blogu? mmh hapa tufikirie zaidi! (Jumuiya maana yake kazi na kazi zitafanywa na sisi wanajumuiya wenyewe au MWANDANI unasemaje naona uko kimya katika mada hii.) Jah Bless!
KATIBA NI MUHIMU.
Pili nachangia hoja ya Ndabuli.

Uanachama unaotokana na mahusiano.
Wapewe uanachama kutokana na mahusiano yao na wanablogu.

Kama ilivyosemwa na wengine awali, kuna wasio na blogu lakini wanarutubisha sana blogu kwa kuchangia maoni na kuwapa wenye blogu moyo kwamba kuna wanaosoma na kushiriki. Wanaotoa maoni kwa namna hii si busara kuwatenga.

Nipe ruksa niongee kwa mfano. Pengine nitumie mfano wa jumuiya ya wamakonde. Ikiwa mimi ni mmakonde niliyeoa msukuma. Ninaishi na msukuma, msukuma ananishauri masuala mbali mbali ya kila siku, tunashirikiana kwa hali na mali. Naona itakuwa si vyema kwangu kumuacha nyumbani msukuma wangu wakati nikienda kwenye shughuli za jumuiya ya wamakonde. Kwamba mapenzi na ushirikiano wetu una mipaka.

Ukiwachilia hivyo, huyu msukuma wangu anaweza kuwa na mawazo mazuri tu ya kunufaisha shughuli za jumuiya ya wamakonde. Anaweza kuwa na ujuzi au ustadi wa namna fulani ambao wamakonde hawana kwa wakati uliopo, naye akautoa kwa wamakonde. Sasa huyu msukuma ukimtenga atakuwa hana moyo wala sababu ya kutaka kujifunza kimakonde au hata kuwasaidia wamakonde. (sisemi kuwa wasio na blogu ni wake wa wanablogu – huu ni mfano tu)

Kwa mfano huo naona ni vyema kuwapa wasio na blogu uanachama – pengine sharti liwe kwamba wanaweza kuwa wanachama ikiwa wao ni washiriki hai au ambao wanachangia kuboresha mijadala, au kutekeleza majukumu Fulani pengine ni wajuzi wa mambo ya teknolojia, pengine ni mwalimu anayeweza kuendeleza harakati ya darasa lake kuangalia blogu au kutumia nk, penginew ni project officer anayejua masuala ya kuandika maombi ya funds Fulani nk.

Pili, ni rahisi sana kwa mtu kufungua blogu na kuiwacha ilale. Kuna wale wasio na blogu ambao hawachoki kuchangia na kushiriki. Je yupi kati ya hawa – yule mwenye blogu yenye ujumbe mmoja wa kwanza katika miaka miwili au yule anayechangia kila siku – ambaye anahuisha ulimwengu wa blogu za watanzania?

Kuhusu utunzaji wa nidhamu: Unajua unaweza kumvua mtu uanachama wa jumuiya ya kublogu na akaendelea kublogu. Nadhani kuna nchi nyingine ambazo waliwavua uanachama wa jumuiya wale wanaondika matusi, wanaodhalilisha wanawake na kadhalika. Matokeo yake wale waliofukuzwa wameendelea kuandika wanayotaka bila kukinzwa na jumuiya.

Dawa ambayo inaweza kufanya kazi kwa mtu mkorofi ni kufuta maoni yake, huo ni wajibu wa lazima wa mwanachama anayetaka kutunza maadili (naomba kuwakilisha hapa juu ya roles and responsibilities of members japo hatujafika huko) au kumshitaki kisheria – shughuli ambayo ni ya kisayansi na inayoweza kuwa na gharama kubwa.

NAMI NAUNGA MKONO KUWA MWANAJUMUIYA SI LAZIMA AMILIKI GAZETI TANDO. Halafu katiba MUHIMU.
Ndugu wanablogu,kwa mtazamo wangu naona wengi wetu tumeegemea katika swala la nani mwanajumuiya,na kuachia mbali kuchangia katika katiba.

Swala katiba ni muhimu na nzito,katiba hiihii tusipokuwa makini itakuja kutushatiki tusipokuwa makini.Naona ni wakati wa kukaa na kutafakari kwa makini.

Napendekeza katiba iwe hivi:
1.Kila mwanajumuiya apewe nembo au namba ambayo itatumika kumtambulisha.
2.Njia moja wapo ya kuwaondoa vingozi ni kupitia au kutumia mfumo wa VOTE OF NO CONFIDENCE.
3.Katiba haitaruhusu blogu za ngono au picha zisizo kubalika katika jamii.
4.si lazima mwanajumuiya amiliki blogu.
5.blogu kutetea yatima kwa hali na mali.
jah bless.
Da Mija,nimefurahi jinsi ulivyo malizia maoni kwa kutumia JAH BLESS nami nakwambia JAH LIVE.
@Ndabuli. Niliposema Jumuiya hii yetu ni lugha tu. Naamini inaeleweka namaanisha nini.Au kuweka mambo sawa namaanisha wote tujiuhusishao na blgou hizi za Watanzania.

@Damija: naamini hata wenye blogu wanaweza kupotea.Nazungukia blogu nyingi tu sikuti wenyeji hata hivi sasa. Hivyo naamini tatizo hili litajitokeza tena na tena. Ila naamini majukumu yatatolewa kikamati. Hivyo si mtu mmoja atahusika katika utekelezaji. Mtu akipotea awe na blogu asiwe nayo ndio moja ya sababu za kumuengua katika jukumu hilo
Tunajadili sana suala la kutengwa, kutenga au kutenganisha, tunapozungumzia uanachama, lakini je, ikiwa wanachama watakuwa wote wenye blogu tu, mnadhani hiyo katiba haitawaweka katika makundi fulani fulani kulingana na malengo ya Jumuiya?

1. Tunahitaji Katiba kwa ajili ya kuweka UWIANISHO kati ya wanachama na sio kuweka USAWA. Hivi kiongozi atakuwa sawa na asiye kiongozi kweli kimajukumu na wajibu? Tusiwe kama wanasiasa jamani tunapojadili masuala ya msingi.

2. Tunahitaji kuwa na wanachama wasiokuwa na Blogi kwasababu kutokuwa kwao na blogi hakumaanishi kuwa hawana mchango mkubwa. Ni vyema tukajua kuwa kuna wana blogu wa aina mbalimbali; WAANDISHI, WASOMAJI, WADADISI, WACHANGIAJI MAONI, nk, na wote hawa wapo hatuwezi kukataa.

Suala hapa ni kuangalia kuwa tutakuwa na wanachama wa aina ngapi au makundi mangapi, katiba isiwaweke sawa watu hawa, bali iwaweke kwa uwiano wa kimajukumu, wajibu na mengine kama hayo.

Anayekaa jikoni akiungua moto, mwenye kumshikia nyama wakati anaikata kata, anayeandaa meza, anayenawisha watu mikono, kwangu wote hao ni wapishi isipokuwa tu kuwa wanatofautiana majukumu
@Msangi mdogo: siku kadhaa nimeshindwa kuingia katika blogu yako
Wanablogu wenzangu!

Mie naona kuwepo na muda wa kujadili mada ili tusiwe tunasubiri wali kwa muda mrefu baada ya kunawa. kimsingi tumeshakunbaliana kwamba jumuiya ianze na katiba itungwe. mada ya nani atakuwa/hatakuwa memba itajipa yenyewe kwenye kuichambua katiba.

Vile vile nakazia hoja yangu ya kuundwa kwa uongozi wa muda haraka sana ili mambo yaende mbele. ama sivyo tutagota 2008 tupo hapa hapa...
Namuunga mkono Michuzi
Ndugu wanablogu tunatumia muda mwingi sana katika swala moja,hatusongi mbele tunabaki palepale.

swala la nani ni mwanajumuiya litaamuliwa na viongozi watakao chaguliwa kwasabubu tumeona tunatumia muda kutatua swala hili.

Ndugu wanablogu naomba tusonge mbele.

Juma limekatika bado nani mwanajumuiya.
Jah bless.
lakii kumbuka hata viongozi wakichaguliwa wakaamua kuna baadhi ya watu watalalamikia maamuzi yao. Halafu nahisi kama Rasta Luhiamu hajachaguliwa, atakuwa mstari wa mbele kulalamika. Nabunia tu !
kweli Mzee Simon,nisipo chaguliwa nitashangaa sana na mimi huwa napenda kuwa muwazi Rasta huwa anasema ukweli katika jamii.Jah Bless.
Hee jamani, mkichoka na siasa na chokochoko basi pitieni kidongo kwa Mzee Mikundu mburudike na mikundu kia namna, angalieni msijiumize kwa punyeto:

http://mikundu.blogspot.com/
http://mikundu.blogspot.com/
http://mikundu.blogspot.com/