Muundo wa Uongozi uliokubalika.

Sunday 4 February 2007
Haya wanablogu. Ni wakati mwingine tena umewadia wa kutoa jibu lililokubakika katika mada tuliyokuwa tukiijadili. UONGOZI.

Kama wote tunavyojua, tulianza kwa kutafuta jina la Jumuiya, na kufuatia kuchanganua jinsi muundo wa jumuiya utakavyokuwa. Suala la muundo kwa ujumla ni pana na lenye vipengele vingi. Mwanzoni tuliliweka suala hili zima zima, lakini ikaonekana ingekuwa bora kulichanganua kulingana na vipengele vyake na kila kipengele kijadiliwe peke yake.

Mawazo yalikubalika, na kipengele cha UONGOZI kilikuwa cha kwanza kujadiliwa. Kipengele hiki kilipata majuma mawili mazima. Wachangiaji wametoa mawazo yao na hivi ndivyo ilivyokubalika:-

Jumuiya itakuwa na,

1. Mwenyekiti.
2. Katibu.
3. Mweka hazina
4. Kamati mbalimbali.

Katika kipengele cha nne hapo juu cha KAMATI, kutakuwa na kamati zifuatazo:-

1. Kamati ya harakati
2. Kamati ya teknolojia
3. Kamati ya Ufundi
4. Kamati ya picha
5. Kamati ya maadili na sheria
6. Kamati ya uenezi na uhamasishaji

Pamoja na hayo yote, pia kutakuwa na kitengo cha USHAURI na cha KAZI ZA KUJITOLEA.

Vilevile kuna jambo la maana sana lilijitokeza katika juma la majadiliano juu ya uongozi. Jambo hili ambalo Michuzi aliliibua ni juu ya kuwa na NEMBO na BENDERA ya Jumuiya. Jambo hili limekubalika na litatangazwa rasmi ili wajuzi wajitokeze na kuanza kulifanyia kazi. Lakini ikumbukwe ni kazi ya kujitolea bila malipo.

Wanablogu tunashukuru kwa ushirikiano wenu na kaeni chonjo kusikiliza mada itakayofuatia kuanzia juma la kesho.
 
© Blogu Tanzania | Tarehe: 2/04/2007 |

Maoni: 8

  Tarehe: 4 February 2007 at 23:11 Anonymous Anonymous Anasema:
maneno hayo mwanangu!
  Tarehe: 5 February 2007 at 19:42 Anonymous Anonymous Anasema:
Nina IMANI Watanzania tutahamasika sana na MAMBO haya.

Ndugu Macha niliwasiliana na Fred nikamwambia, maneno haya "kujifunza si lazima mtu akae darasani" Mtu/Watu wakitembelea popote kwa kutumia macho yao wanaweza kujifunza mambo mbalimbali, Mtu/Watu wakisoma vitabu, makala zenye kuelimisha (Nimesoma Mwananchi Jumapili jana nimeona makala yako Macha) Nikweli wa-Tanzania wengi bado tunasoma magazeti mabovu yasioelimisha, Umejitahidi kutoa mifano hadi ya Vitabu vitakatifu/vitukufu. MAPINDUZI NI LAZIMA.

Hii kitu mliotengeneza/Mnayotengeneza ni nzuri sana. Poleni kwa kazi kubwa mnayoifanya

Hapa mimi nitalia na kamati No.5. CHONDE CHONDE, MAADILI MAADILI MAADILI LAZIMA YAZINGATIWE.

Nasema hivi kwa sababu mimi ni miongoni mwa wasomaji wa blog malimbli na hakika huwa nakuwa na IMANI na yalioandikwa kwa 100%

Mimi ni mpenzi mkubwa wa KILIMO, tizameni blog ya MJENGWA, anacho adika na kuonesha (PICHA)nina amini na kufanyia kazi.

KILA LA HERI

Eti kuna taarifa kuwa MKURANGA-TANZANIA Gas imegunduliwa, na eti Gas ni dalili ya Mafuta!!!!!!

Mungu wangu hii ni NEEMA, lakini huyu G. Kichaka na TB sijui kama watatuacha!!! Tuwaombee Viongozi wetu wawe na busara hekima ya kuweza kuamini kuwa hata WATANZANIA WAKIHAMASISHWA WANAWEZA.

Nina hofu kubwa na huyu Kichaka, viongozi wetu wasione FAHARI ya kusifiwa na huyu bwana. Nina Mashaka hata na hii Misaada, Hizi ni PINGU.
Nakubaliana na Kamati zote.
  Tarehe: 8 February 2007 at 04:29 Anonymous Anonymous Anasema:
Sorry for my silence,
Hii ni kazi nzuri. Nafurahi sasa tunaelekea mahali. Nakubaliana na kila kitu. Pia nina swali.
1. Hii tovuti itakuwa sasa tovuti yetu au tununue (.org) au (.net)?
2. Kama ni tovuti yetu, rangi gani tutumie? Tuamue.
3. Tutahitaji pesa za shughuli mbali mbali?
4. Na kama tutahitaji, tutatumia njia gani? kila mwanachama atoe kitu au tutafute watu watakaotusaidia?

Tuanzie hapo.
Haya ndio mambo tunataka kusonga mbele Kaka ndesanjo,michuzi na wengine wote kazi nzuri tupo pamoja na niwakati wetu sasa kuonyesha,kuelimishana, kupashana taarifa kwa kutumia hii technolojia mpya. Tupo pamoja ndugu zangu
Hii itasaidia kutuunganisha wanablog wote na pia itakuwa chachu katika kuelimishana.
Inafurahisha kuona juhudi hizi. Tuko pamoja!
/maggid
Dada Mariam hapo juu kaja na mawazo aali kabisa. Naomba nijaribu kujibu kwa maoni yangu.

1. itakuwa tovuti yetu
2. nadhani rangi ya taifa itafaa
3. pesa ni muhimu ila nionavyo mimi tuanze kwa kujitolea. kwa mfno wewe Mariam najua ni bingwa wa It hivyo si vibaya ukatengeneza sampo ya tovuti yetu ambayo wataingia wanachama tu. kisha baada ya hapo tuone wanachama watavyochangia. weka pia link ya michango.
4.kuhitaji pesa halina mjadala. pia kutafuta wa kusaidia si vibaya.

kwa kuihitimisha naomba nitoe malalamiko kwamba tunasusasua sana na hili jambo kwani sijaona mchango wa washika ofisi wa chama chetu. pia ile mada ya katiba inahitajika wakati uongozi wa muda unawekwa madarakani kusimamia hiuyo katiba na hatimaye uchaguzi mkuu.

Kaka Ndesanjo naomba uanzishe mchakato wa kuchagua viongozi wa muda kuendeleza mbele azma yetu hii ambayo naona inapiga mark-time kwa muda sasa.

Naanza kwa kupendekeza majina kama ifuatavyo

1. Mwenyekiti - Ndesanjo Macha
2. Katibu - Makene
3. Mweka Hazina - Miriam ama Jeff Msangi

Kamati

1. Harakati - Da Mija
2. Teknolojia - MK
3. Ufundi - sina hakika
4. Picha - Maggid Mjengwa
5. Maadili na Sheria - Jeff Msangi
6. Uenezi na Uhamasishaji - F Mtimkubwa


Haya ni maoni yangu, nakaribisha kukosolewa.

Nawasilisha