Mija shija Sayi - Nafasi ya uweka hazina.

Tuesday 22 May 2007
Wasifu.

Umri: 34.
Utaalamu: Mtaalamu wa sanaa za jukwaani na za mikono.
Tabia: Msumbufu.

Sababu za kugombea nafasi ya hazina.

Ninaamini mwanamke ni mpangaji mzuri wa matumizi, na mimi ni mmoja wapo. Hivyo nataka kuisimamia jumuiya katika wakati huu wa awali na kuhakikisha haiyumbi wala kuyumbishwa katika kitengo cha hazina.
Zaidi ya hayo ninataka kushirikiana na wenzangu katika uundaji wa katiba ya jumuiya.

Naombeni Kura zenu.

http://www.damija.blogspot.com/
 
© Blogu Tanzania | Tarehe: 5/22/2007 |

Maoni: 26

  Tarehe: 24 May 2007 at 10:25 Anonymous Anonymous Anasema:
Nakuunga mmono kwa nafasi hiyo na hasa kwa kuzingatia mchango wako wakati wa kamati ya mpito ya kuunda shirikisho
  Tarehe: 25 May 2007 at 07:13 Anonymous Anonymous Anasema:
Mmmhh....:)
  Tarehe: 25 May 2007 at 07:55 Anonymous Anonymous Anasema:
Sasa kama ni mambo ya hazina, basi lazima tuchukue "fingerprint" zako!!

Haya, karibu kwenye kinyang'anyiro. Kuna watu wameniambia nao wataingia bado nawasubiri.
  Tarehe: 25 May 2007 at 12:46 Blogger luihamu Anasema:
Greetings,
haya uwanja wako.Hongera sana.
Pongezi kwa kuamua kugombea ndugu Mija, ila naomba nitoe wasiwasi kuhusu huo wasifu wa "Msumbufu".

www.jadili.blogspot.com
haya Da Mija,kila la kheri kwa kujitokeza.Nilikuwa nadhani Mija uko ktk 20's; i was planning to "bid" for you ila mmhhh...gap miaka kama 6 au 7 hivi,nitaweza kweli? i'm joking!
Hureee Da Damijo...we kwa kujitokeza tu mie tayari umeniwakilisha kama Mwanamke.../Mcchonge ninaubaguzi wa jinsia ...Bali ninakupitisha kwa kuwa umetuwakilisha...katika kupambana na mfumo dume...MIE I WISH...lakini bado kidogo nadhani nitawapokea awamu ijayo..inshaallaw!!
Kura yangu umeopata, ila alama aza vidole na picha zako inabidi nije nikupige.
Hahahahahaaaaa!!!!
www.blog.co.tz/mrocky
FATHER KIDEVU
Nilikuwa sijaona mfumo wa Uongozi, nimepitia kumbe ninanafasi amabyo ipo wazi nitagombea hiyo.
MJUMBE WA KAMATI YA PICHA
  Tarehe: 28 May 2007 at 16:00 Blogger ngono Anasema:
nakutakia kila la heri
  Tarehe: 30 May 2007 at 01:20 Anonymous Anonymous Anasema:
Kila la kheri Damija,
Hongera Da mija!Kura yangu unayo
Da mija eeh!Sasa wewe na Egdio mnanitia mashakani:-)!
  Tarehe: 10 June 2007 at 09:35 Blogger luihamu Anasema:
Duh afadhali kuna bwana mmoja nilikuwa namhofia sana,atleast now napumuwa.

Kura yangu unayo.

Kila la heri.

Jah Guidance.
msumbufu, natamani mmoja ajitoe kati yako na egidio, napata wakati mgumu kwelikweli. kila la heri
Chemshabongo, usihofu mambo yatakwenda murua kabisa. Kila la heri na wewe.
Hazina hiyo Da Mija! Nakuaminia mwanamke wa shoka
  Tarehe: 13 June 2007 at 08:16 Anonymous Anonymous Anasema:
Mmmm!

Mambo yanazidi kuwa mambo.

DaMija, unajua kwa nini unanishawishi kukupa kura yangu mpaka sasa?

Ni kwa sababu ya katabia kako ka USUMBUFU. Mi napenda sana watu wasumbufu, yaani wanaokereketwa na jambo fulani na wanaohakikisha kuwa kero hiyo inakwisha kabisakabisa.

Hongera.
  Tarehe: 14 June 2007 at 20:06 Blogger luihamu Anasema:
Da Mija,kamati ya maandalizi ikiamuwa kutumuia maoni kama kura wewe umeshapita lakini mechi bado binchi kabisa,mimi naanda mtandao wangu wakusimamia oparesheni Rasta.

Nuff Nuff Respect.

N.b BLOGU YAKO HAIJABADILIKA,KULIKONI?AU NDIO UNAANDA OPARESHENI SISTER DREAD.
  Tarehe: 16 June 2007 at 10:58 Blogger Mkina Anasema:
Da Mija,
uko tayari kwa kuchukuliwa alama za vidole na FBI? Haya kazi umepata. Jamaa zangu wanauliza mshiko wao wa kura namna gani na vipi utaanza kuweka fedha kwenye hazina yetu...unazo zako za kuanzia? Majibu unayo mwenyewe. Kila jema. Tusubiri tarehe 30 na nadhani matokeo mtayatoa lini sijui na je ni njia gani mtatumia kuhesabi kura? Naomba mtujibu tafadhali
  Tarehe: 17 June 2007 at 19:04 Anonymous Anonymous Anasema:
damija naomba uandike mapema utaratibu mzima wa uchaguzi mapema, tusije poteza haki ya kucgua au kaharibu kura
  Tarehe: 17 June 2007 at 19:06 Anonymous Anonymous Anasema:
Swali: Utatumia njia gani kutunisha mfuko wa jumuiya tukikupa nafasi ya uhazini?
Naomba jibu linaloshawishi
Pius
  Tarehe: 18 June 2007 at 19:25 Anonymous Anonymous Anasema:
Da'mija nimetoa comment kuhusu sheria ya uchaguzi wa tarehe 30/6/2007 naomba upitie pale kwenye kidirisha cha maoni.Naomba jibu la swali langu hapo juu.Bado natafakari kura yangu iende wapi.
Pius
Damija , Kama inawezekana , ongeza vitu vionekanavyo katika ukurasa huu wa kwanza, ili wagombea wote wawe wanaonekana ukiingia tu katika ukurasa huu wa kwanza wa Jumuwata.
hivi kama kuna 'faulo' kwenye uchaguzi huu tuataenda wapi kukata rufaa? na je, ukiwa mhazini utatunza vipi na wapi michango yetu?
  Tarehe: 22 June 2007 at 11:07 Anonymous Anonymous Anasema:
Damija,

Lazima apite. Mwanamke huyu ndiye anayeweza kusemekana kuwa most active katika safu ya mablogger wa kike. Pia alikuwa na maudhui yake ya wanawake wa shoka ambayo yalituhabarisha sana juu ya wanawake mbali mbali wa Afrika waliofanya mambo ya kumakinikia. Lakini siku hizi kanyamaza. Muda mrefu sasa hajawatoa wanawake wa shoka. Akirudi nitamuuliza kama kina Jide, Ray C, Klin, Cynthia Masasi, Aisha Madinda, Lilian Intanet na wenenguaji wengine, Amina Chifupa, Shyrose Bhanji, Mama Simbaulanga, Flavian Matata, na mamiss wengine kama nao pia ni wanawake wa shoka na kama ndivyo basi aanze kututundikia mavitu yao.

Kura yangu umeipata!

Masalaamia ni miye maridhiya,

F M Tungaraza.