SIMON MKINA- NAFASI YA MWENYEKITI

Wednesday 30 May 2007
WASIFU
Jina: Simon Martha MKINA
Umri: Miaka 36.
Utaalamu: Mwandishi, mchambuzi na mjasiriamali
Kazi ya sasa: Mwandishi
Uhusiano: Nimeoa na nimejaaliwa watoto wawili
Nafasi ninayogombea: Uenyekiti
Uraia: Mtanzania
Kuingia Blogu: mwaka 2004

SABABU ZA KUGOMBEA
Nimeamua kuwaomba wanablogu wenzangu kunipa fursa ya kuongoza chama chetu kwa lengo kubwa la kutetea uwepo wake, kutambulika, kuongeza wanachama, kutoa mafunzo anuai;ikiwemo ya kutambua haki zao na zaidi sana kuwa na ushirikiano mkubwa ndani ya utaratibu wa kublogu na hata masuala ya kijamii; kusaidia wakati wa shida na raha.
Mara nyingi umoja umekuwa ni nguzo muhimu katika kufanikiwa, nitafanya kila linalowezekana, kwa msaada wa wanachama wenzangu kuhakikisha chama kinakua kwa kuwa na wanachama wengi wa kada mbalimbali.

Nitatumia uwezo wangu wa kushawishi na kuhamasisha kupata njia za wazi katika kukisaidia chama kwa rasilimali ili baadaye kuwa na mtazamo wa kuanzisha miradi itakayosaidia, siyo wanachama tu, bali mama yetu Tanzania.
Katika kuyatekeleza hayo, ninaamini mimi ni DARAJA la kumfikia kila mwanachama na kumpa fursa ya kutambua nafasi yake katika kuendeleza na kuimarisha chama ambacho nitakuwa mstari wa mbele kuhakikisha kinasajiriwa na kutambulika na taasisi zote za serikali, umma, binafsi na mashirika ya kimataifa.
MATARAJIO:
Ninaamini kabisa kuwa nitapewa fursa ya kuwa kiongozi na kamwe sitabweteka na kuwa mtawala ambaye anaona dhamana aliyopewa ni bora kuliko wanachama waliomwezesha kuingia katika uongozi.
Nitawashirikisha wanachama wote kuleta maendeleo makubwa zaidi ya fikra komavu, uchumi, jamii na zaidi sana kuboresha taswira na nguvu ya mawasiliano huru ya blogu katika Tanzania.

AMINI:

MIMI NI DARAJA LA KUTETEA NA KUHAKIKISHA YOTE YANAWEZEKANA KUBORESHA AFYA YA MWILI NA AKILI KWA WATANZANIA WOTE KUPITIA VIONGOZI NA WANACHAMA WA BLOGU TANZANIA.
 
© Blogu Tanzania | Tarehe: 5/30/2007 |

Maoni: 25

Hongera kwa kujitokeza Mzee!Tukopamoja
  Tarehe: 2 June 2007 at 11:17 Anonymous Anonymous Anasema:
Simon,
hongera kwa kujitokeza. wewe ndio kati ya "mababu" wa blogu (ulianza mwaka 2004 kublogu).
  Tarehe: 4 June 2007 at 15:45 Anonymous Anonymous Anasema:
Tumekuona mzee, tuko pamoja na tunakuahidi mengi mazuri, ikiwemo kukuunga mkono, tunasubiri kuruhusiwa muda wa kuanza kukampeni, sijui utakuwa ni lini na njia gani zitatumika. Karibu sana mwasisi wa blogu unayeishi Tanzania
  Tarehe: 11 June 2007 at 03:20 Anonymous Anonymous Anasema:
Safi kabisa Mkina.Kila la kheri.
  Tarehe: 12 June 2007 at 18:30 Anonymous Anonymous Anasema:
Tumekuoa mzee, tunakupa peace na twakuhakikishia kila jema na ushindi tele siku ya siku. Unafaa
  Tarehe: 12 June 2007 at 18:32 Anonymous Anonymous Anasema:
Tuko pamoja, umepata. kwani kupiga kura ni lini na saa ngapi, mahali au ni humu humu kwenye mtandao, kama kuna ka-lunch ka ugali, kwa kuwa wewe ni mkandamizaji, naomba unipe kwanza kabla ya kukupa kura nawe
  Tarehe: 12 June 2007 at 18:33 Anonymous Anonymous Anasema:
Umepata mzee, unatisha na unaonyesha umakini, bado uko Dar na magazeti kongwe?
  Tarehe: 12 June 2007 at 18:34 Blogger Mkina Anasema:
Hapana mzee, siku hizo gazeti jipya la serikali linaitwa HabariLeo, nilitoka huko na nikaenda kuanzisha gazeti la serikali ya Zanzibar, walinipa ka u- expati mzee, tuko pamoja na aksante sana
  Tarehe: 13 June 2007 at 08:11 Anonymous Anonymous Anasema:
Bw Mkina

hongera kwa kujitokeza. umefanya jambo la maana.

Jamani wengine woote jitokezeni ili tuwe na uchaguzi mwanana.

kila la heri.
  Tarehe: 16 June 2007 at 09:20 Anonymous Anonymous Anasema:
Mzee Simon Mkina,
Tumekufikia, tunakuahidi ushindi mzee, kampeni shirikisha wengine pia na uwape na pesa za usafiri wa hapa na pale kuwanasa wapiga kura, jipe moyo, umepata.
  Tarehe: 16 June 2007 at 09:40 Blogger Mkina Anasema:
Jamani,
Nawashukuru wote waliojitokeza kunipa moyo na ahadi za awali kwamba watanipa uwezo wa kushiriki katika nafasi ya uenyekiti kushirikiana na wanablogu wote kuipa nguvu jumuia yetu inayotarajiwa kuwa pevu. Kila mwanablogu aliyejitokeza anastahili kupewa nafasi na ninaona wote wanafaa, lakini lakini atakayepatikana ashirikiane vyema na awe kijakazi wa wengine, siyo bwana mkubwa. Hapo tutafanikiwa na kufika mbali.Tuko pamoja. Hata hivyo, kabla sijasahau NAOMBENI KURA ZENU siyo ya kupiga kura Juni 30, 2007
  Tarehe: 16 June 2007 at 10:53 Anonymous Anonymous Anasema:
Kaka tumekuona na tumekusikia, mie nitakuwa kampeni meneja wako, fuko la mafeza liko wapi nianze kazi? Ahhh...tehetehe.
Umepata bwana nafasi, anza kujog na kupanga mikkati namna ya kuimarisha jumuia yetu
  Tarehe: 16 June 2007 at 11:06 Anonymous Anonymous Anasema:
Kaka tumekupata, lakini utawezaje kukandamiza maslahi yetu ya kifedha kama tuna matatizo
  Tarehe: 16 June 2007 at 12:15 Anonymous Anonymous Anasema:
Mabo ndiyo yameiva sasa, kila mtu anapaswa kufunga mkanda na kuanza kazi ya kutafuta watu wa kumuunga mkono ili jumuia yetu ipate viongozi bora na siyo bora viongozi. Tunahitaji watu wenye uzalengo, wasio na woga na wenye mwelekeo na maono ya kuleta maendeleo na nguvu ya jumuia yetu. Nadhani una nafasi, nakutakia kila jema na ukiona nafaa kukupa kura yangu basi nitafute, tuone tunafanya nini kuimarisha Jumuwata. Kila jema na ubarikiwe
  Tarehe: 16 June 2007 at 13:40 Blogger Mkina Anasema:
Nawashukuru wote mnaonipa moyo wa kuendelea kuwa nanyi katika masuala ya kuimarisha jumuia yetu ya wanablogu. Aksanteni nawatakia jema na uchaguzi wenye fanaka huku nikiendelea kusisitiza kura zenu kwa nafasi ninayoomba ya ueneyekiti. Tuko pamoja
  Tarehe: 16 June 2007 at 15:00 Anonymous Anonymous Anasema:
Mjomba nimekuona na nimepokea kwa furaha kujitokeza kwako, nakuhakikishia kura yangu, hesabu umekuwa kiongozi wangu. Unatisha na ninaona wenzako wataamua kujitoa kukupisha, ili upite bila kupingwa. Nakufagilia mtu wangu
  Tarehe: 17 June 2007 at 17:39 Anonymous Anonymous Anasema:
Ndugu Mkina,
Kabla ya kuuliza swali kwanza naipongeza taifa stars kwa ushindi muruwa jana usiku. Sina shaka Ghana tunakwenda.
Sasa swali:-
Una mkakati gani wa kuongeza idadi ya wanabblogu wenye blogu pindi utakapoukwaa uenyekiti wa jumuiya?Hapa naomba jibu linaloeleweka na si la kisiasa.
Kumbuka ni wengi tupendao kuwa na blogu lakini hatujajua kuanzisha blogu.Natambua juhudi za Ndesanjo katika hili.
Utafanyaje kusaidia wasio na blogu wawe nazo? Tupo WENGI tunaohitaji kuwa na blogu zetu wenyewe.Nomba jibu mzee.
  Tarehe: 17 June 2007 at 17:42 Anonymous Anonymous Anasema:
Sorry, namaanisha una mkakati gani wa kuongeza wana blogu wasio na blogu wawe na blogu?Yaanikuwasaidia kuzitengeneza.
Nimefafanua swali hapo juu
  Tarehe: 17 June 2007 at 17:44 Anonymous Anonymous Anasema:
Ukiniridhisha kwa jibu la swali hapo juu kura yangu utaipata mzee.
  Tarehe: 18 June 2007 at 10:55 Blogger Mkina Anasema:
Nakushukuru sana mjomba kwa kunipa swali la kwanza katika mchakato huu. Ingawa umeficha jina, nina imani una blogu au utakuwa nayo karibuni.
Njia nitakazotumia kuhakikisha wanachama wengi zaidi, kama nilivyoeleza katika maelezo yangu binafsi ya awali, ni kuhakikisha, Watanzania wengi wanakuwa na mahali pa kusemea, wakiwa na mawazo huru kabisa. Hili litawezekana kwa kuhamasisha idadi kubwa ya watu kwa kuandika makala kadhaa namna ya kuanzisha blogu (gazeti tando), kwa kuandika makala kwenye magazeti kama ambavo nimewahi kufanya kwenye magazazeti ya Uhuru, Mzalendo na HabariLeo, vipeperushi rahisi, kuweka njia rahisi katika blogu yangu binafsi na ya chama. Zaidi ya hapo nitahamasisha kwa kuweka matangazo madogo ya bure katika magazeti kuhamasisha watu kutembelea blogu ya chama ili kufahamu namna ya kuwa na blogu. Aksante na Naomba kura yako
  Tarehe: 22 June 2007 at 10:32 Anonymous Anonymous Anasema:
Damija,

Lazima apite. Mwanamke huyu ndiye anayeweza kusemekana kuwa most active katika safu ya mablogger wa kike. Pia alikuwa na maudhui yake ya wanawake wa shoka ambayo yalituhabarisha sana juu ya wanawake mbali mbali wa Afrika waliofanya mambo ya kumakinikia. Lakini siku hizi kanyamaza. Muda mrefu sasa hajawatoa wanawake wa shoka. Akirudi nitamuuliza kama kina Jide, Ray C, Klin, Aisha Madinda, Lilian Intanet na wenenguaji wengine, Amina Chifupa, Shyrose Bhanji, Flavian Matata, na mamiss wengine kama nao pia ni wanawake wa shoka na kama ndivyo basi aanze kututundikia mavitu yao.

Masalaamia ni miye maridhiya,

F M Tungaraza.
  Tarehe: 22 June 2007 at 16:58 Anonymous Anonymous Anasema:
Bwana Mkina,
Aminia baba'ke,
Ninakusalimia kwa staili hiyo nikiamini ni kijana mwenye nguvu za mwili na akili kuweza kuwa miongoni mwa viongozi wa Jumuwata.
Napenda namna unavyowagaragara hata viongozi wa serikali, licha ya kuwa jikoni. Tunakujua na twaomba iwe kweli isiw unazuga tu. Vipi mbona uliacha kutuletea mavitu ya namibia, au walikuziba mdomo
  Tarehe: 23 June 2007 at 10:28 Blogger Mkina Anasema:
Nakushukuru mzee anonymous kwa kunipa big five, hivi sasa nipo nimejaa tele kama tetele na ninasubiri kuwa teteleze siku ya kura ili tusaidiane kuimarisha jumuia yetu changa. Inshaalla'h tutafika na kuwa na nguvu siku chache zijazo endapo kila mmoja wetu atatimiza wajibu wake. Kila Jema na ninaomba uanzishe blogu ili uweze kuwa na sifa za kunipigia kura na maneno yako yako yawe kweli.
Aminia pia
  Tarehe: 23 June 2007 at 15:40 Anonymous Anonymous Anasema:
Mkina,
Nakupongeza kwa kujitokeza na kugombea nafasi ya juu kabisa katika jumuia mpya. Naomba kukuuliza, nimeona makala yako kwenye gazeti la HabariLeo na nyingine kwenye Daily News, ukihimiza namna ya kuanzisha blog, mbona sijaona kama umeeleza vyema maana nimefuata maelekezo na kukuta nakuwa blocked kwenye mtandao, sijui ni nini, nijulishe zaidi na unipe na ufafanuzi rahisi ili nianze na nipige kura. Kila heri na ubarikiwe
  Tarehe: 23 June 2007 at 18:10 Blogger Mkina Anasema:
Khamis,
Aksante kwa kuonyesha dhamira ya kujiunga uandishi wa magazeti tando. Ninakushauri utembelee ukurasa huu, kamati ya muda imeweka namna rahisi ya kujiunga na ulimwengu wa blogu. Kaka Ndesanjo ameeleza vyema, ukishindwa na kama uko Dar es Salaam naomba tuonane au nipigie simu: 0754 020880, ili tuonane na nikuelekeze kwa vitendo. Karibu sana na ninashukuru.