Waombaji wa nafasi za uongozi.

Saturday 12 May 2007
Katika kubooresha zaidi zoezi zima la uchaguzi wa viongozi wa Jumuiya, kamati imeona ni vyema waombaji wa nafasi hizo wawe wakituma maombi yao katika kamati na baadaye yatabandikwa katika ukurasa wa mbele.

Mambo ya kuzingatia katika uombaji:-

1. Tuma picha yako.

2. Wasifu wako.

3. Maelezo kwa nini unagombea nafasi unayoomba.

4. Nini unatarajia kufanya katika kuikuza Jumuiya.

Tuma maelezo kwa anuani hii mijasayi@yahoo.com
 
© Blogu Tanzania | Tarehe: 5/12/2007 |

Maoni: 7

  Tarehe: 13 May 2007 at 09:52 Blogger luihamu Anasema:
Ndugu wanablogu licha ya kuwa na hamu ya kuongoza jumuiya,nimeamuwa kujitoa kugombea nafasi yoyote ile.

Asanteni.
  Tarehe: 14 May 2007 at 07:41 Blogger luihamu Anasema:
Kumradhi,

baada ya kuona majina ya wanablogu maarufu Tanzania nikadhani sito weza kuchuana nao lakini baada ya kutafakari kwa kina zaidi ninaendelea na mpango wangu wa kuwania uwenyekiti.

Asanteni
  Tarehe: 14 May 2007 at 07:45 Blogger luihamu Anasema:
samahani kiti cha mwenyekiti.
  Tarehe: 16 May 2007 at 21:02 Anonymous Anonymous Anasema:
Wangombeaji mko wapi? Jitokezeni.
  Tarehe: 17 May 2007 at 06:03 Blogger Mjengwa Anasema:
Ni kweli Ndesanjo, tunawapongeza waliojitokeza tayari.
Mjengwa,
tukakuchukulie fomu? Naamini unafaa kuwa kiongozi.
Hongera kwa waliojitokeza