MUDA UMEONGEZWA.

Saturday 26 May 2007
Kutokana na watu kutojitokeza katika kugombea nafasi za uongozi wa jumuiya, uongozi wa muda umeamua kuongeza muda hadi tarehe 9 / 06/ 2007. Hii itakuwa ni siku ya mwisho ya kupokea maombi. Wanablogu tunaomba tujitokeze kwani madhumuni ya blogu si kutoa maoni peke yake bila kutenda yale tunayoyajadili. Umefika wakati sasa wa kutenda yale tunayoyakosoaga hivyo tujitokeze.
Fungua hapa upate maelekezo ya jinsi ya kutuma maombi.

Karibuni wote.
 
© Blogu Tanzania | Tarehe: 5/26/2007 |

Maoni: 9

  Tarehe: 28 May 2007 at 09:35 Blogger CM Anasema:
This comment has been removed by the author.
  Tarehe: 28 May 2007 at 10:04 Blogger CM Anasema:
Nafikiri kuna tatizo la publicity kuhusu huu uchaguzi. Baadhi ya wana-blog akina sisi ndiyo kwanza tunapata taarifa leo kwamba kuna uchaguzi.

Jambo la kufanya:
Watanzania kupitia blog zetu tuweke post inayohamasisha au kuweka link ambayo itawavuta Watanzania wengi zaidi kushiriki kwenye uchaguzi huu.Kama mimi nilivyoweka pale kwenye blogu yangu ya Yanga (www.yangatz.blogspot.com)

Kuhusu suala la mimi kugombea, naungana na MICHUZI katika kuwania nafasi ya kamati ya Utendaji (kama itakuwepo katika katiba mpya)

Naomba kutoa hoja.
  Tarehe: 28 May 2007 at 12:20 Anonymous Anonymous Anasema:
Nishukuru Mija kuja kunisalimu na kuniomba kujiunga humu. Wakuu nipo nanyi natazama lakini nina kompyuta ambazo nikitoa maoni zinagoma kuyaingiza. Napata mshtuko wa moyo hali inayonifanya kushindwa kutangaza harakati zangu katika kinyang'anyiro hiki kizito. Lakini nikuombeni wajumbe tupeane muda, nashawiksihika kutumia habari hii katika gazeti huku nyumbani. Nitarudi tena nikipata uwezp wa kuingiza maoni. Bonny Makene
Mimi naungana na wote waliochukua fomu, ninahamu ya kugombea lakini naomba kwa sasa nitoe nafasi kwa wengine lakini mimi nitakuwa mjumbe kama katiba itaniruhu kufanya hivyo.
Bt Father Kidevu. www.blog.co.tz/mrocky
  Tarehe: 28 May 2007 at 15:11 Blogger luihamu Anasema:
Nakumbuka Tarehe kamili ilipangwa ya wanablogu na wale si wanablogu kujitokeza kuwania nafasi katika jumuiya ya wanablogu Tanzania.

Tulipewa takribani wiki tatu kama sikosei.

Leo nimefunguwa blogu na kukuta siku zimeongezwa mpaka tarehe 9/6/07.

Napata mawswali mengi sana kwanza
1.waliojitokeza kabla ya muda kuisha hawanasifa au vipi?
2.Je ifikapo 9/6/07 na majina ni yale yale watazidi kuongeza muda?

Lengo letu nikuunda Jumuiya na sikuwa na watuwengi wa kuwania nafasi ya uongozi,labda kawa tuneweza kukaribisha na kamati pia tungepata watu wengi wa kuwania nafasi hizo.

Natumai kuongeza muda si KUAANDA WALE WANAOFAA KUONGOZA JUMUIYA.
ASANTENI.
  Tarehe: 28 May 2007 at 16:17 Blogger ngono Anasema:
kuongeza muda ni wazo zuri ila kutoa nafasi zaidi.
  Tarehe: 29 May 2007 at 01:30 Blogger Unknown Anasema:
Nikiwa kama mwana Blogu napenda
kuwapongeza wagombeaaa wote kwa
nafasi zao ...
nawatakia kila la kheri katika
kutumikia umma wa watanzania kwa
njiaa hii ya technologia....
daima
haki-hakingowi.blogspot.com
  Tarehe: 6 June 2007 at 07:50 Blogger luihamu Anasema:
Zimebaki siku tatu,natumai kamati ya maandalizi haita ongeza muda tena kwani tunapitwa na mambo mengi mazuri.

Jumuiya lazima isimame
Kamati za jumuiya lazima ziundwe ndani ya wiki moja na viongozi wa kamati hizo wachaguliwe ndani ya hiyo wiki moja,sisotaka kuonda tunachukuwa tena mienzi mitatu kuunda kamati au kuchaguwa viongozi wa kamati.

TIME IS NOT ON OUR SIDE,WE NEED TO MOVE VERY FIRST WHILE CHECKING OUR STEPS.

Jah Rastafarian.
  Tarehe: 14 June 2007 at 07:19 Blogger luihamu Anasema:
Hongera waler wote waliojitokeza kuwania ungozi wa JUMUWATA.

BAADA YA WANABLOGU KUJITOKEZA NA KAMATI YA MAANDALIZI KUTOA TAMKO NA TAREHE YA MWISHO,KAMATI YA MAANDALIZI BADO IMEKAA KIMYA.

NAELEWA KABISA KUNA UTARATIBU WA KUTENGENEZA DHANA ZA KUPIGIA KURA LAKINI NI VIZURI KAMATI YA MAANDALIZI ITUPE HABARI AU MWELEKEO.

NAOMBA KAMATI YA MAANDALIZI ITUAMBIE KINACHO ENDELEA NI NINI,HUU UKIMYA NA SHINDWA KUELEWA,LICHA YA KUKAA KIMYA KAMATI INAWEZA ANDAA SIKU YA KUPIGA KURA MWENZI WA SABA NA TUKUMBUKE KAMATI HAZIJAUNDWA BADO,SASA HEBU FIKIRIA TUNAWEZA KUTUMIA MWAMZIMA KUPIGA KURA.

LET US BE CREATIVE,LET US MOVE LIKE THE MCHALE NDANI YA SAA.

NAOMBA KAMATI YA MAANDALIZI ITOE TAMKO.