TANGAZO: Nafasi za uongozi katika jumuiya ya wanablogu Tanzania.

Sunday 6 May 2007
Jumuiya ya wanablogu Tanzania (Jumuwata) inatangaza nafasi za uongozi wa Jumuiya katika nafasi zifuatazo:-

1. Mwenyekiti

2. Katibu

3. Mweka hazina.

SIFA.

1. Awe na umri kuanzia miaka 18

2. Awe na mapenzi na harakati za blogu, si lazima awe na blogu.

Kazi kubwa ya mwanzo ya viongozi hawa itakuwa ni kuandika katiba ya Jumuiya na kuunda kamati mbalimbali kulingana na katiba itakavyokuwa ikisema. Kwa maelezo zaidi juu ya suala zima la uongozi wa jumuiya mnaweza kurejea hapa.

Zoezi hili liko wazi hadi tarehe 25 mwezi wa 5. Tarehe 26 itakuwa ni uchaguzi wa viongozi Nembo, tarehe 27 matokeo na ufunguzi rasmi wa jumuiya.

** Kwa kujiandikisha, tumia kidirisha cha maoni kuandika jina lako na nafasi unayotaka.

WOTE MNAKARIBISHWA.
 
© Blogu Tanzania | Tarehe: 5/06/2007 |

Maoni: 16

  Tarehe: 7 May 2007 at 17:38 Blogger luihamu Anasema:
Ndugu wanablogu.

Mimi Luihamu W.Ringo ningependa kuwania kiti cha Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanablogun Tanzania.
Mimi naona pia kama inawezekana Mtu kama Jeff Msangi , Ndesanjo , Damija wasokosekane katika uongozi huu wa mwanzo , ingawa nahisi wako bize.Nahisi kuwepo viongozi fulani wanaoweza kuipanguvu jumuiya katika kipindi hiki jumuhia imevaa nepi.Ni wazo tu!Luihamu asisahaulike kwasababu nguvu yake si ya soda .
Ni wazo tu!
Simon.Uweka hazina naona hiyo post inakufaa.
  Tarehe: 10 May 2007 at 18:50 Anonymous Anonymous Anasema:
Mh!Binafsi mimi yangu macho!Ndio kwa sababu ndio kwanza nimeanza kutumia blogu so i don't know more about blogs.Nnaendelea kujifunza mengi pamoja na kwamba mimi ni mwana blogu.Nawaomba wale wenye sifa wawe tayari kutufikisha kule tunakoelekea.But akina Macha wote wanastahili uongozi!
  Tarehe: 11 May 2007 at 19:43 Anonymous Anonymous Anasema:
Wapi mwanapicha maarufu Maggid Mjengwa?

HUYU naye tusimwache nyuma, huyu bwana anaonesha pia ana busara.

Hivyo iwapo ataonekana huku, tujaribu kuangalia kwani kazi yake kwa kiasi kikubwa inaelimisha jamii

5 5 5
Naomba nitoe mapendekezo kama ifuatavyo:

1. Mwenyekiti: Ndesanjo Macha
2. Katibu: Maggid Mjengwa
3. Mhazini: Da Mija

Kungekuwa pia na wajumbe 10 wa kamati ya utendaji
  Tarehe: 13 May 2007 at 09:48 Blogger luihamu Anasema:
Ndugu wanablogu niwakati muafaka na kuamuwa kujitoa kugombea nafasi yoyote.

Nimechukuwa uamuzi huu na kuwaachia wale wanaofaa kuendesha jumuiya.

Asanteni.
  Tarehe: 14 May 2007 at 07:44 Blogger luihamu Anasema:
Kumradhi,

Baada ya kusoma maoni ya wengi na kuingiwa na hofu ya kuchuwana na hawa wanablogu maarufu duniani nikachukuwa uamuzi wa kujitoa,lakini nimerudi tena kuwania kiti cha mwenyekiti.Kama wao wanaweza kwanini mimi nishidwe?

Asanteni.
  Tarehe: 15 May 2007 at 16:35 Anonymous Anonymous Anasema:
Ndugu wanablogu zoezi hili linaenda kea kusuasua sana.
Napendekeza.
Ndesanjo ajitokeze nafasi ya u cheamenakaungane na luihamu.Jeff akaungane na braza kitururu.da'mija ajitokeze uhazini.Hawa wandugu wanaombwa kujibu maombi yetu kwao.Wadau naomba kuwasilisha.
  Tarehe: 15 May 2007 at 16:36 Anonymous Anonymous Anasema:
Ndugu wanablogu zoezi hili linaenda kea kusuasua sana.
Napendekeza.
Ndesanjo ajitokeze nafasi ya u cheamenakaungane na luihamu.Jeff akaungane na braza kitururu.da'mija ajitokeze uhazini.Hawa wandugu wanaombwa kujibu maombi yetu kwao.Wadau naomba kuwasilisha.
  Tarehe: 17 May 2007 at 05:59 Blogger Mjengwa Anasema:
Wanablogu, mawazo yanayotolewa ni mazuri. Bado tuna siku chache za kutafakari.
Wanablogu mbona mmenilia kobisi juu ya wazo la kuwa na kamati ya utendaji ya watu 10. Mie natamani kugombea nafasi moja, ndo mana nakazia nafasi hizo. Naomba kujibiwa tafadhali
Kaka Michuzi,

Nafasi za uongozi wa kamati zitatangazwa baada ya katiba kuwepo, katiba itaundwa na viongozi wa tatu wa mwanzo yaani M/kiti, katibu na mweka hazina. Hii ndiyo sababu tunatafuta viongozi hawa kwanza.

Michuzi unaruhusiwa kugombea hizi pia usisubiri kamati.
  Tarehe: 21 May 2007 at 11:44 Anonymous Anonymous Anasema:
Jamani mboma watu hamjitokezi kugombea?,Mi nakubaliana na kitururu alivyosema wakati jumaiya ikiwa imevaa nepi, watu kama JEFF,NDESANJO NA DA'MIJA inabidi waje hapa kwenye kinyang'anyiro tuhangaike nao!
Au kama vipi,Luihamu uenyekiti umapita bila kuingwa.
Braza Kitururu ukatibu umepita kwa kishindo, bila kupingwa.
Na mimi ananymous uhazini nitapita bila kupingwa.Si nitakuwa peke yangu!
Sasa huu ndo uchaguzi gani wajameni!, Kama wa sisiemu wakati wa chama kimoja?
Kumbukeni tutakaowachagua watashughulikia swala muhimu la uandishi wa katiba na uundwaji wa kamati.
Shime shime mjitokeze tuwachague.
  Tarehe: 21 May 2007 at 11:49 Anonymous Anonymous Anasema:
Kina Makene,Chemi Che Mponda,Cherahani mko wapi?.Mbona humu ndani hamonekani?.Karibuni tujenge jumuiya.Pia mjitokeze kugombea.
  Tarehe: 28 May 2007 at 15:32 Anonymous Anonymous Anasema:
Katika Tanzania, wapo watu wenye kueza kujaza nafasi hizo lakini hawajajitokeza. Nakumbuka ukiacha macha, Mkina (anaitwa Simon Martha) ni miongoni mwa watu wanaoweza kugombea na hata kupata nafasi za juu. Anafaa kuwa mwenyekiti kwa kuanzia kwa maana amekuwa kwenye safu ya uandishi, uongozi wa vyama vya waandishi na zaidi anaweza.Tumshauri agombee na tumpe nafasi hiyo.