Jina lililokubalika.

Monday, 22 January 2007
Kamati ya muda inachukua nafasi hii kufunga mjadala juu ya JINA la jumuiya tunayotaka kuiunda ya wanablogu wa Tanzania. Mada ilikuwa hewani kwa muda wa juma zima, tunasema asante kwa wote waliochangia kwani wamesaidia kupiga hatua moja mbele. Hadi wakati huu tumekwisha kupata jina la Jumuiya yetu, ambayo kwa mawazo ya wengi wamependekeza iitwe "JUMUIYA YA WANABLOGU TANZANIA. Kamati ya muda haina budi kukubaliana na maoni ya wengi. Hivyo basi Jumuiya yetu itaitwa "JUMUIYA YA WANABLOGU TANZANIA.

Asanteni sana.
 
© Blogu Tanzania | Tarehe: 1/22/2007 |

Maoni: 5

mimi nimekubaliana na hilo
  Tarehe: 22 January 2007 at 01:16 Anonymous Anonymous Anasema:
Naunga mkono.
Tumepiga hatua moja. Bado ya pili, ya tatu, nne, na kuendelea.
Rasta feelin Irie Man coz i man can express my mind and I and I man a happy.Jah bless.
naunga mkono na kuwapongeza washiriki wote wa kufanikisha suala hili. Ni mchakato ambao umekuwa ukienda kama utani utani vile lakini muda si mrefu tutajua kuwa kumbe yale mambo ambayo huonekana katika jamii kama ya mzaha mzaha huwa ndio yana nafasi kubwa sana katika kuleta mabadiliko chanya.
Naunga mkono hoja na kuipongeza kamati kwa hatua hii muhimu.