Mjadala juu ya mada ya UONGOZI umeongezeka.

Sunday, 28 January 2007
Ndugu wanablogu, kutokana na unyeti wa suala zima la uongozi, kamati ya uongozi wa muda imekubali ushauri uliotolewa mwandani, kwamba muda zaidi uongezwe wa kujadili na kuipanga mada hii ya uongozi. Muda ulioongezwa ni juma moja, hivyo wanablogu tujitahidi kuutumia muda huu vizuri ili itakapofikia mwishoni mwa juma tuwe tumepata jawabu.

Pamoja na hilo, suala la kamati limejitokeza pia katika majadiliano yaliyopita. Suala hili ni muhimu sana ili kuunda uongozi uliokamilika. Hivyo basi katika kipindi hiki kilichoongezwa tutajadili pia kamati zitakazounda jumuiya yetu.

Hadi sasa kamati zilizopendekezwa ni pamoja na :-

1. Kamati ya maadili,
2. kamati ya ufundi na teknolojia
3. Kamati ya uhamasishaji,
4. Kamati ya Jamii (Watoto yatima),
5. Kamati ya sheria.

Bado tunahitaji michango zaidi ili kukamilisha mada hii.

Karibuni uwanjani.
 
© Blogu Tanzania | Tarehe: 1/28/2007 |

Maoni: 15

Mwenyekiti!

Kwanza smahani kwa kutohudhuria vikao vilivyopita bila kutoa udhuru. Kungekuwa na faini ya kukosa vikao ningetoa bila kusita, kwani sababu ya kutoujua mtaa ambayo ningetoa si ya msingi. Hivyo namshukuru Da Mija kwa kunielekeza.

Waama, baada ya salaam naunga mkono maamuzi yote yaliyopita, ikiwa ni pamoja na kuchagua jina; ambalo napendekeza litumike kwa ufupi. Vinginevyo jina bomba, linajieleza.

Mchango wangu katika kipengele hiki cha kuchagua kamati ni wa upnde wa mambo ya picha, kwani naona kamati karibu zote isipokuwa hiyo, zipo. Ama itaingizwa kwenye mojawapo ya kamati hizo? Hapana, mie naona kuwepo na kamati inayojitegemea ya picha, jina naomba wajumbe tujadili.

Nasema hivyo kuna mazoea ya kuundwa vyama vya kiuandishi bila kufikiria umuhimu wa picha. Hata kwenye vyombo vyetu vya habari vingi, kitengo cha picha huwa ni cha mwisho kufikiriwa, yaani inakuwa kama upendeleo ama bahati mbaya. Naombe tusielekee huko, kwani hivi sasa naona wapiga picha wapo kibao bloguni, japo nyanja zao ni za kiuandishi. Hivyo si vibaya kuanzisha Kamati ya Picha.
Naomba ufafanuzi kwenye kamati naona kama kamati namba 1 na 7 kama zinafanana au? Kuna tofauti gani kati ya kamati namba 2 (ufundi) na 4 (teknolojia). Naunga hoja ya Michuzi(kuwe na kamati au Kitengo cha picha).Nachangia!
  Tarehe: 29 January 2007 at 15:13 Anonymous Anonymous Anasema:
Nakubaliana na Michuzi. Pengine tunachoweza kufanya ni kuwa na kamati ya Blogu za Picha, Kamati ya blogu za video, na kamati ya Podikasti.

Au kabla ya kuendelea labda tujiulize hizi kamati kazi yake itakuwa ni nini? (sio lazima tuseme kazi zake zote ila jukumu lake kuu, kwa mfano, kamati ya picha, itakuwa nini?).

Kumetokea kosa kidogo kwenye kamati hizo kama ulivyosema Ndabuli. Kamati namba 1 na 7 ni hiyo hiyo.

Kamati ya ufundi na teknolojia, kama ulivyogusia Ndabuli, naamini ni kamati moja.

Je, kwanini kamati ya maadili na sheria isiwe moja?

Kamati ya Jamii (watoto yatima) naona tutafute jina ambalo litabeba upana wa kamati hii. Kamati hii inaweza kujihusisha na masuala ya kijamii kama watoto yatima, magonjwa, masuala ya elimu, na hata masuala mengine ambayo yanaweza kuingia kwenye kundi la kisiasa (kwa mfano, jumuiya yetu inaweza kufika wakati ikawa inatoa semina kwa wanasiasa na wabunge jinsi ambavyo wanaweza kutumia blogu kama njia ya mawasiliano na ujenzi wa demokrasia shirikishi).

Nashauri tuiite Kamati ya Harakati (bila kutaja aina ya harakati yenyewe).
Ufundi na teknolojia viko karibu karibu. Lakini mtumiaji au mtu anayetathmini teknolojia fulani anaweza asiwe fundi. Kwa mfano teknolojia ya simu mpya apple wengi wameitathmini ambao hawana ufundi.

Wengi tunaweza kutumia interface au teknolojia fulani - lakini ufundi wa kurekebisha au kukochakocha inapobidi, sharti aitwe fundi, mfano mambo ya code au utatuzi wa matatizo ya aggregator kama yakitokea nk. kuna ufundi maalum.
Haidhuru, naunga mkono, teknolojia na ufundi ni mtu na ndugu yake.

Kamati ya jamii kwa mtazamo wangu itakuwa kama mwavuli wa shughuli nyingi. Ningeshauri iitwe kamati ya maendeleo ya jamii.

Naamini pamoja na mambo mengine, kwamba lengo la jumuiya hii ni kuipa nguvu jamii - hata kama njia itakuwa kwanza kwa kusaidia. Ili kuweka wazi kwamba lengo siyo charity bali kumpa mtu uwezo - jina muwafaka ninavyoona ni:
kamati ya maendeleo ya jamii.
Nakubaliana na wazo la Mzee Ndesanjo.Kamati ya Harakati.Safi sana.
Nimerejea kusoma vyema ushauri uliotolewa awali na Ndesanjo:

"Nashauri tuiite Kamati ya Harakati (bila kutaja aina ya harakati yenyewe)"

Poa pia.
  Tarehe: 30 January 2007 at 10:06 Anonymous Anonymous Anasema:
Nakubali uchambuzi wa Mwandani kuhusu teknolojia na ufundi. Ingawa hawa ni ndugu, kila mmoja ana umuhimu wake na kuna tofauti fulani baina yao. Naunga mkono pendekezo lake la kuwa hizi ziwe kamati mbili tofauti.
  Tarehe: 31 January 2007 at 10:40 Anonymous Anonymous Anasema:
Naunga mkono harakati zinazoendelea. Hata hivyo, nadhani kamati tulizonazo zinajitosheleza, labda ikiongezwa ile aliyopendekeza Bw Michuzi, ya picha, basi JUWATA itakuwa imekamilika.

Nadhani tuishie hapo kwenye kamati ili tusije kuwa na kamati kibao ambapo maana yake itakuwa kuwa na viongozi lukuki. Sidhani kama tunahitaji kuwa na chombo chenye urasimu mkubwa, maana kadiri unavyoongeza kamati ndivyo unavyoongeza urasimu wa kushughulikia mambo. Baadaye tutapata utata kuwa suala fulani, je lishughulikiwe na kamati ipi hasa, maana itakuwa vigumu kusema jambo hili linaangukia kwenye kamati fulani. Kutakuwa na mambo ya namna hiyo.

Hivyo, naomba kuwakilisha kuwa kamati zilizopendekezwa tayari zinatosha, tutazame yanayofuatia.

Ciao!
Habarini wana blog japo leo ni mara yangu ya kwanza kuzuru eneo hili baada ya kuhamasishwa na kaka NDESANJO...kwanza naomba awepo kwenye kamati ya uhamasishaji sababu uwezo huo anao

pili nakubaliana na hizo kamati zilioundwa Especial hiyo ya Kamati ya jamii....hapo naona mmetoa watoto yatima kama mfano ...lakini naomba tusikwamie tu hapo kwenye watoto yatima...maana yapo meengi katika jamii ya kuangalia...kina mama na saratani ya matiti, wajane, nk

ni hayo tu.....naunga mkono hoja asilimia 101
Naunga mkono mapendekezo ya kamati hizo hapo juu.Labda tunachoweza kuongeza ni kwamba ili tusije kuwa na utitiri wa kamati,basi tupanue majukumu ya kamati zilizopo.Tatizo la kuwa na kamati nyingi sana ni katika utendaji.
Baada Ya kusoma mapendekezo ya wachangiaji hapo juu naugana na wengi katika haya:
Tuanze na Kamati chache ambazo zitakuwa na majukumu yaliyopanuka ,kwa sababu huu ni mwanzo ni vyema kuwa na kamati zenye watendaji,na kama mchangiaji mmoja alivyosema kuondoa ukiritimba,na vilevile tuangalie wajumbe amabo watakuwa tayari na muda wa kuifanya hiyo shughuli maana kunaweza kuwa na kamati zisio na wanakamati au wanakamati kutokuwa na muda lakini kama baadhi ya majukumu yakiwa yameunganishwa kwenye kamati moja ni rahisi kuepukana na hilo.Hapo jumuia inapokuwa na kupata uzoefu yataonekana mahitaji mengine ambayo yanaweza kujadiliwa kama ni kuundiwa kamati au kuunganisha kamati. Nauliza vipi nafasi ya washauri (kwenye swala lolote)
Kamati zimetosha naomba tuingie katika mambo mengine yanayo tusubiri.Hii Kamati ya HARAKATI ninaiangalia kwamakini sana,nimuhimu mwanablogu kujitoleo na kutuoa habari kamili kutoka katika mikoa iliyo athirika na watoto yatima.Jah Bless I and I.
  Tarehe: 1 February 2007 at 20:20 Anonymous Anonymous Anasema:
Wazo la kupanua majukumu ya kamati badala ya kuongeza kamati nakubaliana nalo kwa asilimia 100. Ni sahihi kusema kuwa kuwepo kwa kamati nyingi kutaleta usumbufu na matatizo mengi kiutendaji. Hivyo kamati ziwe chache na majukumu yagawanywe kwenye hizo kamati. Siku zinavyokwenda, tutakavyokuwa tunajifunza zaidi jinsi ya kuendesha jumuiya ya aina hii, na mambo mengine kujitokeza, huenda tukaona umuhimu wa kuongeza kamati (au hata kuzipunguza zaidi au kuziunganisha).

Hivyo naunga mkono wazo la kuwa kamati zisiongezwe.

Suala la Ndabuli kuhusu washauri. Sikuwa nimefikiria kuhusu kuwepo kwa washauri. Nadhani sio wazo baya. Binafsi nadhani washauri sio lazima wawe wanablogu. Mnasemaje?

Kama wazo hili litaungwa mkono, je tunataka washauri wangapi? Ni yapi majukumu yao ya msingi? Huenda majukumu yao yataandaliwa na viongozi watakapochaguliwa wakishirikiana na wanakamati.
Naunga mkono hoja zilizotolewa.Lakini hivi wanablogu wenyewe si ni miongoni wa tunaoshauriana?Basi naona tusiwe na washauri wengi ingawa nadhani ni muhimu kuwa na baadhi ingawa naona katika kipindi hiki itakuwa vigumu kutaja namba.Lakini tusimsahau mshauri wa mambo ya sheria. Halafu katika maswala ya washauri naonaingekuwa ni ushauri tuutakao ndio utuongoze kuchagua mshauri.Tukitaka kuwaiga mfano wanablogu wa Chile basi tupate ushauri wa-Chile.Tukitaka ushauri wa kumuengua mwanablogu aliyedakwa na sheria wakati tunajua Mmisri aliyefanikiwa kujiengua kutoka katika tatizo hilo basi si vibaya kupata kutoka huko..nk.
heheheheeee mmeniacha nyuma tokea mnaanza, tafadhalini naminawaunga mkono na miguu yoote karibu pia mnitembelee plz naona mapendekezo yeenu yoote ni mazuri ahsante Da'mija 4 that, plz dnt leave me behind