Muundo wa Jumuiya ya Wanablogu Tanzania.

Monday, 22 January 2007
Baada ya kupata jina la Jumuiya yetu, sasa tunaingia hatua ya pili. Juma hili tutajadili suala zima la MUUNDO wa Jumuiya yetu. Hapa tutajadili vitu kama:-

1. Uongozi,
- je tunataka uongozi wa Jumuiya uweje? kuwe na Mwenyekiti au Rais,
- Kuwe na idara au wizara zozote?
- Kuwe na uongozi wa muda au wa kudumu?
- Viongozi watakuchaguliwa vipi? n.k

2. Wanajumuiya,
- Je mwanajumuiya ni nani? mtu yeyote mwenye blogu au hadi aombe kuingia katika
Jumuiya?
- Kuwe na taratibu zipi za mtu kujiunga na jumuiya? (sifa)
- Kuwe na taratibu zipi za mwanablogu kutolewa katika Jumuiya?
- Je kuna haja ya kuweka mipaka yoyote ya kinidhamu kwa mwanablogu? ipi?

3. Katiba.
- Je tunahitaji kuwa na katiba?

Hivyo basi wanablogu, juma hili hayo ndiyo tutakayoyajadili, kumbuka hivyo ni vidokezo tu, kama utakuwa na jambo lolote la nyongeza katika hayo basi usisite kuongeza.

Hatua hii ni muhimu sana kwani ndiyo itakayotupelekea kujenga katika yetu kama tuahitaji kuwa na katiba.

Karibuni tena uwanjani.
 
© Blogu Tanzania | Tarehe: 1/22/2007 |

Maoni: 9

  Tarehe: 22 January 2007 at 17:11 Anonymous Anonymous Anasema:
Ngoja nifungue njia:
Ningeshauri tuwe na vyeo vikuu vitatu ambavyo vitakuwa ndio msingi wa uongozi: mwenyekiti, katibu, na mweka hazina.

Kisha tuwe na idara au wizara au vitengo vyenye viongozi wake: teknolojia (hawa watahusika na suala la tovuti yetu na mambo mengine yanayohusu teknolojia), uenezaji/uhamasishaji, n.k.

Nahitaji kufikiri zaidi kuhusu aina ya idara/wizara au vitengo ambavyo tutavihitaji.

Au tunaweza kuwa na mwenyekiti, katibu, mweka hazina kisha tukawa na kamati mbalimbali (kamati ya teknolojia, kamati ya fedha, kamati ya uenezaji, n.k.).
Naona hatua ya pili imeanza kwa kasi sana. Hivyo vipengele vya MUUNDO wa Jumuiya naona vimekuwa vingi sana kuvijadili vyote kwa wakati mmoja. Kwa vile muda wa kujadili ni wiki ninashauri hivyo vipengele viwe vichache ili tuweze kuchangia kiufanisi.Kwa mfano wiki moja kipengele namba 1. UONGO(-)ZI kijadiliwe halafu tuhamie kipengele cha pili.Wakati wa kujadili cha kwanza wakati huohuo wanablogu wanajitayarisha na mjadala unaofuata. Natoa ushauri.
Jamani tunasemaje juu ya ushauri wa Ndabuli?
Mimi nakubaliana na Ndabuli
  Tarehe: 23 January 2007 at 13:26 Anonymous Anonymous Anasema:
Naunga mkono hoja ya Ndabuli. Tuanze na uongozi.
Alichokisema Ndabuli ni kweli kabisa
Ni kweli kuchaguwa viongonzi si kazi kama kuunda jumuiya.

Ndugu wanablogu mimi Ras Luihamu naomab kura zenu.
  Tarehe: 27 January 2007 at 21:32 Anonymous Anonymous Anasema:
Luihamu: lazima kwanza tukubaliane nafasi za uongozi na mambo mengine kabla ya kuingia kwenye hatua ya kuomba kura na kuchagua viongozi.
Sawa Mzee ndesanjo.