Uongozi wa Jumuiya ya wanablogu Tanzania

Tuesday, 23 January 2007
Kutokana na ushauri wa mwanaharakati Ndabuli na wengine wote waliounga mkono hoja aliyotoa, (fungua hapa usome alichokisema) kamati ya muda imeona ni kweli kabisa kwamba mada hii ya uongozi ni nzito na yenye vipengele vingi kuweza kujadiliwa yote katika juma moja. Hivyo basi mada hii tunaiweka huru ndani ya majuma manne au zaidi kulingana na vipengele vyake. Hadi sasa hivi tunavipengele vinne vikuu ambavyo ni UONGOZI, UANAJUMUIYA, KATIBA na IDARA kila kipengele kimepewa juma zima kujadiliwa.

Haya, bila kuchelewa tutaanza na kipengele cha UONGOZI.

- je tunataka uongozi wa Jumuiya uweje? kuwe na Mwenyekiti au Rais,
- Kuwe na uongozi wa muda au wa kudumu?
- Viongozi watakuchaguliwa vipi? n.k

Uwanja uko wazi karibuni.

*Shukrani sana Ndabuli. Wanablogu tusihofu kutoa ushauri popote pale tunapodhani panahitaji kuwekwa sawa. Maendeleo hayaji pasipo kubadilishana mawazo.
 
© Blogu Tanzania | Tarehe: 1/23/2007 |

Maoni: 21

1. Napendekeza kuwe na mwenyekiti, katibu na mweka hazina.

2. Pia uongozi napendekeza uwe ni wa muda na si wa kudumu. kwa kuanza tungeanza kwa mwaka mmoja.

3. kuhusu jinsi ya kuchagua viongozi, wawe wanapendekezwa na wanablogu wote, wale watakaopendekezwa na watu wengi zaidi itabidi wapewe ka-mtihani ka kulielezea jambo lolote litakalopendekezwa, linaweza likawa linahusiana na Uchumi, Siasa, elimu au jambo lolote. Sasa yule atakayeshusha vitu zaidi ndiye atakayechukua nafasi.

Hayo ndiyo mapendekezo yangu.
mimi na kubaliana na Damija asilimia mia.
Nimestuka!Ninapunguza asilimia kutoka katika aliyopendekeza Damija. Kutoka katika mtihani alio shauri,elimu aliyonayo mwanablogu naona isiwe kigezo.Mtihani kwa mgombeaji kwa ujumla usiwepo. Atakapo jitokeza yoyote, kama wanablogu wanaamini anafanikisha jumuiya itakavyo, na wanablogu wanaamini kwa kura ambazo ziwe ni kawaida kupigwa kwenye blogu ya jumuiya, basi anafaa, inatosha. Lakini wapewe kipaumbele wanao jitokeza kama Rasta Luihamu, ambao kwanza wananguvu ya kujituma, kwa muda.Lakini Watakao pendekezwa na wanablogu wakubaliwe kwa muda . Naamini kwa sababu hii ni kujitolea, tuwe na muda tofauti kwa wajitoleao na wapendekezwawo. Kwa sababu wajitolewao wana mchango tofauti na wajitoleao.
Naamini anayeweza si lazima awe msomi. Ni mawazo yangu tu.
Safi sana hilo la wanaojitolea na wenye nguvu za kujituma.
  Tarehe: 25 January 2007 at 13:59 Anonymous Anonymous Anasema:
Kwa mawazo yangu, sio vizuri uongozi wa jumuiya ukawa ni kundi dogo la watu wawili, watatu. Hivyo naona ni sawa kabisa tukiwa na mwenyekiti, katibu, na mweka hazina. Pengine tunaweza kufikiria pia suala la makamu mwenyekiti, katibu mkuu msaidizi...kitu kama hicho kuwasaidia hawa mabwana kazi.

Halafu ili kupanua wigo wa uongozi na usambazaji wa madaraka ninapendekeza tuwe na kamati mbalimbali kama vile Kamati ya maadili na taaluma, Kamati ya Uenezaji/Uhamasishaji, Kamati ya teknolojia na kamati nyingine ambazo tunaweza kuona zinafaa. Katiba inaweza kutoa mwanya kwa uongozi kutangaza kamati wakati wowote iwapo kutakuwa na ulazima.

Hoja yangu ni kuwa tukianzisha kamati tutakuwa tumegawanya madaraka na pia kufanya uongozi kuwa mpana zaidi badala ya kuwa kundi la watu wachache.

Wachaguliweje? Wanachama watangaze nia za kutaka uongozi na sifa zao na visheni walizonazo kuhusu jumuiya hii. Kisha wanachama wengine tupime uwezo wao na mwelekeo wanaotaka jumuiya hii ielekee halafu tuwapigie kura.

Kupendekezwa au kujitolea: Sioni ubaya kama wanachama watakuwa na uwezo wa kupendekeza. Ila pia mwanachama awe na uwezo na haki ya kukataa kutokana na sababu atakazozitoa au sababu binafsi ambazo hatazianika kwa kadamnasi.

Kamati: pengine viongozi wa juu ndio waunde kamati na wajumbe wa kamati hizo?
hiyo ni nzuri ila katiba itoe mwanya wa kupiga kura ya kutokuwa na imani na uongozi au kiongozi.ili pale mathalani akiwa ras luiham kachemka tunamwonyesha mlango....
Wanablogu kutoka Tanzania,tujipongeze kwa hatuwa kubwa tuliyopiga.Asante.

DaMija hiyo mitihani nani atasahihisha?

Mzee Simon Kitururu,mimi nipo tayari kupewa nafasi yoyote ile katika jumuiya yetu,asante kwa kunipendekeza.

Mimi Rasta Luihamu Ringo napendekeza tuwe na Mwenyekiti,wa muda pili ningependa tupige kura safi kura za kweli sio kwasababu ya majina au maslahi.

Mwenyekiti na makamu mwenyekiti makao yao makuu yatakuwa Tanzania Dar Es Salaam.
Napendekeza makamu mwenyekiti Da Mija Shija,ninauhakika nitafanya nea kazi vizuri.

Mapendekezo ya Mzee Ndesanjo nakubaliana nayo.

Ndugu wanablogu naomba kura zenu,mafanikio ya kublogu nisawasa ni imani dhatiti ya Rastafarian,niwakati muafaka wakumpa Rasta uongozi katika jamii yetu.

Napendekeza.
  Tarehe: 26 January 2007 at 12:06 Anonymous Anonymous Anasema:
Ingekuwa bora zaidi tungesikia mawazo zaidi. Hata wanaounga mkono ni vyema wakasema kuwa wanaunga mkono.
Kuhusu Uongozi
1.Kuwepo na Mwenyekiti
2.Katibu
3.Mweka hazina
4.Mratibu Mkuu.Naomba nipendekeze majukunu yake:-
a)kuweka bayana mipaka ya maoni.
b)Lugha fasihi na Fasaha(Isiyo na matusi au utata)
c)kuangalia mwelekeo maoni (wa wakati)hasa kuhusiana na maoni/hoja aua Ushauri.
Kwa ujumla mawazo yote yaliyotolewa hapo juu nayaunga mkono.Nayaunga mkono nikiamini kwamba katikati ya mawazo hayo mengi tunaweza chagua yanayoendana zaidi na aina ya jumuiya tunayoitengeneza ili tupate kitu bora kabisa.

Labda kwa kuwa specific zaidi naunga mkono au napendekeza wazo la kuwa na uongozi usio wa kudumu.Wanaotaka uongozi wajitokeze na pia wanaweza kupendekezwa ila,kama alivyodokeza Ndesanjo,wawe na uhuru wa kukataa.

Naamini kuna umuhimu wa kuwa na mwenyekiti,katibu na mweka hazina(kama zitakuwepo hazina) na pia kamati ndogondogo kama za maadili,tekinolojia na muungano wetu wenyewe(ikumbukwe kwamba tumetapakaa dunia nzima na kazi hii akiachiwa mwenyekiti na katibu wake tu itakuwa ngumu.Kwa maana hiyo tunaweza kuwa na co-ordination commitee(samahani kwa kutia kizungu)

Pamoja na kwamba blogs ni jamii huru na inayojaribu kumshirikisha kila mtu,suala la uwezo alionao kiongozi(sio kwa kuzingatia elimu wala fedha wala alipo)ni muhimu.Lazima mtu aonekane kweli ana uwezo wa kuongoza jumuiya.Kwa maana hiyo lazima tuwe na vigezo fulani fulani huku tukiwa makini kwamba habaguliwi mtu.
Ni hayo tu kwa sasa.
Inasikitisha kidogo kuwa sio watu wengi wanaojitokeza kuchangia mawazo.

Nakubaliana na yaliyosemwa na wenzangu hapo Juu.
Mengi yameshapendekezwa. nayaunga mkono kwa silimia kubwa.

Nashauri tuwe na uongozi kama wa asasi nyingine kwa kuanzia mpaka pale itakapoonekana haja ya kubadili mfumo wetu. uongozi wa kipindi cha mwaka mmoja mmoja naona ni mzuri. Sina hakika kama tuwe na kikomo kiongozi achaguliwe kwa mihula mingapi ya mwaka mmoja mmoja.

1. Mwenyekiti
2. katibu
3. mweka hazina
4. kamati mbalimbali zitakazoongozwa na ma-coordinator watakaoshirikiana na mavolunteer watakaojipendekeza kusaidia kamati hizo.

Kamati nazopendekeza kwa sasa ni za pr/uenezi/uhamasishaji umma; kamati za kiufundi; pia kamati ya maadili/sheria.

Sina la zaidi bali kuunga mkono hoja zilizotolewa na wengine hapo juu.
NB: Kutokana na uzito wa shughuli hii, naomba tuongeze wiki kabla ya kufikia uamuzi.

hasa kuhusiana na kamati mbalimbali ningependa tufikirie kamati. Ndesanjo umegusia: "Kamati ya teknolojia na kamati nyingine ambazo tunaweza kuona zinafaa"

nakumbuka Luihamu pia alikuwa ameguswa na suala la watoto yatima hapo nyuma...

Katika uongozi mnafikiria kuwe na kamati zipi?
Naunga mkono mwandani alivyo shauri. Tuongeze wiki kwenye swala hili
  Tarehe: 27 January 2007 at 21:14 Anonymous Anonymous Anasema:
Hata mimi nakubali tuongeze muda. Basi kama mmoja wa viongozi wa muda, suala hili naahidi tutalijadili na kutangaza mara. Wiki moja zaidi itatosha.

Tujitahidi kujibu maswali yanayoulizwa na wachangiaji. Kwa mfano, Mwandani kauliza kuhusu kamati. Inaelekea kuwa wengi wanakubali tuwe na viongozi wakuu watatu (mafiga). Kisha tuwe na kamati. Kamati hizo ni zipi? Ndio swali la Mwandani.

Napenda pia wazo la Jeff la kuwa na kamati ya kutuunganisha kutokana na ukweli kuwa tumezagaa kila kona (tuna wanablogu India, China, Uswidi, Australia, Tanzania, Uskoti, na wengine wanakuja).

Suala la watu wa kujitolea kufanya kazi mbalimbali naona litabidi lianze kukumbatiwa mapema maana huko mbeleni kutakuwa na kazi nyingi zitakazohitaji watu kujitolea. Utamaduni huu tuanze kuujenga mapema.

Mweka Hazina: mwanzoni huku pengine hazina itakuwa haina jambo. Ila mbeleni nadhani masuala ya hazina yanaweza kuwa na umuhimu (huenda tukawa na kitengo cha kutetea wanablogu kisheria, au tukahitahi fedha kwa mambo fulani fulani yahusuyo siku ya blogu Tanzania, n.k.). Ninachosema ni kuwa tuweke cheo hiki maana naona kitahitajika huko mbeleni.
Naunga mkono hayo yote yaliyosemwa hapo juu.Naomba tuwe na kamati ya watoto yatima kweli kabisa nami najitolea kuwa mwanakati kama sito chaguliwa katika uongozi wowote ule katika jumuiya ya wanablogu Tanzania.

Hili swala la watoto yatima nijukumu letu sisi wanablogu kilivalia njuga.

Naomba kuuliza uongozi wa muda, hawa wanablogu wa tanzania ambao hawachangii maoni mtawachukulia hatua gani?Naomba kujibiwa.
Naunga mkono yote yaliyosemwa isipokuwa kipengele cha mfumo wa uongozi, naomba kuwepo na

1. Mwenyekiti
2. Katibu
3. Katibu Mipango
4. Mhazini
4. Kamati mbalimbali na viongozi wake kama hapo juu

Namaanisha tukiweka kiongozi Rais demokrasia huenda ikaleta utata kwani Rais anaweza kujiamulia ama kauli yake ikawa ya mwisho hata kama kuna manung'uniko

Vile vile tuwaze ama tutoe tenda kwa ajili ya nembo ya chama na bendera pia. Hivyo wadau walio wataalamu kwa hilo watusaidie, kisha kura ipigwe kukubali ipi
  Tarehe: 29 January 2007 at 15:16 Anonymous Anonymous Anasema:
Wazo la Michuzi la kutoa tenda ya nembo ni zuri sana. Najua, ndugu yetu wa myafricatoday.com ameshaanza kutengeneza nembo ya kikusanya habari. Nadhani tukifika wakati wa kujadili kikusanya habari, itabidi suala la nembo yake litazamwe na jumuiya.

Kwahiyo zaidi ya nembo ya kikusanya habari, tunahitahi basi nembo ya jumuiya. Naamini viongozi wa muda wazo hili tutalipitisha rasmi na kulitangaza. Ngoja tuwasiliane. Tuna watu wana vipaji, waje hapa tuhangaike nao!
Kimsingi nakubakliana na mawazo mbalimbali yaliyotolewa na wachangiaji wote walionitangulia. Ila kidogo natatizwa na wazo la Luihamu kuwa mwenyekiti na katibu wawe na makao makuu dar es salaam Tanzania. Natatizwa na hili kwasababu sijajua kuwa Jumuiya yetu itakuwa ya mtandaoni au itasajiliwa mahali (kwa walioshiriki mkutano wanakumbuka juu ya hili).

Pili, suala la kamati nadhani ni la muhimu sana, lakini tulipanue zaidi kwa maana ya kuwa mtawanyiko wetu ni vyema ukawa unaratibiwa na kamati maalum za kimaeneo. Napendekeza kuwe na kamati kila bara (kwakuwa tumesambaa kila kona ya dunia), na ziwe na mratibu wao mkuu ambaye atasimamia shughuli na maendeleo ya eneo fulani. Mfano Amerika kuwe na mratibu, Asia, kuwe na mratibu nk.

Tatu; Kuna kazi nimekuwa nikiifanya chini chini baada ya kushauriwa na mmoja kati ya wadau wetu. Alinishauri kama ikiwezekana tuwe na gazeti la walau kila wiki litakalokuwa likipitia na kuripoti yaliyojiri katika Blogi za Watanzania, nikaliona ni wazo zuri sana na ninalifanyia kazi. Nimeshaliandikia muswada wa kuomba fedha kwa wafadhili na washirika mbalimbali nasubiri majibu yake kwa sasa ila kwa mwenye wazo zuri zaidi ya hapo anaweza kuwasiliana nami moja kwa moja ama kwa simu au kuniandikia.

Luihamu utasimamia uchapaji hapo Dar? tehe tehe tehe
Kipengele cha tatu katika safu ya Msangi mdogo kimenivutia sana.Sio kazi rahisi lakini lazima tujitume.Napata picha kuona gazeti la wanablogu Tanzania mitaani huku raia wakigagania kama vile mpira wa kona.Napendekaza wazo la Msangi mdogo.
  Tarehe: 30 January 2007 at 10:11 Anonymous Anonymous Anasema:
Sidhani kama kuna ulazima wa kusema viongozi lazima wawe wanaishi mji fulani. Hii itakwenda kinyume na teknolojia yenyewe ambayo inatufanya tuvunjevunje kabisa masuala ya mipaka na nchi. Nadhani kipimo kikuu ni kuwa huyo mtu awe ana makazi kwenye nchi iitwayo "Mtandaoni." Basi.

Naunga mkono suala la kuwa na waratibu, ambalo Jeff naye ameliongelea, katika maeneo mbalimbali. Tunaweza kuanza na mabara ambayo tayari tupo, wakitokea wanaoishi Antaktika, basi tutaunda kamati ya huko.