Mada ya juma hili: Kikusanya habari (Aggregator) na Tovuti ya Jumuiya.

Monday 19 February 2007
Naam, mambo yaenda yakipamba moto. Baada ya kumaliza juu ya katiba, sasa tunaingia katika ukumbi mwingine muhimu wa ukusanyaji habari na nyumba ya habari. Kama wote tunavyojua suala zima la blogu ni upashanaji na uchambuzi wa habari. Je habari hizi tunazipata wapi? Jibu dhahiri ni hutafutwa na kuwekwa mahala ili wasomaji wasome yanayojili kila siku.

Katika mkutano wa kwanza tulioufanya 2006, yalitoka mawazo kwamba ni vyema tuwe na tovuti ya Jumuiya na pia kikusanya habari (aggregator) hiki kitasaidia kukusanya habari za wanablogu kwa wakati mmoja na hivyo kupunguza safari za kutembelea wanablogu kujua kama wanajipya au la. Kikusanya habari huonyesha nani kaandika habari hivi karibuni na mambo mengine mengi.

Sasa wakati umewadia wa kukubali au kukataa mawazo yaliyopendekezwa juu ya kuwa na au kutokuwa vitu hivi viwili, tujadili huku tukizingatia majina ambayo tutayapa Kikusanya habari na Tovuti. Kama unaunga mkono unaruhusiwa kutoa na jina unalodhani litafaa.

karibuni wote.

**Kuna hiki kikusanya habari cha wanablogu wa Kenya unaweza kuangalia ili kuona inavyofanya kazi.
 
© Blogu Tanzania | Tarehe: 2/19/2007 |

Maoni: 26

Naunga mkono jumuiya iwe na kikusanya sauti.

Majina napendekeza

1.TANZANIA ACTIVIST

2.HAKI TANZANIA

3.NDUGU MTANZANIA

jah bless.
Nakubaliana na kuwa na Kikusanya Habari na Tovuti

Kikusanya habari nakipa jina la NGWANGA, na tovuti PATA HABARI.

Nawasilisha hoja.
Nakubali kuwa na kikusanya habari na Tovuti pia.
- kikusanya habari kiitwe KACHUMBARI
- Tovuti iitwe MAWAZO MBADALA
Mimi naona hiki kisusanya habari tukiita majina mengine hakitaleta maana sana.naona ni bora tukakiita
-KIKUSANYA HABARI.Au hata ya Da Mija PATA HABARI

Kwa sababu hata mtu mwingie akiingia isimuwie vigumu kujua na ana kwenda moja kwa moja katoka kikusanya habari.

Hayo ni mawazi yangu.
This comment has been removed by the author.
Nakubaliana na:
#Kikusanya habari
au...
#Bloguni Wasemaje
#Kipya Bloguni
Tovuti...
Watanzania Bloguni
  Tarehe: 21 February 2007 at 15:21 Anonymous Anonymous Anasema:
Nakubaliana na hoja kuwa kikusanya habari kiwe na jina linalojieleza lenyewe. Neno "kikusanya habari" nakubaliana nalo ila neno hili linakuwa halielezi habari hizo zinatoka wapi. Labda sio lazima. Kama nisingesoma mapendekezo ya Simon ningetoa pendekezo moja tu ambalo ni "kikusanya habari."

Mchango wa Simon yamenichanganya maana karibu yote naona yanafaa na yanajieleza yenyewe. Ninalalia zaidi kwenye "Kipya Bloguni" na "Sauti za Watanzania Bloguni" (na labda kama hili ni refu tunaweza kufanya "sauti za wanablogu.")

Tovuti naona iwe na jina la jumuiya. Tungekuwa tumeshakubaliana juu ya kifupi cha jina la jumuiya ningesema neno hilo ndio litumike pale kwenye www (www.jumuwata.com, www.juwata.com, n.k.).
naunga mkono kuwepo kwa kikusanya habari.jina:jina la simon ni zuri,si vibaya kama tungelibadilisha kidogo kuwa "mpya bloguni" kwa vile tunakusanya habari mpya.
Na mimi naona MPYA BLOGUNI imekaa vizuri, au YALIYOJILI BLOGUNI. Bado nafikiri zaidi juu ya Tovuti.
Nakubaliana na jina YALIYOJIRI BLOGUNI au BLOGUNI WANASEMAJE zaidi kuliko Mpya Bloguni kwasababu kikusanya habari hakitakuwa kinakusanya habari mpya tu bali habari zote zilizoandikwa na walioandikishwa humo ndani isipokuwa kwa kuzipanga zikianzia na mpya
WATANZANIA BLOGUNI naona iko mwake.
Yaliyojili bloguni kutoka wapi?TANZANIA?KENYA?UGANDA?CHILE?MAREKANI?WAPI.

Mimi siwaelewi kabisa wale wanaopendekeza YALIOJILI BLOGUNI.Blogu ni nyingi kutoka nchi tofautifofauti kwa hiyo nilazima tujivunie nchi yetu kwa kutanguliza jina TANZANIA mwanzo wa jina.

BLOGUNI WANASEMAJE,bado sijarithika kabisa wanasemaje kina nani na kutoka wapi?

NAUNGA MKONO WATANZANIA BLOGUNI AU MTANZANIA.
WATANZANIA KWENYE BLOG.Hiyo je?
TANZASANYA-B:TANZAnia + KikuSANYA habari + Blog.
Luihamu, naomba unisaidie kidogo katika Magazeti ya Tanzania, je majina yake yanajieleza kama yanatoka Tanzania?

Mfano: Mwananchi. Mwananchi gani? au wa wapi? Arusha? Kyela au?

Mzalendo. Wa wapi, Tanzania Kenya au Zaire.

Uhuru, wa wapi? Wa Afrika, wa watoto majumbani au wa kina nani?

Kwa hiyo nadhani si lazima sana kila kitu tuwatafunie wasomaji. Si vibaya tukiwaweka katika hali ya kujiuliza. Itawafanya hata watake kujua zaidi na huo ndio unakuwa mwanzo wa kusoma kilichojili.
Duh!
Da mija hapa tunanzungumzia gazeti tando.Gazeti tando.kwa mfano watu wanataka kupata habari kutoka tanzania atatafuta wapi?lakini kama tukitumia jana TANZANIA inakuwa rahisi kwa yeyote yule kuelewa na kufahamu ya kwamba hawa ni wanablogu kutoka Tanzania.kwa mfano wewe unataka kupata habari kutoka tanzania au wanablogu wa tanzania wana yapi mapya utafunguwa kenyan unlimited?

Ndugu wanablogu nawaomba tutumie jina lenye jina la nchi yetu.Damija unapozungumzia magazeti kama UHURU,MWANANCHI na kadhalika,kuna sehemu wameandika Tanzania katika kurasa ya mwanzo wa gazeti.

Napinga wazo au hoja ya Da Mija Shija.
Da mija hapa tunanzungumzia gazeti tando.Gazeti tando.kwa mfano watu wanataka kupata habari kutoka tanzania atatafuta wapi?lakini kama tukitumia jana TANZANIA inakuwa rahisi kwa yeyote yule kuelewa na kufahamu ya kwamba hawa ni wanablogu kutoka Tanzania.kwa mfano wewe unataka kupata habari kutoka tanzania au wanablogu wa tanzania wana yapi mapya utafunguwa kenyan unlimited?

Ndugu wanablogu nawaomba tutumie jina lenye jina la nchi yetu.Damija unapozungumzia magazeti kama UHURU,MWANANCHI na kadhalika,kuna sehemu wameandika Tanzania katika kurasa ya mwanzo wa gazeti.

Napinga wazo au hoja ya Da Mija Shija.
  Tarehe: 25 February 2007 at 20:58 Anonymous Anonymous Anasema:
Sauti za Wanablogu
  Tarehe: 25 February 2007 at 20:59 Anonymous Anonymous Anasema:
Wasemayo Wanablogu
  Tarehe: 25 February 2007 at 20:59 Anonymous Anonymous Anasema:
Kunani Bloguni
napendekeza JuwataBlog
Nakubaliana na 'Sauti za wanablogu' kwa tovuti, na 'Kunani bloguni' kwa kikusanya habari.
  Tarehe: 27 February 2007 at 17:48 Anonymous Anonymous Anasema:
Tovuti bado naona ni sawa ikabeba jina la jumuiya yetu. Kikusanya habari: Kunani Bloguni.
Kunani bloguni:kikusanya habari
Tovuti:jina la jumuiya
Naunga mkono tovuti kuchukua jina la jumuiya, lakini je hili ndilo litakalo simama katika anuani pia?, nina maana pamoja na urefu wake? au anuani itaandikwa katika kifupi chake? kama itaandikwa kwa kifupi basi tukumbuke bado hatujapata kifupisho kimoja kilichokubalika.

Tuendelee tutafika.