Mada ya juma hili: TUZO

Monday 26 February 2007
Kwa mara nyingine tena tunachukua nafasi hii kuwashukuru wale wote wanaofanikisha mjadala huu. Mambo yanazidi kusonga mbele, na tuna furaha kuwasilisha tena mada mpya tutakayohangaika nayo katika wiki hii nzima. Wiki hii tutajadili juu ya TUZO. Mjadala utalenga kuwa au kutokuwa na TUZO kwa wanablogu wa Tanzania. Sambamba na hili tutajadili pia MFUMO WA UTOLEWAJI wake kama tutakubaliana ziwepo. Tunahitaji kujadili kujua zitatolewaje? Kwa kupigiwa kura au? Tuzo hizi/hii itakuwa ni nini? na pia Sifa za kupata TUZO. Hatuna mengi ila tusisahau kupiga kura juu ya jina la Tovuti na Kikusanya habari cha Jumuiya hapo chini.
 
© Blogu Tanzania | Tarehe: 2/26/2007 |

Maoni: 11

kwa maoni yangu nadhani ni mapema mno kuzungumzia kuku wakati bado yai halijapasuka. mie nadhani tukubaliane kuundwa kwa jumuiya, kisha katiba, na hatimaye uongozi ambao huu utaamua (kwa ridhaa ya mkutano mkuu wa wanajumuiya) shughuli za kufanya. sina nia ya kupinga lakini muono wangu ni kwamba tuanze kuogelea baada ya kuufikia mto.
kaka michuzi ni sawa nimekukata ila si wajua kila kitu kina mipango na malengo na nia kila kitu kitaenda sawa...hivyo vibaya tukianza kuongeaa hayo masuala ya tuzo maana zitakuwa ni moj ya changamoto kwa wanablog.
  Tarehe: 28 February 2007 at 21:58 Anonymous Anonymous Anasema:
Nadhani tunachofanya sasa ni kutaka kujua aina za tuzo zenyewe na mfumo wa kuzitoa. Mengine yatakayofuata naona viongozi wanaweza kuyashughulikia. Ila hili la aina za tuzo na namna ya kuchagua blogu za kutunzwa sioni ubaya tukajadili hivi sasa.
shamim na ndesanjo!

tuko pamoja. nilichotaka kukazia si kukataa mjadala wa tuzo bali kusisitiza kumaliza ngwe ya katiba, kisha uongozi maana tukiendelea na tuzo inagusa sehemu za 'activities' za wanajumuiya ambapo bila katiba na uongozi japo wa muda, tutakuwa tunaruka kitu. hivyo naomba niombe tena umuhimu wa kuhitimisha katiba na kisha uongozi kabla ya kuanza kuogelea nchi kavu
Michuzi, naomba mimi nijibu hoja kama mwanakamati wa muda. Unachosema ni kweli kabisa, ila tunachofanya sasa hivi ni kujadili vipengele vikuu vilivyopendekezwa katika mkutano wa Nov 18,2006. Tunataka viwe wazi kwa wanablogu wote ili jumuiya itakapoanza kazi rasmi kila mmoja awe anajua kipi na kipi kitaendeshwa jumuiyani.

Jaribu kufungua kwenye kumbukumbu za Januari, halafu uende chini kabisa kwenye posti ya kwanza ya ufunguzi utaona hivi vipengele vikuu vitakavyojadiliwa sasa hivi kabla ya jumuiya kuanza rasmi.

Asante kwa mchango wako.
Naunga mkono kuwa na Tuzo kwa wanablogu, hizi naona ziwe zinatolewa siku ya Blogu Tanzania kama itakubalika kuwepo, na upatikanaji wake uwe ni kwa njia ya kupendekezwa na baadaye kupigiwa kura.

Nawasilisha hoja.
namuunga mkono Da'mija hapo juu.
  Tarehe: 4 March 2007 at 11:56 Blogger luihamu Anasema:
Namuunga mkono Da Mija hapo juu.
namuunga mkono Da'Mija kuhusu tuzo, siku ya kutolewa na mchakato wa kupata washindi
  Tarehe: 4 March 2007 at 21:14 Anonymous Anonymous Anasema:
Naunga mkono tuzo zitolewe siku ya Blogu Tanzania (ambayo ni tarehe ngapi?...umeshasahau?).

Ila uongozi ndio utakuwa unaamua kila mwaka wanaochaguliwa wapewe kitu gani. Pia kuhusu tuzo zitolewe kwenye makundi yapi (mfano: blogu bora ya mwaka, blogu bora ya picha, podikasti bora, n.k.) naona iwe ni kazi ya uongozi maana inawezekana kila mwaka kukawa na tuzo mpya na nyingine zikabadilika, nyingine kuondolewa, n.k.

Naona kuwe na blogu ambazo zitapewa tuzo kutokana na kura za wasomaji na blogu nyingine zitapewa tuzo kwa kuteuliwa na uongozi (au kamati ya tuzo???!!)

Mnasemaje?
Ni kweli Ndesanjo.