Matokeo ya mada iliyopita, Tovuti na Kikusanya habari.

Sunday, 25 February 2007
Juma lililopita tulikuwa katika mjadala mzito juu ya kuwa na TOVUTI na KIKUSANYA HABARI katika jumuiya yetu. Mjadala ulienda vizuri na hadi kufikia leo ambapo ndiyo mwisho wa mjadala wa mada hii wanablogu wamekubali Jumuiya iwe na Tovuti na pamoja na Kikusanya habari.

Katika mjadala huo, tulitakiwa pia tupendekeze majina ya Tovuti na Kikusanya habari kama tutakubaliana viwepo. Tumependekeza majina mbalimbali, lakini hadi sasa hivi bado halijapatikana jibu moja lililokubaliwa. Bado kuna utata katika mapendekezo ya wachangiaji ambao mawazo yao yameonekana kuungwa mkono na wengi, kwa mfano Kitururu amependekeza majina mengi, lakini yaliyoonekana kupendwa zaidi ni KIPYA BLOGUNI, wengine wakamrekebisha na kutaka iwe MPYA BLOGUNI, sasa hapo inabidi tukubaliane jina tunalolitaka. Huu ni mfano tu. Kwa hiyo kutokana na hali hii kamati inaongeza muda wa juma lingine katika mada hii. Majina yote yaliyopendekezwa yatapigiwa kura upya na kwa vile huu ni muda wa ziada, tunaomba tusiongeze majina mapya kwa kuwa muda wake umekwisha, tuunge mkono au kukataa haya tuliyonayo.

** Pia kuna habari njema tumezipata hivi punde kwamba kuna mdau mmoja ameshajitolea kugharamia gharama za TOVUTI na KIKUSANYA HABARI, wote tunafahamu vitu hivi si bure, kuna malipo katika kupata domain name na mambo kama hayo. Mungu atupe nini jamani!!
 
© Blogu Tanzania | Tarehe: 2/25/2007 |

Maoni: 6

napendekeza tujiite bongobloggers.com
jina limetulia hilo la bongo bloggers.com

au mkusanyowahabari.com
jina limetulia hilo la bongo bloggers.com

au mkusanyowahabari.com
jina limetulia hilo la bongo bloggers.com

au mkusanyowahabari.com
jina limetulia hilo la bongo bloggers.com

au mkusanyowahabari.com
Shamim na Michuzi, mnaweza pia kusoma maoni ya majina yaliyopendekezwa hapo chini katika mada iliyopita ya tarehe 18 feb.

Karibuni.