Yaliyokubalika kuhusu KATIBA na nani ni MWANAJUMUIYA.

Sunday 18 February 2007
Haya tena ndugu wanablogu, kama ilivyo kawaida ya kila Jumapili kutoa jibu la yale yaliyokuwa yakijadiliwa katika juma zima, leo tena muda umewadia. Juma lililopita tulijadili kama Jumuiya iwe na katiba yake au la, na pia tuliendeleza mjadala juu ya nani awe Mwanajumuiya. Yafuatayo ndiyo yaliyokubalika:-

KUHUSU KATIBA.
Imekubalika kwamba jumuiya itakuwa na katiba yake. Hii itafanya Jumuiya kuwa na mwongozo maalumu na pia itasaidia katika utekelezaji wa mambo mbalimbali.

KUHUSU NANI MWANAJUMUIYA.
Kutokana na maoni ya wengi imekubalika kwamba mwanajumuiya si lazima awe anamiliki blogu. Mtu yeyote anaruhusiwa kujiunga na Jumuiya hii isipokuwa ni lazima aombe uanachama na akubaliane na masharti ya kujiunga na Jumuiya.

Kwa mara nyingine tena tunatoa shukrani kwa wote waliojitokeza kufanikisha mjadala huu. Kaa tayari kwa mada itakayofuatia.
 
© Blogu Tanzania | Tarehe: 2/18/2007 |

Maoni: 0