Yaliyokubaliwa kuhusu Mwanajumuiya na Nembo.

Sunday 11 February 2007
Kwanza tunawashukuru wachangiaji wote wa mada iliyopita, mada ambayo hadi kufikia siku ya leo ya kutoa matokeo bado ina kipengele kilichosimama njiapanda.

Juma lililopita tulijadili kuhusu Mwanajumuiya na taratibu zitakazomzunguka na pia tulijadili juu ya Nembo ya jumuiya kama mada ya ziada.(mada hii iko huru kuendelea).

Na kama tulivyokubaliana kwamba kila Jumapili litakuwa likitolewa jibu, basi yafuatayo ndiyo majibu yaliyokubalika.

1. Kuhusu nani awe ni mwanajumuiya.

Katika hali ambayo haikutegemewa kipengele hiki kimepata kura sawa kwa sawa na
kufanya kukosa jibu kamili hadi sasa hivi.

Kuna wachangiaji ambao wamependekeza kwamba mwanajumuiya ni lazima awe na blogu
yake mwenyewe hawa ni Michuzi, Kaka Pori, Ras Luihamu na Ndabuli.

Vilevile kuna wachangiaji ambao wamependekeza kwamba mwanajumuiya si lazima awe
na blogu yake mwenyewe na hawa ni Kitururu, MsangiMdogo, Ndesanjo na Da'Mija.

Kwa maana hiyo basi, kipengele hicho itabidi kipigiwe kura ili kupata kundi lenye
watu wengi zaidi.

2. Kuhusu taratibu za mtu kujiunga na kusimamishwa katika jumuiya.

Katika kipengele hiki wachangiaji wote wamekubali kuwepo na taratibu hizi ili
kulinda nidhamu ya jumuiya na utendaji kazi wake.

Kwa maana hiyo kutakuwa na mipaka ya nidhamu ya Jumuiya itakayoundwa na wanajumuiya wenyewe pale jumuiya itakapoanza Rasmi.

Ndugu wasomaji na wachangiaji, tunashukuru kwa mchango wenu na tunapenda kutangaza kwamba mada hii imefungwa isipokuwa kipengele cha nani anapaswa kuwa mwanajumuiya. Kipengele hiki kitaendelea hadi kura nyingi zinazopendekeza upande mmoja zipatikane.

Karibuni kwa mada ya Nani awe mwanajumuiya.
 
© Blogu Tanzania | Tarehe: 2/11/2007 |

Maoni: 9

Kura yangu ni kwamba si lazima mwanajumuya awe na blogu,Aamen!
Mwanajumuiya si lazima amiliki blogu.

Baada ya kutafakari kwa makini zaidi nimeamuwa kutoa uamuzi wangu na ninamuunga mkono Da Mija,ndesanjo,simon,msangi mdogo.

Sijapokea chochote.Jah live.
Mimi Kura yangu inabaki palepale mwanajumuiya awe na blogu.KWA NINI? Mfano ni swala la kujiunga na kusimamishwa katika jumuiya/nidhamu. Huyu mwanajumuiya asiyekuwa na blogu swala hilo litamgusa vipi?unamsimamisha vipi? Maana yeye ni mtu wa kutoa maoni sehemu yoyote hana sebule yake maalumu sasa mfano akiwa ni mkorofi na jumuiya haimtaki unamuondoa vipi kwenye jumuiya ? unadhibiti vipi nidhamu yake?
Wanaopiga kura ya si lazima hebu tupeni hoja za kura yenu.
Mimi naamini mtu yeyote anaweza kuwa mwanachama. Sidhani kama mwanablogu mwenye blogu anatishiwa na yule asiye na blogu. Kwa sababu mwanablogu ndiye atengenezaye hoja ambazo wasio na blogu huchangia fikira.Halafu mwanablogu anauwezo wa kuondoa maoni asiyoyataka katika blogu yake ikiwa hafurahishwi na mchango wa mchangiaji. Ila naamini kuwa wasiokuwa na blogu wanaweza kuwa mchango mkubwa kwa wenye blogu. Naamini kuwa mwanachama kama unablogu utafaidika zaidi kuliko ukiwa huna blogu.lakini sioni sababu ya kumnyima asiye na blogu kujiunga kama mwanachama. Kwanza yeye mwenyewe atakuwa anakosa uroda wa kuanzisha hoja kwa uhuru. Ni kweli kumfukuza aliye na blogu ni rahisi.Lakini hata akifukuzwa unafikiri atashindwa kuchangia kama anonimosi?Nafikiri bado tunaangalia ni nini mwanachama atafaidika nacho katika jumuiya. Lakini sioni kwanini mchangiaji asiye na blogu ajulikanaye kama mwanajumuiya atengwe
Naunga mkono aliyosema Kitururu, Ndabuli hoja unaziona?
Sijaona hoja, naona hoja yangu simoni hajaielewa ni kwamba sijasema kuwa mwenye blogu anatishwa na asiye na wala sijaandika kuwa atengwe,la, asiye na blogu kama alivyoandika simoni hakataziwi kuchangia sehemu yoyote ya wanajumuiya, swala ni utendaji,mfano:(ninayo mingi naweza kuandika makala ila sehemu hii sio yake) kwa sana sema sehemu wewe Da mija wakati unawahamasiha watu wachangie mjadala si wengi wao umewafuata kwenye blogu zao au,fikiria mwenywe shughuli za kiutendaji. Simoni amekubali kumsitisha uanachama asiye na blogu ni rahisi kuliko asiye kuwa nayo akichangia kama anonimasi ni anonimasi hana uhusiano na jumuiya ,hivyo jumuiya haina mamlaka juu ya vitendo vyake.
Kwenye swala la kumtenga nimeona kwenye mjadala wa Katiba ndio mmeanza kuwatenga wasio kuwa na blogu mnapoanza kutenganisha "majukumu ya aliye na blogu na asiye nayo" maelezo yangu kwa hili tazama kwenye mjadala wa Katiba.
NB: Maswali yangu lakini hayajajibiwa?
Naomba nirekebishe sehemu chache za hapo juu...:mifano(ninayo mingi naweza kuandika makala ila sehemu hii sio mahalipake) Da mija wakati unawahamasiha watu wachangie mjadala si wengi wao umewafuata kwenye blogu zao au,fikiria mwenywe shughuli za kiutendaji.
Simoni amekubali kumsitisha uanachama aliye na blogu ni rahisi kuliko asiye kuwa nayo, akichangia kama anonimasi ni anonimasi hana uhusiano na jumuiya, hivyo jumuiya haina wajibu wowote juu ya vitendo vyake.
  Tarehe: 14 February 2007 at 15:28 Anonymous Anonymous Anasema:
Ndabuli: hata mwenye blogu anaweza kutoa maoni ambayo yanakwenda kinyume na maadili ya jumuiya kwa kutumia jina la uongo au anonimasi.
Jamani naomba mnishawishi basi kwa kunijibu maswali niliyouuliza .