Mjadala umefungwa.

Monday, 12 March 2007
Leo hii imetimia miezi miwili kasoro siku mbili tangu tuanze mjadala katika blogu hii. Tulianza tarehe 13 ya mwezi wa 1, na kumaliza leo tarehe 11 ya mwezi wa 3. Ni furaha iliyoje kupiga hatua hii!

Tulipoanza tulikuwa na lengo ya kujadili vipengele vikuu sita ambavyo vitasaidia kuunda Jumuiya muafaka ya wanablogu wa Tanzania. Vipengele hivi ni pamoja na:-
1. Uundaji wa jumuiya ya wanablogu Tanzania.

2. Jina la jumuiya na aina ya muundo wake.

3. Kikusanya habari na jina lake.

4. Ujenzi wa tovuti ya jumuiya.

5. Tuzo na mfumo wa utolewaji wake.

6. Siku ya blogu Tanzania.

Leo hii kutokana na ushirikiano wenu tunashukuru tumeweza kupata msingi wa jumuiya yetu ambao ndio utasaidia kusimamisha nguzo tuzitakazo. Tukumbuke jumuiya bado haijajengwa, hii ni hatua ya kwanza iliyotupatia msingi, tutaingia hatua ya pili ambayo itatukamilishia ujenzi mzima wa jumuiya yetu.

Kwa kweli hatuna la ziada tunawashukuru kwa mawazo yenu na sasa tunatamka rasmi kwamba hatua ya kwanza ya mjadala imefungwa.
Asanteni.
 
© Blogu Tanzania | Tarehe: 3/12/2007 |

Maoni: 5

  Tarehe: 14 March 2007 at 22:05 Blogger Unknown Anasema:
tunaishukuru kamati ya maandalizi kwa kazi nzuri ya kuendesha mjadala wa mambo nyeti ya jumuiya.tunawatakia afya njema wakati tujiandaa na hatua inayofuata.
Namuunga mkono na Mguu Mzee Zemarcopolo hapo juu. Lakini viongozi tupeni basi dondoo za hatua ifuatayo.
@Watu fulani....
Nilisikia kuna watu wanapinga michango ya wasio na blogu ambao ni muhimu katika jumuiya. Mfuatilie Mzee Zemarcopolo ambaye hana blogu yake halafu utaelewa ....
  Tarehe: 18 March 2007 at 09:13 Blogger luihamu Anasema:
Kamati ya maandalizi kinachofwata ni nini? Tumepoteza siku saba bila kujuwa kinachoendela,we have to be faster kabla ya SABASABA.

Mzee Simon unalionaje wazo la SABASABA?Wakati wakujitangaza ndio huu,pindi tu sabasaba inaanzaa nasi tuwe tumejiandaa JUMUIYA YA WANABLOGU TANZANIA.(Da Mija upo hapo)
jah rastafarian.
  Tarehe: 22 March 2007 at 17:18 Blogger luihamu Anasema:
Hivi kinachofwata ni nini?
  Tarehe: 25 March 2007 at 04:18 Anonymous Anonymous Anasema:
Toka Kwa wanakamati:
Kitakachofuata kikubwa ni uchaguzi wa viongozi. Hii ni hatua muhimu sana hivyo lazima kuhakikisha kuwa tunaifanikisha. Tunatafiti njia bora zaidi ya kufanikisha zoezi hili la uchaguzi ili uwe wa haki.

*Wanakamati*