Shindano la kubuni nembo ya Jumuiya ya wanablogu Tanzania.

Sunday 25 March 2007
Wanablogu na wasomaji wote, kama ilivyokubalika hapo awali juu ya kuwa na nembo, Sasa tunakaribisha rasmi nembo hizo. Shindano litaendeshwa hadi tarehe 30-04-2007, na zawadi itakuwa ni kuchaguliwa na kutumika kwa nembo yako. Tulikubaliana pia kuwa nembo zitakapotumwa hatatajwa mbunifu bali picha yake itapewa namba kitu ambacho kitasaidia kuepuka kuchaguliwa kwa picha kutokana na umaarufu wa mchoraji. Wote mnakaribishwa wachoraji na wasio wachoraji.

Kwa kutuma Nembo hizo tumia anuani hii: mijasayi@yahoo.com
 
© Blogu Tanzania | Tarehe: 3/25/2007 |

Maoni: 4

ZAwadi ni ipi wakubwa ili tuilie tizi
Chediel,
Zawadi itakuwa ni kuchaguliwa na kutumika kwa nembo yako.
  Tarehe: 30 March 2007 at 19:03 Blogger luihamu Anasema:
KWA WAWAKILISHI AU UONGOZI WA MUDA WA JUMUIYA YA TANZANIA

NDUGU NDESANJO MACHA
NDUGU RAMADHANI MSANGI
NDUGU DA MIJA SHIJA
NDUGU JEFF MSANGI.

Nawaomba kabla ya SABASABA TUWE TUMESHAPATA NEMBO NA UONGOZI MZIMA WA JUMUIYA YA WANABLOGU TANZANIA.

SIELEWI KWA NINI TUNACHELEWESHA MAMBO,BAADA YA KUJADILI ZAIDI YA MIEZI MITATU BADO WAWAKILISHI WALIKAA KIMYA ZAIDI YA WIKI MBILI BILA KUTUAMBIA KINACHOFWATA,WALICHOTUELEZA NI MAJADALA UMEFUGWA.

SWALA LA UONGOZI NAONA LINAVUTWA SANA NA SIJUI KWA NINI.NASHAURI WIKI INAYO KUJA TUANZE KUCHAGUWA VIONGOZI PASIPO SABABU ZOZOTE.

KAMA UPATIKANAJI WA NEMBO NI SHIDA TUNAWEZA KUTUMIA BENDERA YA TANZANIA KAMA NEMBO YETU NA RAMANI YA TANZANIA.

PIA NAOMBA WAWAKILISHI WAWE WANATUPA MAENDELEO KILA SIKU PASIPO KUKOSA.

NILIWAHI KUJADILI NA MWANABLOGU MAHIRI KABISA HAPA NYUMBANI NDUGU MAGGID MJEGWA NA AKANIHAKIKISHIA ANAWEZA KUAANDA ILI BAADHI YA WANABLOGU KUHOJIWA NA BAADHI YA VITUO VYA LUNINGA,LAKINI INAKUWA VIGUMU KWASABABU JUMUIYA HAIJA KAMILIKA, NA SIJUI KWA NINI HAIJAKAMILIKA MPAKA WA LEO.

HUU MWENDO TUNAO KWENDA NAO UNAWEZA HATA KUCHUKUWA MWAKA MZIMA.

JAH RASATAFARIAN.
  Tarehe: 7 April 2007 at 19:18 Anonymous Anonymous Anasema:
Ushauri tu, Mtu hawezi kukaa siku nzima kutengeneza nembo mwisho usimpe Credit anayo itaji kupewa. Hivyo mwanzo mpeni namba lakini mkianza kutumia ni lazima mumpe Credit zake kwamba ni nani aliye tengeneza.