Siku ya Blogu Tanzania

Monday, 5 March 2007
Wapenzi wasomaji na wachangiaji wote. Juma hili
tutajadili mada ya mwisho kabisa ya vipengele vikuu
tulivyokuwa tukivijadili tangu kuanza kwa mjadala huu.


Mada hii ni fupi inayohusu kuwepo au kutokuwepo kwa
siku ya blogu Tanzania. Katika mkutano wa kwanza,
ilionekana kwamba upo umuhimu wa kuwa na siku hii,
lakini ilionekana kwamba ni vyema suala hili likawekwa
bayana kwa kupewa muda wa kutosha kujadiliwa, na ndiyo
sababu leo hii tumeiweka mada hii hewani ili wote
tujadili.

Je ni vipi tutakuwa tukiienzi siku hii?

Mawazo yenu yanahitajika. Asanteni.

Labels:

 
© Blogu Tanzania | Tarehe: 3/05/2007 |

Maoni: 8

  Tarehe: 6 March 2007 at 01:11 Blogger Unknown Anasema:
siku ya blog ni muhimu.hata hivyo mimi nadhani tunaweza kuwa na wiki ya blog ambayo tutaitumia kuandika makala mbalimbali kwenye blog na kwa magazeti ya tanzania kwa dhumuni la kuufungua umma wa tanzania macho juu ya kublog.siku ya mwisho ya wiki hiyo tunaweza kuitumia kwa bloggers chat ambapo tukabadilishana mawazo mbalimbali online kwa muda fulani ikiwa ni pamoja na kufahamiana.
Naunga mkono hoja ya Zemarcopolo na napendekea siku ya Blogu ya Wanajumuiya iwe ile siku wazo la kuanzisha mchakato mzima huu lilipoaliwa, kisha juma linalofuata liwe hivyo - juma la wanablogu wa tanzania.
Zemarcopolo umesema. Na kuunga mkono.
  Tarehe: 7 March 2007 at 09:05 Anonymous Anonymous Anasema:
Naunga mkono pia.
Namuunga mkono Mzee Zemarcopolo. Namuunga mkono pia Michuzi kuwa siku ya wanablogu iwe ni ile ya tarehe wazo lilipozaliwa rasmi.Tarehe mkutano wa kwanza ulipofanyika.
  Tarehe: 7 March 2007 at 18:27 Blogger luihamu Anasema:
Namuunga mkono Mzee Mercopolo.jah live.
Kufahamiana ni jambo jema sana pamoja na kuwa wengine mpo ughaibuni lakini kujua kuwa fulani yupo nchi gani nk,pia mengine yanaweza kufuatia kama Ras Luiham huko mwanzoni alipowahi uliza kama wanablogu mnaweza kuoana kwa wasiokuwa na ndoa.
  Tarehe: 10 March 2007 at 23:41 Anonymous Anonymous Anasema:
Wazo la Zermacopolo ni zuri sana. Tunaweza kuwa na shughuli mbalimbali wiki nzima kisha hitimisho likawa ndio ile tarehe tuliyokutana kwa mara ya kwanza.
Nakubali kuwa kati ya mambo tutakayohitaji kufanya ni kuandika makala, wanablogu kutokea kwenye luninga kufanya mahojiano na pia kwenye vyombo vingine vya habari, kuwa na warsha, n.k. Pia kuwe na ujumbe maalum kila mwaka.