Yaliyokubalika katika mada iliyopita... ''Siku ya blogu Tanzania.

Sunday, 11 March 2007
Kama ilivyo ada yetu ya kutoa hitimisho la kila mada inayojadiliwa, leo tena tunafuraha kuwaletea yaliyokubalika katika mada iliyopita iliyohusu siku ya blogu Tanzania kama ifuatavyo:-

- Wanablogu wamekubali kuwepo kwa siku ya blogu ambayo itakuwa ni kila tarehe 18 ya mwezi
wa 11, tarehe ambayo mkutano wa kwanza wa wanablogu wa Tanzania ulifanyika.

- Pamoja na siku hii, imependekezwa iwepo wiki ya wanablogu wa Tanzania ambapo katika wiki
hii zitafanyika shughuli mbalimbali za kuitangaza blogu kwa umma, shughuli kama uandishi wa
makala mbalimbali, kufanya mahojiano na vyombo vya habari kama redio, luninga na hata
maonyesho ya sanaa. Pamoja na haya yote wiki hii ambayo kilele chake ndiyo kitakuwa 18/11
itakuwa na ujumbe maalumu utakaokuwa ukiongoza shughuli nzima.

Ndugu wanablogu, hayo ndiyo yaliyokubalika lakini tunaamini yako mengi yatakayozaliwa wakati utekelezaji utakapoanza, milango iko wazi kwa mawazo zaidi wakati wowote. Asanteni.
 
© Blogu Tanzania | Tarehe: 3/11/2007 |

Maoni: 0