YALIYOKUBALIKA KUHUSU TUZO + MAJINA YA TOVUTI NA

Monday, 5 March 2007
Wapenzi wanablogu na wasomaji wote, kwa mara nyingine tena tunafurahi kuwaletea matokeo ya mada mbili zilizopita. Kama wote tunavyojua kwamba katika juma lililopita tulikuwa na mada kuu moja hii ilihusu Tuzo kwa wanablogu wa Tanzania na nyingine ambayo ilihitaji kukamilishwa hii ilikuwa ni juu ya majina ya Kikusanya habari na Tovuti.

Kutokana na ushirikiano wenu leo hii tumeweza kupata majibu ambayo tulikuwa tukiyatafuta, na tunapenda kuyawasilisha kama ifuatavyo:-
1. JINA LA TOVUTI NA KIKUSANYA HABARI.
Wanablogu wamependekeza kwamba Tovuti ichukue jina la jumuiya. Kwa hiyo basi
Tovuti hii itakuwa ikiitwa 'JUMUIYA YA WANABLOGU TANZANIA.
Kuhusu kikusanya habari, wanablogu wamependekeza kiitwe 'KUNANI BLOGUNI'.

2. TUZO.
Kuhusu Tuzo, wanablogu wote waliochangia hoja wamekubali kwa nguvu moja kuwa na Tuzo kwa wanablogu. Na imependekezwa kwamba ziwe zikitolewa katika siku ya blogu Tanzania kama siku hii itakubalika kuwepo. Kuhusu aina za Tuzo na mfumo wa utolewaji wake hili litakuwa likishughulikiwa na uongozi husika utakaokuwepo madarakani kwa wakati huo.
Ndugu wachangiaji mada, tunashukuru sana kwa michango yetu na Jiandaeni kwa mada nyingine wakati tukielekea mwisho wa mijadala.

Labels: , ,

 
© Blogu Tanzania | Tarehe: 3/05/2007 |

Maoni: 0