Luihamu ringo - Nafasi ya Mwenyekiti

Sunday 13 May 2007

Katika kuitikia wito wa kuomba nafasi za uongozi wa Jumuiya, mwanablogu Luihamu amejitokeza tayari, yeye anaomba nafasi ya kuwa Mwenyekiti. Yafuatayo chini ni maelezo yake binafsi, malengo yake kwa jumuiya na kwa nini anataka kuwa Mwenyekiti.

WASIFU.
Kazi: Mtaalamu katika masuala ya data entry.
Umri: Miaka 28.
Utaifa: Mtanzania.


Maelezo kwa nini nagombea nafasi ninayoomba.

Kwa mtazamo wangu au dira yangu, napenda jumuiya iwe sauti ya watoto yatima.Watoto wengi wanabaki katika hali mbaya ya maisha. Hakuna wakulaumiwa bali ni sisi wenyewe kuchukuwa hatua ya kuona watoto yatima wanalelewa katika mazingira mazuri.


Nini natarajia kufanya katika kuikuza Jumuiya

1. Kuelimisha jamii kuhusu blogu. Dhana mpya ya uandishi wa habari.
2. Kukuza kamati na kuziwezesha .
3. Dira ya kujenga kituo cha watoto yatima chini ya jumuiya ya wanablogu tanzania mfano
JUMUIYA YA WANABLOGU TANZANIA KITUO CHA WATOTO YATIMA.

http://luihamu-rastafarian.blogspot.com/

Naombeni kura zenu.
 
© Blogu Tanzania | Tarehe: 5/13/2007 |

Maoni: 9

  Tarehe: 30 May 2007 at 07:27 Blogger luihamu Anasema:
Ngoja nijipongeze mwenyewe kwa kuchukuwa nafasi hii.

Baada ya kuona wale wote waliojitokeza kuwania uongozi kuwa na maoni ya kuwapongeza kwa hatua waliyochukuwa na mimi kutokuwa na maoni nimeomua angalau kuacha comment moja.
kumbukeni.

NOT MANY WILL ACCEPT HIM,BUT FEW CHOOSEN BY HIM(Robert Nesta Marley)

Nuff Nuff Respect.
@Hongera Luihamu kwa kuchukua hatua hii ya kugombea Uongozi wa Jumuiya.
  Tarehe: 3 June 2007 at 15:57 Anonymous Anonymous Anasema:
Tuko pamoja kamanda!
  Tarehe: 6 June 2007 at 07:53 Blogger luihamu Anasema:
Anonymous Asante sana.

Mzee Au asante sana.

Nashangaa kuona Da Mija hajanipongeza.

Jah bless.
Mzee wa nguvu! Una kura yangu. Lakini Mzee saa nyingine unanipa dondoo ambazo unaonyesha kutojiamini. Halafu una mchezo wa kubadilisha mawazo ghafla leo hivi, halafu kesho unabadilisha tena, Naamini unaelewa naongea nini kwasababu haya mambo unayafanya pabuliki. Nikiondoa hilo Mzee Rasta simjui mtu mwingine mwenye nguvu hata ya kufuatilia maswala ya jumuiya kuliko wewe. Kura yangu unayo.
  Tarehe: 10 June 2007 at 09:40 Blogger luihamu Anasema:
Ni kweli nimekuwa nikifanya hivyo.umewahi kusikiliza mahojiano ya Peter Tosh,wengi walishindwa kumwelewa lakini matunda yake waliyaona.

Mimi na jiamini kabisa ila nilikuwa na hofia Mzee mmoja,Mwanablogu maarufu duniani,huyu bwana angechukuwa kura zote yani angepita bila wasiwasi.Nadhani unamfahamu Mkuu Simon.

Jah guidance.
Mzee Kitururu naungana na wewe juu ya suala zima la kubadilikabadilika kwa Mzee Luihamu. Ras hebu naomba kuuliza kisa huwa nini hasa?
  Tarehe: 10 June 2007 at 15:13 Blogger luihamu Anasema:
mimi sibadilikibadiliki,kwanza niliona majina ya wanablogu wanaopendekwenzwa kuongoza jumuiya yatu.

Nikakumbuka ule msemo unaosema

IF YOU CANT BEAT THEM JOIN THEM.

Lakini baada ya masaa kadhaa nikaamuwa kurudi ulingoni.

Ninajiamini kabisa.

Respect.
  Tarehe: 18 June 2007 at 18:20 Blogger Rundugai Anasema:
RAs hatabadilika kamwe ninamwaminia kwa sasa.Tumpe kura afanye kazi tunayotaka wana jumuiya,napenda apite kwani ni MTU ANAEJITUMA SANA KATI YA VIJANA NILIOWAHI KUKUTANA NAO.Hivyo ninaimani kuwa tutapata kiongozi bora.TUMPE KURA