Ramadhani Msangi- Nafasi ya Mwenyekiti.

Saturday, 26 May 2007
WASIFU
1. Umri : miaka 31
2. Utaalamu: Biashara (masoko & matangazo), Habari na Sheria
3. Sijaoa

KWANINI NAGOMBEA:
Kuweza kushirikiana na wenzangu katika kuunda Jumuiya imara itakayowawezesha Watanzania kupata taarifa na maarifa kwa ajili ya maendeleo yao, hasa katika zama hizi ambapo kuna aya za kishetani zinazopigiwa debe kwa jina la sheria za uhuru wa habari.

NINI NITAFANYA:
- Kushirikiana na wenzangu kuunda katiba kwa ajili ya Jumuiya
- Kujenga mazingira ya kuifanya Jumuiya, tegemeo la kila Mtanzania
- Kujenga mazingira ya kuwawezesha na kuwavuta Watanzania zaidi katika ulimwengu wa TEKNOHAMA (Teknilojia ya Habari na Mawasiliano).

http://www.msangimdogo.blogspot.com
 
© Blogu Tanzania | Tarehe: 5/26/2007 |

Maoni: 4

  Tarehe: 30 May 2007 at 01:16 Anonymous Anonymous Anasema:
Hongera Msangi kwa kuingia uwanjani.Kila la kheri
  Tarehe: 30 May 2007 at 07:29 Blogger luihamu Anasema:
Hongere Kamanda kwa kuchukuwa nafasi katika jumuiya ya wanablogu Tanzania.
  Tarehe: 30 May 2007 at 21:58 Anonymous Anonymous Anasema:
Hongera kwa kuonyesha nia ya kuongoza jumuiya yetu.
Hongera Mzee!