EGIDIO NDABAGOYE - NAFASI YA UWEKA HAZINA.

Saturday, 9 June 2007

Wasifu.

Jina: Egidio Ndabagoye
Umri: 25
Utaalamu: Uhasibu na Ushirika
Uhusiano: Sijaoa
Utaifa: Mtanzania

Sababu ya kugombea nafasi hii.

Naamini nafasi hii inatakiwa mtu mwenye taaluma ya uhasibu ili kujua mapato na matumizi na mipango endelevu ya kuendeleza jumuiya yetu na kuifanya iendane na mabadiliko ya kibiashara. Nami naona kwa kushikirikiana na wanablogu wenzangu uwezo huu wa kuiendeleza jumuiya ninao.

Naomba kura zenu

http://www.gaphiz.blogspot.com
 
© Blogu Tanzania | Tarehe: 6/09/2007 |

Maoni: 6

Duh!Sasa hapa katika uhasibu mnanigawa! Maana wewe na Da mija wote mimi naona poa.Sasa si nitaharibu kura kweli hapa:-)
  Tarehe: 10 June 2007 at 09:33 Blogger luihamu Anasema:
Mzee Ndabagoye,karibu sana ndani ya uwanja huu.Hapa kuna kazi tena kazi ya Ziada si mchezo.

Umewahi kuangalia mechi kati ya CHELSEA NA MAN UNITED?Ndio hii.

Mzee kila la heri.

Jah Guidance.
Egidio karibu ukumbini mzee tuchuwane. Sasa huu ndiyo uchaguzi, kila mtu japo kapata mpinzani.
Simon usiharibu kura mkuu sera zinamnadi kila mgombea.Ahsante Ras Luihamu.Mara nyingi wanakwenda suluhu bin suluhu lakini hii mshindi atapatikana
Da mija nishakaribia ngoja tuangalie wapiga kura watasemaje.
  Tarehe: 11 June 2007 at 12:22 Anonymous Anonymous Anasema:
Nakubaliana na Simon. Karibu nafasi zote naona kuna dalili za kuharibu kura. Lakini mchuano unavyokuwa mkali ndio tunaimarika.

Egidio, kumbe ulikuwa umebana tu. Au ulikuwa unawasiliana na kamati ya kampeni...wana mtandao wako?

Heshima zikujie kwa kuwa na moyo wa kututumikia.
bwana egidio naamini kura yangu umeipata damija atanisamehe lakini ni kutokana na kujua histiria yako kiundani kwenye mambo ya fweza nakujua kaka na a.k.a kitasa haikuwa chombweza time katika kupiga kampein waambie wanablog kwanini uliitwa kitasa utapata makura ya kumwaga,damija katoka mbali kweli anastahili kuwa kwenye chat ya uongozi, ndomaana akina kitururu na ndesanjo wanapata shida kufanya maamuzi, lakini embu egidio tushauriane hivi damija hakustahili ukatibu wenezi? yaani muhamasishaji na mambokama hayo naamini angefit sana,lakini tuache wanablog waamue, tchao!!!