Jinsi ya kuanzisha blogu.

Tuesday, 19 June 2007
Wanablogu, kutokana na ukweli kwamba watakaopiga kura ni wale wenye blogu pekee, uongozi wa muda wa umeona ni vema kutoa dondoo za jinsi ya kuanzisha blogu yako mwenyewe ili kila mmoja asikose nafasi ya kupiga kura.

Mzee wetu Ndesanjo ameandaa mwongozo mzuri sana wa kusaidia hili, unaweza kufungua hapa kusoma. Na kama unaona ni maelezo marefu sana na una haraka ya kufungua kwanza na kusoma baadaye, basi fungua hapa na ujaze utakayoulizwa ukikamilisha unakuwa tayari na blogu yako.

Karibuni wote katika ulimwengu wa kublogu.
 
© Blogu Tanzania | Tarehe: 6/19/2007 |

Maoni: 6

  Tarehe: 20 June 2007 at 07:45 Blogger luihamu Anasema:
Naomba kuuliza kamati ya maandalizi,JE WALE WANAOMILIKI BLOGU ZAIDI YA MOJA AU MBILI?WATAPIGA KURA MARA NGAPI NA WAMETUMIA MAJINA TOFAUTI.


NUFF NUFF RESPECT.
Swali zuri Luihamu.
  Tarehe: 20 June 2007 at 14:36 Anonymous Anonymous Anasema:
Wenye blogu zaidi ya moja itabidi wapige kura mara moja kwa kutumia blogu blogu moja. Wengi wenye blogu zaidi ya moja tunawajua, hivyo wakipiga zaidi ya mara moja kura ya pili au ya tatu itakuwa imeharibika.
  Tarehe: 20 June 2007 at 16:22 Blogger Mkina Anasema:
Kazi nzuri ya kuongeza wapiga kura kwa kuwaeleza namna ya kufungua blogu. Lakini naomba wote wataaoanzisha wawe na mtazamo endelevu, kwa maana zisiwe blogu za uchaguzi tu na baada ya hapo zinakufa. Je wenye blogu na kuamua kutumia majina badnia watatambulika, ili wasipige kura nyingi kwa nia ya kumpa ushindi mtu mmoja? Tuelimishwe
Damija nimefungua blogu, sasaaa pale bloguni kwangu,inasema anonymous are not allowed, ni kwa nini, naomba nisaidiwe kwa hili.
Kuuliza kamwe haiwezi kuwa ujinga
Pius kwanza hongera kwa kukata shauri, karibu saana ulingoni. Kuhusu swali lako fuata haya maelekezo.

1. Sign in kama kawaida, utakutana na Dashboard. Hapo kuna sehemu ya New post na kulia kwake Manage POST, SETTING, LAYOUT. Bonyeza SETTING, ukija ukurasa wake angalia palipoandikwa COMMENT bonyeza hapo utakuja ukurasa wa comment halafu angalia palipoandikwa..'who can comment'.. hapo ndo chagua unayetaka atoe maoni.

Nakushauri ufungue na nyingine kwa ajili ya kujaribu jaribu ili kuona inakuwaje unapobonyeza kitu fulani, si unajua tena huwezi kugundua kitu bila kujaribu sasa ukijaribu sana katika blogu iliyo hewani unaweza ukafuta vitu muhimu ukabaki mdomo wazi. Mzee Luihamu alisha delete blogu yake kipindi fulani.

Kwa mara nyingine tena wanablogu tunakukaribisha jukwaani.