Mabadiliko madogo ya siku ya kupiga kura.

Wednesday 20 June 2007
Wanablogu na wadau wote, tumefanya mabadiliko madogo juu ya siku ya kupiga kura. Hapo awali tulitangaza kwamba siku hiyo itakuwa ni tarehe 30/06/2007, siku hii iko pale pale isipokwa tumeongeza siku moja yaani tarehe 29/06/2007, hii ni kutokana na hali halisi ya upatikanaji wa kompyuta, wengi wetu ni lazima waende internet cafe au maofisini na wakati huo huo kuna vikwazo kama vya ukatikaji wa umeme n.k. Kwa hiyo tumeongeza siku moja ambayo ni ijumaa ili kutoa fursa zaidi kwa kila mtu kupiga kura kwa nafasi bila kukimbizana.

Kwa maana hiyo basi, tuna masaa 48 kamili ya kupiga kura, baada ya hapo hakuna kura zitakazoingia tena.

Asanteni.
 
© Blogu Tanzania | Tarehe: 6/20/2007 |

Maoni: 4

Kwa viongozi wa muda - Hongereni sana kwa kua hai kila wakati.

pili kwa sababu imependekezwa kuwa na masaa 48 ya kupiga kura hii ikiimaanisha kuwa tarehe 29 - 30 Juni, 2007, nashauri muda uwe ni kuanzia saa 6 kamili usiku wa kuamkia tarehe 29 mpaka saa 6 kamili usiku wa tarehe 30 Juni, 2007.

Naomba kupendekeza!!
Lakini pia msimamo wangu ni kuwa kura moja kwa mpiga kura mmoja. Na hapa nasisitiza suala la ustaarabu kwa wapiga kura. Sioni sababu ya kura kuharibika wakati utaratibu mzima utakuwa wazi na wa kueleweka. Ikiwa hujaelewa ni vyema kuuliza kuliko kuharibu.
  Tarehe: 21 June 2007 at 23:44 Anonymous Anonymous Anasema:
HIVI KAZI YA UWEKA HAZINA NINI HASWA NDANI YA JUMUIYA HII? ATAKUWA NA KAZI KWELI? AU JINA TU? KUNA MAMBO YA FEDHA HAPA? AU?????
  Tarehe: 22 June 2007 at 19:43 Anonymous Anonymous Anasema:
Damija,naendele kuwapongeza kwa kazi nzuri mnayoendeleza,daima msikate tamaa, tuko pamoja. Mawasiliano kati ya kiongozi na waongozwao ni jambo la muhimu katika katika kufanikisha lengo.
Kuna mambo pale kwa michuzi (si yote) kina anonymous na wengine wameuliza nadhani si vibaya wakajibiwa( si wote) ili wasioelewa waeleweshwe.
Nadhani Michuzi pia anaweza kutoa sauti yake juu ya jumuiya hii.
Wamesema, wameuliza,wachache kwa kutokuelewa wamekebehi nadhani ni busara viongozi wa muda wakawajibu mle mle kwa ndugu Michuzi.
Ni wazo tu.
Naomba kuwasilisha.
Pius