MIRIAM KINUNDA (MALAQUIAS) - NAFASI YA KATIBU

Saturday, 9 June 2007
WASIFU.

JINA: Miriam Kinunda (Malaquias)
UMRI: 38
UTAALAM: Teknolojia.
URAIA: Mtanzania
BLOGU TOKA: 2006
TOVUTI TOKA: 2004 .
Kwa nini Nagombania Ukatibu.
Kupewa nafasi ya uongozi naamini ni kutumikia wale walioniteua, pia kushirikiana na viongozi wengine kutekeleza maombi yanayoletwa na wale waliotuteua. Elimu yangu ya teknolojia inaweza kutumika vizuri wakati huu ambao JUMUWATA bado changa. Nitatumia uwezo wangu na elimu yangu kutengeneza blogu mpya na pia kutekeleza majukumu yeyote kusaidia tovuti ya JUMUWATA iwe imara. -JUMUWATA inahitaji viongozi wenye uwezo wa kusikiliza sauti za wanachama wote bila ubaguzi, mimi nina Uwezo wa kusikiliza sauti ya kila mtu bila kupendelea. Uwezo huu ni wa muhimu sana wakati huu ambao JUMUWATA ni bado Changa na tuna majukumu ya kuunda katiba ya jumuiya.
NAOMBA KURA ZENU.
http://blog.mirecipe.com/
 
© Blogu Tanzania | Tarehe: 6/09/2007 |

Maoni: 16

  Tarehe: 9 June 2007 at 14:14 Blogger mwandani Anasema:
Vyema umechukua uamuzi wa kutaka kuitumikia JUMUWATA. Utaalamu wako unahitajika.
  Tarehe: 9 June 2007 at 20:01 Blogger luihamu Anasema:
Hongera sana,karibu ndani ya uwanja,ingawa huwa napitia blogu yako kila siku sijawahi kuoona chakula aina ya I-TAL FOOD.

Hongera sana.

Nuff Nuff Respect.
Miriam, halafu tunahitaji websaiti fulani ya jumuiya nzuri. Kura yangu unayo
Miriam hongera kwa kujitosa uwanjani. Kitururu unasemaje hapo?
Da mija: Sasa ndio uchaguzi.
Dah! mchuano mkali.
  Tarehe: 11 June 2007 at 03:19 Anonymous Anonymous Anasema:
Hongera kwa uamuzi huu.
  Tarehe: 11 June 2007 at 12:19 Anonymous Anonymous Anasema:
Wanaojitokeza wanatia moyo sana. Kutumikia watu ni wito. Jua kuwa nia yako ya kujitokeza kutuongoza tunaiheshimu.

(niko katika moshi mlimani nikila mtori...bado hujatuandikia habari za mtori!)
  Tarehe: 11 June 2007 at 19:10 Anonymous Anonymous Anasema:
Luihamu,
Mimi nilifikiria uta taka mapishi ya Jamaica? Basi nitakuwekea I-Tal special kwa sababu yako tu!! Lakini baada ya kura.

Kitururu,
Ndugu yangu usiwe na haraka, mambo yataanza yatakapo anza. Lakini atakayechaguliwa tutasaidiana eti heee.

Ndesanjo
Sasa naona unaturingishia mtori. Basi usiponipa kura, unilete mtori, usiponiletea mtori, unipe kura. Sawa!!!!
@Miriam:Tuko pamoja
  Tarehe: 12 June 2007 at 18:28 Blogger Mkina Anasema:
Hongereni wote kwa kuinga katika kinyang'anyiro kitakachoamriwa na wapiga kura makini kwa wagombea makini kwa neema na ustawi wa wanablogu wa Tanzania na kwingineko.
Big Up Mariam, Kitururu, Egidio, Da Mija, wengine wote na mwisho kabisa kabisa mimi mwenyewe.
Tuko pamoja twasubiri siku ya kutumia demokrasia yetu muktadha
Kidumu chama cha...(ahhh nini vile?) Wanablogu
Mimi nakupa hongera kwa kuamua kugombea ili kushika hatamu ya uongozi wa jumuiya yetu dada, wacha kura zifanze kazi yake!!
  Tarehe: 14 June 2007 at 20:02 Blogger luihamu Anasema:
Naomba nikuite Sister Mariam,

ulichosema ni kweli ngoja tusubiri naanda kamati yangu ya kampeni.

Kazi ipo.

Nuff Nuff Respect sister Mariam.
  Tarehe: 17 June 2007 at 19:12 Anonymous Anonymous Anasema:
Dada Mirium, endapo tutakupa nafasi ya ukatibu, utawasaidiaje wana jumuiya wasio na blogu kuwa nazo.Kwani wapo wengi wahitajio wasio nazo.
Naomba jibu lenye mkakatio unaoerlezeka sio siasa.
Kura yangu kwako yategemea uhawishi wa jibu lako.
Pius
  Tarehe: 17 June 2007 at 23:17 Anonymous Anonymous Anasema:
Pius,
Kama tulivyoamua wakati wa mikutano, nategemea kuunda kamati ya watu wachache wenye ujuzi wa kutengeneza blogu. Hawa watakaojitolea pamoja na mimi mwenyewe tutachukua majukumu ya kuwa saidia nawachama wapya.

Kuanzia mwezi ujao nitakuwa na muda wa kusaidia watu katika mambo kama haya.

Pia Ndesanjo amesha weka tovuti yenye maelezo ya kuanzisha blogu mpya http://mwongozo.wordpress.com/. Ningependa nijiunge nae ili tuandike maelezo(Tutorial) vizuri zaidi na kwa urahisi ili hata mtu ambaye hajui kutengeneza tovuti ataweza kuweka pamoja blogu yake mwenyewe.
  Tarehe: 22 June 2007 at 10:44 Anonymous Anonymous Anasema:
Hello Miriam,
You have my vote for some reason, but what I would want to hear is-what can a blog help people like me in the village and do you have a website?
IPS