Tarehe ya uchaguzi 30/06/2007

Thursday 14 June 2007
Wapendwa wanablogu, kamati ya muda inapenda kuwatangazia kuwa tarehe ya uchaguzi wa jumuiya itakuwa ni 30/06/2007. Tarehe hii imefikiwa ili kutoa muda kwa wagombea kufanya kampeni zao huku na kule na kuhakikisha wanablogu na wadau wote wanapata habari juu ya uchaguzi huu.

Pamoja na hilo, pia kamati imetoa nafasi za lala salama kwa yeyote ambaye bado angependa kugombea ajitokeze, bado tunahitaji watu na tunaamini watu tunao wenye kila uwezo wa kuinyanyua jumuiya yetu.

Asanteni wote.
 
© Blogu Tanzania | Tarehe: 6/14/2007 |

Maoni: 2

  Tarehe: 14 June 2007 at 19:59 Blogger luihamu Anasema:
Nakubaliana na kamati ya maandalizi.Tamko lenu ni muhimu kwa wanablogu wote.

Jah live.
  Tarehe: 17 June 2007 at 23:05 Anonymous Anonymous Anasema:
Siku hii sitakuwa karibu na computer mbaka tarehe moja mwezi wa saba. Sasa nitawezaje kupiga kura?