Gerald Shuma - Mshindi wa shindano la Nembo.

Tuesday, 3 July 2007


Wanablogu tulikubaliana kwamba baada kupata nembo itakayo simama katika jumuiya ndipo tutakapomtangaza mbunifu wake. Leo hii nachukua nafasi hii kumtangaza Ndugu Gerald Shuma mchoraji wa nembo namba 2 iliyochukua ushindi. Hongera sana Gerald!!!
 
© Blogu Tanzania | Tarehe: 7/03/2007 |

Maoni: 50

Hongera Gerald Shuma!Kazi nzuri!
  Tarehe: 4 July 2007 at 19:00 Blogger luihamu Anasema:
Kwa uongozi wa JUMUWATA.

Samahani kama nitakuwa naingilia ratiba zenu.

umuhimu wa kuunda kamati katika jumuwata,natumai uongozi hauta chukuwa mienzi kuunda kamati,narudia tena mimi pamoja na wanablogu wengine hatuta subiri mienzi miwili kamati ziundwe.

Kamati zinahitajika mapema,sio naandika ili nipate kamati baada ya kushindwa katika kuwania kiti cha uenyekiti lakini ile JUMUIYA IWE NA KAMATI ZAKE.

Nimweanza kuhesabu siku baada ya uchaguzi kuona kamati zitaundwa lini.

jah bless.
  Tarehe: 6 July 2007 at 18:32 Anonymous Anonymous Anasema:
Gerald
Hii ni kazi nzuri sana. Asante sana kwa kujitolea. Najua wanablogu wote wanashuuru inalau hawajaweka maoni yao hapa ya kukushukuru.
  Tarehe: 7 July 2007 at 02:24 Blogger Unknown Anasema:
nawashukuru sana kwa kunipa nafasi hii, asanteni wote.
  Tarehe: 7 July 2007 at 02:27 Blogger Unknown Anasema:
kwa wale wote wanaotoka nembo BURE au kwa bei nafuu sana, mnaweza kuwasilia nami kwenye email hii: isibingo@gmail.com
  Tarehe: 8 July 2007 at 14:38 Blogger luihamu Anasema:
Leo imitimia wiki baada ya uchaguzi kuisha,Jumuiya ya wanablogu imepata viongozi.

zimebaki siku kama 25 mwezi ukatike.Kwa jumla tuna mwezi mmoja na wiki kama 3 na nusu globalvoiceonline watatoa hale kwa awamu ya pili kuhusiana na miradi.

Sasa basi,viongozi wetu wa JUMUWATA sijui mnalipi la kusema kwani siku zinachomoka kama upepo.

jah live.
  Tarehe: 8 July 2007 at 18:14 Anonymous Anonymous Anasema:
Luihamu,
Naomba nichukue nafasi hii kukuomba utulie na tuache mara moja tabia ya kuwasakama viongozi tuliowachagua.Tumewachagua kwa sababu tuna imani nao na kwa maana hiyo tuna uhakika kwamba watafanya tunayoyatarajia.Tukianza kuwasakama sio tu kuwakosea heshima bali pia ni kama kuwaambia hawafanyi kazi yao.Ndio kwanza tumewapa majukumu mazito,wanahitaji muda kujipanga,kujua lipi walipe kipaumbele kwanza na lipi lifuate.

Wanayo madaraka kamili tuliyowapa kidemokrasia kwa hiyo sisi,kama wanajumuiya,subiri matokeo na maelekezo bila kusahau kuwapa msaada wa hali na mali tutakapoombwa au kuhitajiwa.

Pili kwa sababu tunaamini kwamba viongozi tuliowachagua watakuwa na jukumu zito na nyeti la kuunda katiba ya jumuiya,basi tusubiri tuone yatakayokuwemo kwenye katiba hiyo ili tuone wataweka nini katika kulinda na kuheshimu ethics and code of conducts za wanachama na pia viongozi.Kwa sababu hivi sasa katiba haipo ni vyema tukaepuka maswali kama "sasa basi,viongozi wetu wa JUMUWATA sijui mnalipi la kusema".Tusubiri,tuwe wavumilivu.Mambo mazuri hayataki haraka wala papara.
Nimechelewa kutoa pongezi kwako Gerald Shuma.Tunashukuru kwa nembo ya Jumuiya yetu
  Tarehe: 9 July 2007 at 08:23 Blogger luihamu Anasema:
JEFF MSANGI.
Samahni sana,lengo langu si kuwasakama viongozi wetu na sitawahi kuwasakama.Samahani Mkuu.

kwa viongozi
Lengo langi si kuwasakama au kuwavunjia heshima.Kama hatukuelewana vizuri naomba mniwie radhi,nasema samahani.

Jah bless.
  Tarehe: 13 July 2007 at 01:12 Blogger Gillian Anasema:
Beautiful! Would I be able to use it on my blog which supports the School of St Jude in Arusha?

I don't speak Kiswahili, so I haven't been able to read or respond to your blogs, though I would like to.
@Gillian:Of course U can use it.
@WanaJUMUWATA:Msione kimya, mambo yako jikoni yanapikwa.
  Tarehe: 17 July 2007 at 22:32 Anonymous Anonymous Anasema:
nembo inapendeza sana. Hongera kwa kazi yako nzuri gerald!
  Tarehe: 19 July 2007 at 02:24 Blogger Unknown Anasema:
nawashukuru sana kwa kunipa nafasi hii, asanteni wote.

kwa wale wote wanaotoka nembo BURE au kwa bei nafuu sana, mnaweza kuwasilia nami kwenye email hii: isibingo@gmail.com
Michuzi Blog & E-mail is Hacked! ONYO!

TANGAZO MUHIMU
Wanablogu, nimegundua sasa hivi kuwa Blogu na e-mail ya Muhidini Michuzi imekuwa hacked!

Kuna Tapeli Nigeria amefanya hivyo!

Nimeongea na Michuzi sasa hivi na anaomba watu wasambaze habari kuwa site imekuwa hacked na hiyo e-mail kuwa anaomba hela haitoki kwake.

Kwa sasa mnaweza kumpata kwenye e-mail issamichuzi@yahoo.com.

******************************************************************************************* E-mail iiyokuwa hacked ni hii: muhidin michuzi [issamichuzi@gmail.com]

How are you doing today? I am sorry i didn't inform you about my traveling to Africa for a program called "Empowering Youth to Fight Racism, HIV/AIDS, Poverty and Lack of Education, the program is taking place in three major countries in Africa which is Ghana, South Africa and Nigeria.

It as been a very sad and bad moment for me, the present condition that i found myself is very hard for me to explain. I am really stranded in Nigeria because I forgot my little bag in the Taxi where my money, passport, documents and other valuable things were kept on my way to the Hotel am staying, I am facing a hard time here because i have no money on me. I am now owning a hotel bill of $ 1550 and they wanted me to pay the bill soon else they will have to seize my bag and hand me over to the Hotel Management.,

I need this help from you urgently to help me back home, I need you to help me with the hotel bill and i will also need $1600 to feed and help myself back home so please can you help me with a sum of $3500 to sort out my problems here? I need this help so much and on time because i am in a terrible and tight situation here, I don't even have money to feed myself for a day which means i had been starving so please understand how urgent i needed your help.

I am sending you this e-mail from the city Library and I only have 30 min, I will appreciate what so ever you can afford to send me for now and I promise to pay back your money as soon as i return home so please let me know on time so that i can forward you the details you need to transfer the money through Money Gram or Western Union.

Thanks.

Muhidin Michuzi.

****************************************

NAWAKUMBUSHA KUWA HII HABARI NI UWONGO NA UNATOKA KWA TAPELI HUKO NIGERIA!
  Tarehe: 8 August 2007 at 09:39 Blogger luihamu Anasema:
Kazi safi sana hii,hongera ndugu MK.
Hii kurasa mpya inavutia sana na nimwelekeo mnzuri sana,sasa basi upande wa kuchaguwa blogu napendekeza blogu zote za watanzania ziorozeshwe,kwasababu nimeona blogu chache tu katika kidirisha cha BLOGU MBALIMBALI.

SELASSI I
Blogu zote kwa kweli ni muhimu zikawekwa pale kwani hii ni jumuiya yetu wote SI ya baadhi ya watanzania.
TUPO TUNASUBIRI MAMBO MAPYA TOKA KWA VIONGOZI KWANI KIMYA KINGI KINA MSHINDO MKUU
Karibuni kijiweni
Kweli imependeza.Hapa nimezima taa blogu hii inanipa mwangaza.Hongera uongozi mzima wa Jumuwata na bwana MK.

**Idumu Jumuwata
  Tarehe: 11 August 2007 at 21:34 Anonymous Anonymous Anasema:
MK,
Woo, Kazi nzuri sana sasa naweza kusema tuna blogu yetu.

Ningependa kuongeza kitu ambacho najua naweza kushambuliwa kama kawaida yangu.
1. Si visuri kuweka matangazo ya biashara katika ukurasa wa JUMUWATA kwa wakati huu.

2. Naona itakuwa vizuri tangazo la mahusiano na KMGroup litolewe. Hii ni jumuiya ya kujitolea na sio vizuri kuweka matangazo ya biashara zetu. Kwa sababu biashara zetu haziusiani na JUMUWATA. Lakini pia ingekuwa vizuri kuweka link ya blogu zote za Tanzania. Najua una ukurasa Ndesanjo alioanzisha ambao kuna blogu zote za Tanzania.

3. Kama tukiamua kuweka matangazo ya biashara zetu, tungfanya baadae bada ya katiba kuwa tayari na pia tulipishwe ili JUMUWATA ile na pesa za kujisaidia.

MK, sikukosei heshima nahisi pia utajiunga nami katika wazo hili. Na pia Wana JUMUWATA wenzangu.

Mija, Kitururu and Msangi, I hope you will add this in Katiba, I believe is a very important tiny issue.

Karibuni wanaotaka kunishamulia kwa email for being out spoken send email to info@mirecipe.com
  Tarehe: 12 August 2007 at 05:49 Anonymous Anonymous Anasema:
Hongera sana MK kwa kutujengea nyumba hii mpya.Naamini kwa kushirikiana na wataalamu wengine wa mambo ya web designs tulionao kwenye jumuiya mtaendelea kuiboresha zaidi.Kwa mfano ningependa kuona ule mwongozo wa jinsi ya kuanzisha blog aliouandika Ndesanjo,uweke pale juu ili tuweze kupata bloggers wapya ili jumuiya izidi kukua.

Wakati huo huo,ningependa kuunga mkono hoja ya Miriam.Kwa sababu JUMUWATA ni asasi isiyo ya kibiashara wala faida kwa wakati huu nadhani ni muhimu kubeba sura kamili ya non-profit.Kama hilo litabadilika, ni baadaye na vikao maalumu ndivyo vitaamua.Tunakushukuru MK lakini kwa wakati huu tafadhali tuweke kando kwanza matangazo ya aina yoyote ya biashara.Wazo la ule ukurasa wa Global Voices ni zuri sana.
  Tarehe: 12 August 2007 at 12:43 Blogger MK Anasema:
Habari,

Nashukuru kwa maoni mliyo yatoa ambayo nayaheshimu na pia nitashukuru kwa maoni mengine yatakayo tolewa na yataendelea kuheshimiwa.

Matangazo yametolewa sasa naona hakuna mengi mengine yatakayo semwa!!


Lakini kuna kitu kimoja ambacho sitoweza kukitoa ambacho ni kuonesha credit ya kwamba MK GROUP ndio imetengeneza blog, Hii ni kuonesha heshima na taadhima ya kazi na muda wangu nilio utumia ktk kazi hii.

Nadhani mtakuwa mmenipata.

Nawatakia siku njema.

Nashukuru.


Copyright 2007.

MK GROUP: CHEAP WEB HOSTING, DOMAIN REGISTRATIONS AND MUCH MORE.
MAHUSIANO.COM: BONGO FLAVA, BONGO DANCE, TAARAB, NYIMBO ZA INJILI, ZILIPENDWA AND ONLINE RADIO.
MK JOB PORTAL
VIJIMAMBOZ BLOG
  Tarehe: 12 August 2007 at 15:26 Anonymous Anonymous Anasema:
MK
Asante sana.

Jeff,
Asante kwa kueleza wazo langu vizuri zaidi.
Hivi naomba kuuliza Bwana MK AKIWEKA TANGAZO LAKE KUNATATIZO GANI?
NDUGU MK KAJITOLEA TENA BURE KUTENGENEZEA BLOGU ZETU BURE,TUKIWANASHIDA TUNAMKIMBILIA YEYE,LEO HII KUWEKA TANGAZO INAKUWA SHIDA JAMANI.MIMI SIUNGI MKONO WAZO LA KUTOA MATANGAZO YA MK.
unajua miriam na jeff mnashangaza sana kwani mlikuwa hamfahamu kuwa ktk kipengele cha vyombo vya habari mbalimbali hapo juu pia ni matangazo yale au kwa kua mnachuki binafsi kwakua mk kaweka matangazo yake basi roho ziwaume kama nanyi mnataka kuweka za kwenu basi wekeni lakini chuki binafsi haifai mbona viongozi wa jumuwata hawa jaongea iwejenyie.ametumia mudawake,akili zake na nguvu zake kututengenezea blogu nzuri kama hii bure lakini binadamu hamna shukurani,sio vizuri watanzania wenzangu.watu wengi nimeona blogu zenu zilivyo nzuri kwa ajili yake na hata ukiwanashida ukimfata atengeneze tena huwa hana kinyongo na anatengeza kwa malipo gani BURE.SIONI HAJA YA MK KUTOWEKA MATANGAZO YAKE.
NDUGU MK AMEKUWA MSTARI WA MBELE KUINUA NA KUTENGENEZA BLOGU MBALIMBALI ZA WANABLOGU KUTOKA TANZANIA,NDUGU MK AMEKUWA AKITUSAIDIA PUNDE TU BLOGU INAKOROFISHA,NDUGU MK KATIKA UBUNIFU WAKE KAWEZA KUINUA KWA KUTANGAZA NYIMBO ZA WASANII WA HAPA NYUMBANI KAMA NJIA MOJA YA AJIRA KATIKA KUNDI HILI LA VIJANA.

SASA BASI INGEKUWA VIZURI WANABLOGU WOTE WATANZANIA TUSEME
THANK YOU MR MK FOR YOUR CONTRIBUTION AND WE TAKE THIS OPPORTUNITY TO REWARD YOU IN A WAY YOU CAN ADVERTISE YOUR COMPANY ON THIS BLOG.

INAUMA SANA,TENA SANA MK HAS BEEN ON THE FORE FRONT MAKING SURE THAT WE GET QUALITY BLOGS.

HUU NI MTAZAMO WANGU,MTAZAMO WA RASTA KWASABABU RASTA ANAAMINI KATIKA HAKI NA USAWA KWA WOTE.

NAOMBA WANABLOGU TUPIGE KURA,WALE WANAOTAKA MK AWEKE MATANGAZO YAKE NA WALE WANAONA SI BUSARA KUWEKA MATANGAZO.

HESHIMA KWA MFALME HAILE SELASSI I.JAH LIVE.
  Tarehe: 12 August 2007 at 18:04 Anonymous Anonymous Anasema:
MIMI SIO MWANAGLOBU ILA NADHANI POINT YA KUTOKUWEKA MATANGAZO YA BIASHARA NI NZURI.CAPITALISM ISIPEWE NAFASI NDANI YA JUMUIYA YENU LA SIVYO MTAKUJA VUNJANA VIUNO.KILA MMOJA WENU ATAKUJA TAKA APEWE NAFASI YA MATANGAZO YA BIASHARA YAKE KWA SABABU YA MCHANGO WAKE FULANI.LEO MK ATASEMA MIMI NDIE NIMETENGENEZA BLOGU,KESHO SHUMA ATASEMA MIMI NDIE MTENGENEZA NEMBO,KESHOKUTWA LUIHAMU ATASEMA YEYE NDIYE ALIYEPENDEKEZA MKUTANO WA KWANZA,NDESANJO ATASEMA YEYE NDIE MWASISI WA BLOGU TANZANIA,MSANGI MDOGO ATASEMA MIMI NDIO MWENYEKITI,DAMIJA ATASEMA SIWEZI KUTUNZA HELA ZA WATU BILA KUPEWA NAFASI YA BURE YA MATANGAZO..MSURURU UTAENDELEA...MTAFIKA?KWA UJUMLA KILA MMOJA WENU ANAFANYA AU AMEFANYA KAZI NZURI.ENDELEENI KUJITOLEA,MSIWEKE FAIDA MBELE.

MTAZAMAJI-KUTOKA BUNGENI DODOMA
  Tarehe: 12 August 2007 at 21:14 Anonymous Anonymous Anasema:
kwanza kabisa ni sahihi kumpa pongezi MK kwa kazi yake sio hapa tu kwenye Jumuwata ila kwa wanablogu wengine.

Kuhusu matangazo. Nadhani tofauti zetu ni kiitikadi na kimtazamo. Je tunatazama vipi kazi za kujitolea?

Nimeona baadhi ya watu wamesema, "MK ametumia muda wake" hivyo ni vyema akaweka tangazo lake.

Kutumia muda wake sawa. Ndio maana ya kujitolea. Akitokea mtu mwingine akabadili kitu kwa kujitolea na kutumia muda wake hapo kwenye blogu, akaweka jina na nembo yake. Akatokea na mwingine. Na mwingine. Mbona litakuwa kama bango la matangazo?

Da Mija, kwa mfano, aliunda hii blogu mara ya kwanza kabisa. Alikuwa ndio anapandisha mambo yote mnayoyaona pale. Kila kitu. Lakini hakuna aliyekuwa anajua kuwa ni Da Mija. Alijitolea tu na wala hakukuwa na haja ya kusema kuwa yeye ndio kaiunda na kuweka habari zilizoko hapa.

Nadhani tutakapoanza kuona kuwa unaweza kutumia muda wako na ukaridhika kwa kazi bila kuweka tangazo tutakuwa tunapiga hatua moja ya kujenga utamaduni huu wa kujitolea bila kutaka chochote cha kufidia muda wetu (iwe ni tangazo, nembo, n.k.).
  Tarehe: 13 August 2007 at 11:04 Blogger MK Anasema:
Habari,
Wajameni waungwana naomba ili swala liishie leo na lisiendelee kuzungumziwa kwa maana wale waliotoa hoja hii ya mimi kutoweka matangazo na wengine wanao ungana nao nasema nimefanya kama matakwa yenu yalivyo sema. Nategemea mmelizishwa au kufurahishwa na uamuzi huu.

Ikumbukwe kuna mtu alisema hapo juu mbona mmetangaza Magazeti ya Tanzania (Vyombo vya habari)? Je hayo sio matangazo? Au mmeyaona yangu?

Kuweza kuondoa hizi shutuma za kusema eti nimetumia muda wangu kama wengi walivyoshikiria hilo, Kuanzia jana 12/08/2007 nimesitisha kazi ya kutengeneza blog kama nilivyo andika katika blog yangu ya VIJIMAMBOZ BLOG

Nawatakia siku njema na mkae kwa Amani.

Nashukuru.
Asante MK kwa kazi nzuri!Mengineyo naomba tusubiri kidogo tuyajadili kwenye katiba kuhusu nini kiwe ndani ya JUMUWATA na nini kisiwe.Samahani niko njiani na sijapata nafasi ya kuweka swala hili sawa.Lakini tuko pamoja. Kuhusu blogu zitakazo orodheshwa nazo zitasubiri katiba.Kwa maana nyingine zinaweza kukataliwa kikatiba. Tusubiri na aggregator ya Jumuwata ambayo itakuwa inapandisha mambo mapya yanayojiri katika blogu za JUMUWATA.Kazi inaendelea.Na kujadili maswala kwa kujenga kuendelee. Siku Njema!
NANUKUU,
Kuhusu blogu zitakazo orodheshwa nazo zitasubiri katiba.Kwa maana nyingine zinaweza kukataliwa kikatiba.

Hapa kuna kazi,natumai itabidi Mzee Ndesanjo utupe lecture ya blogu ni nini na katiba ni nini.

Mzee Mk naheshimu maamuzi yako.

Ndugu wanablogu naomba TUSIJEKUWA NA MAKUNDI MAKUNDI KATIKA JUMUWATA,KWAMAANA YA MAKUNDI YA WATU FULANI AU WANABLOGU WENYE (YES) BILA YES YAO MAMBO HAYAENDI,TUSIJE BAGUWANA.


HUU NI MTAZAMO WA RASTA,
HESHIMA NA UTUKUFU KWA HAILE SELASSI I.
  Tarehe: 14 August 2007 at 11:09 Anonymous Anonymous Anasema:
Matabaka na makundi yapo na tumeyaona toka mwanzo.

Tumesoma wote zamani, tumefanya kazi wote zamani, tupo wote nje ya nji, tuna aina moja ya fani ualimu, uandishi basi tabu kweli kweli.

Ingekuwa vipi mtu fulani fulani angeweka tangazo lake. Hacheni noma na kujuana. dole gumba rasta, true fighter.

mtz nawakilisha ndani ya Winnipeg, canada.
  Tarehe: 14 August 2007 at 17:18 Anonymous Anonymous Anasema:
Tafathali,
Nilipoweka maoni yangu kuhusu, matangazo katika ukurasa huu, sikutegemea kuwa tutaanza kuwa kama watoto. Angalia nyama vya wanablogu wa nchi nyingine, mfano KenyaUnlimited. Ukurasa wao mkuu hauna matanazo yao binafsi, na wala hatujui nani anafanya nini.

Ndugu zangu, tuache utoto. Hiki sio chama cha shule ya msingi. Mimi nilipoamua kublogu nilikuwa sijuani na mtu yeyote, na hata kama nikikujua sasa hivi, sita kaakimya nikiona kuna kitu umefanya kwenye blogu ya JUMUWATA ambacho hakifai. Tusiwe kama wanasiasa ambao wakitoa msaada wanataka nchi nzima wajue kuwa wamejitolea. Hawa hawajitolei kwa sababu wanania nzuri, bali wanatafuta kura au kujionyesha. Sisi tunatakiwa, tuendeleze jina la nchi, au tukosoe wanasiasa hao hao wanaojitolea na kujionyesha, mimi mwenyewe napoteza muda wangu jikoni kuandika vipimo vya mapishi yetu kisasa ili nitangaze mapishi ya nchi yetu na wala sijatosheka, ningependa watanzania wengine wajitokeze wafungue blogu nyingine za mapishi. Da Mija anaongelea kuhusu wanawake wa nchi yetu na nyingine, naweza kuendelea mbaka kesho.
Ndugu yangu Luhiamu, siamini kama Uligombea uwenyekiti kama huelewi maana ya "Non Profit Organization", utakuwaje mwenyekiti? Poa ndugu yangu.

Mimi hata Ndesanjo ambaye tunamuheshimu akikosea tu, nitamkosoa. Wanasema nyumba isiyokuwa na mwanamke, haina msimamo. Kaka zangu, kueni. Naanza kuona kuwa hii nyumba, itaitaji wanawake zaidi.

Kama MK alivyosema hapo juu, Yameisha, kashatimiza maombi.
Nakama kuna makundi ya watu sijuo waliosoma pamoja, toeni majina tujue.Hata Mwalimu Nyerere alichagua viongozi aliofungisha nao, au aliowafundisha

Haya mambo ya uswaili tuache, sisi ni watu wazima na pia nategemea tumesoma

Nategemea huu ndio mwisho, tusubiri Katiba ili tuweze kuweka mjadala maalumu.

Umoja kwa wote, na ndugu yangu Luhiamu, irie
  Tarehe: 14 August 2007 at 18:27 Anonymous Anonymous Anasema:
Dada Miriam,
Sidhani kama una haki ya kutukana watu hapa,kuwaita watoto,wakue nk.Kila mtu ana uhuru wa kutoa maoni yake hapa,hata kama yanaonekana ya kipumbavu namna gani.Kama una hasira zako na mambo mengine maishani basi usizilete hapa.Heshimu kila mtu tafadhali.Rasta ana haki ya kugombea nafasi yoyote ile na sio lazima mtu ajue maana ya non-profit ili kugombea cheo.Kama huna cha kuandika kaa kimya.
  Tarehe: 15 August 2007 at 01:33 Anonymous Anonymous Anasema:
Miriam muombe msamaha uliye mtukana sio vizuri kabisaaa ata kama una elimu yako na utu uzima wako sio kutukana wenzio hapa.

Elimu nini haswa zaidi ya ubinadamu wa kuheshimiana. Hapo dada umepotea njia na ni vizuri kuomba msamaha. Mbona watu wana elimu zao kubwa zaidi na mafanikio makubwa duniani na wanazidi kuheshimu wakubwa na watoto? Iweje wewe kushindwa kufanya hayo.

Ungetumia hiyo elimu yako, kutokuwa mswahili na utu uzima wako kufikiria kabla ujasema neno na kutukana watu.

Alafu inaonesha kila tunachofanya hapa ni lazima kifanane na wakenya au tunaiga?

Kuna kipindi Dar hot wire waliweka kazi yako kwenye website yao na wewe kudai waweke jina lako je na wewe sio unajionesha na kuwa mwanasiasa? Angalia unachosema dada usije ukapotea wakati historia ipo.

Think dada respect is very simple thing in life and just as an advice please go and search for a short course known as "Managing Self" so that you can understand better ways to live with other people in respect manner. please do so.

May God open your and our minds so that we can live as noble people.
  Tarehe: 15 August 2007 at 07:05 Anonymous Anonymous Anasema:
Miriam kuwa muungwana tafadhali toa tamko rasmi uombe msamaha kwa lugha ya kebehi uliyoitumia kwa wanachama wenzako.Utaua jumuiya wewe dada na maneno yako hayo
Waungwana turudini katika hoja!Hii kitu tuachie hapa.Ngojea nipandishe Katiba tujadili kuhusu hilo. Kila mtu asomapo au kuongea kitu , kuna pande milioni za kulisoma au kielewa kauli hiyo. Tusianze na mambo nishai katika mizizi ya JUMUWATA. Kila mtu ana haki ya kusema. Na kila mtu anahaki yakuchangia kuweka katiba ya JUMUWATA iwe sawa. Baadaye tunaweza kuitumia katiba kuweka maswala sawa. Na tunataka KATIBA ili iondoe baadhi ya mabo ambay o hayawi sawa. Katiba imechukua muda kutokana na mambo yasiyozuilika. Na KAtiba inajengwa si kiharaka na si kwa msingi wa matope. JUMUWATA tunataka iwe bora na ya manufaa kwa wote.Sasa wote kama wapendao JUMUWATA iwe poa, tusianze kupigana vita au kunyosheana vidole katika njia ambayo haijengi!
Wote ni muhimu!Wote tunahitajiana!Tuko Pamoja!
Tugombanie vipengele vya katiba na sio nani kasema , kafanya nini.Katibu
Nanukuu,kutoka kwa katibu
Tusianze na mambo nishai katika mizizi ya JUMUWATA. Kila mtu ana haki ya kusema.Mwisho wa nukuu.

Katibu kila mtu anahaki ya kusema,mbona mimi kipindi kile nilipokuwa nauliza kuhusu katiba niliambiwa na KEJELI?

Kwani yule msema kweli ndio hana haki hapa?

kuna baadhi ya vitu sasa napata shida kuvielewa,mimi nikisema kitu fulani napigwa stop wengine wakizungumza utasikiwa wakisema yaishia hapa.THIS IS NOT FARE MR.SIMON KITURURU.

Toka nimeanza kublogu sijawahi kumwita mwanablogu au watoa maoni majina kama
1.WASWAHILI
2.WATOTO
3.SISI NI WATU WAZIMA
4.HII SIO SHULE YA MSINGI

Sasa iweje katibu unasema kila mmoja anahaki ya kusema anachotaka kusema?

Mbona mimi kipindi kile nikitoa maoni juu ya katiba niliambiwa nawavunjia heshima na Mzee Ndesanjo akasema wakati mwingine nakejeli.Baada ya haya yote nilitoa tamko la samahani,iweje wewe katibu unasema yaishie hapa tujadili katiba,it is fare?
kwamaana nyingine kuna wale wanaoweza kutoa maoni na wasiulizwe?

Rasta ni mswahili,ni mtoto,sijui maana ya NON - PROFITABLE ORGANISATION,sawa lakini naomba heshima tafadhali,mimi sijawahi kutumia maneno kama hayo kwa mwanablogu yeyote.

Iam dissapointed kweli Simon.
  Tarehe: 15 August 2007 at 12:40 Anonymous Anonymous Anasema:
Nilikuwa nataka kuanzisha blog yangu na kujiunga na hiki chama lakini kama mambo yenyewe ndio haya ya kutukanana na wengine kukaa kimya (uongozi na wanachama wengine) basi mimi basi sitaki tena kuwa mwanachama. Hii ndio kuonesha ubaguzi na kujuana.

Miriam katukane watoto wako na familia yako huko nyumbani kwako na sio watu wengine, ata hao ndugu zako na watoto wako sio vizuri kuwatukana.

Uongozi mzima wa hii jumuiya na wanachama pingeni kitendo cha Miriam la sivyo jumuiya hii itakuwa ndoto hivi karibuni au itakuwa kwa ajiri ya watu fulani fulani tu.
  Tarehe: 15 August 2007 at 13:04 Anonymous Anonymous Anasema:
UAMUZI WA NEMBO YA JUMUWATA ULIPIGIWA KURA. PAMOJA NA KAZI NZURI AMBAYO WENGI WALIIPENDA HAKUNA JINA LA SHUMA PEMBENI AU CHINI YA UKURASA HUU ILI KUTANGAZA BIASHARA YAKE,

NANI KAMPA MK JUKUMU LA KUTENGENEZA DIZAINI HII, KWANINI UTARATIBU KAMA ULE WA KUCHAGUA NEMBO USITUMIKE HAPA, KATIBA INASEMAJE, AU KAMA MTU HAIPENDI DIZAINI ATAWEZAJE KUIONDOA, UKURASA ULE WA ZAMANI ULIKUWA NA MAKOSA GANI

OMBI: TEMBELEENI KURASA ZA VYAMA VINGINE VYA BLOGU NA KULINGANISHA DIZAINI

JE HII NDIO DIZAINI BORA ZAIDI KWA JUMUWATA INAYOMPA DIZAINA NAFASI YA KUWEKA JINA LA BIASHARA YAKE?

NAOMBA MAJIBU
  Tarehe: 15 August 2007 at 13:23 Anonymous Anonymous Anasema:
Kweli watu wanashangaza sana yaani unaona MK MK MK kila unapofungua hii globu!! Au biashara zake wewe zinakunyima usingizi na kazi ya kufanya?

Kwanini usione matusi ya Miriam? au wewe ni ndugu au rafiki yake?

Uliza uongozi wa jumuwata nani kampa MK jukumu la kutengeza globu hii, simple watakuwa wao tu.

MK kawa mtu mwenye busara na kutoa hayo matangozo lipi tena?! Au ndio chuki binafsi?

Unadhani biashara za MK zitasimama kwa kutoweka tangazo hapa? Jamani sio vizuri tulipe fadhila yeye katengeneza blog na kashatoa hayo matangazo nini cha zaidi?

Cha msingi na la maana ni kwamba Miriam aombe msamaha kwa matusi aliyo toa na sio kuona MK kila wakati. Ona aibu.
  Tarehe: 15 August 2007 at 15:16 Anonymous Anonymous Anasema:
tusiongee sana kwani hatujui miriam anawapa nini hao mpaka asikilizwe kiasi hiko na kusapotiwa.
Ndugu katibu pole na shughuli,tunasubiri katiba ipate kujadiliwa.

Nashukuru.
Kwa Katibu,
lini tutaijadili katiba na kamati zake?muda unazidi kwenda,weka mambo mezani tujadili kwa haki na amani pasipo UPENDELEO WOWOTE ULE.

AMANI.
  Tarehe: 18 August 2007 at 02:56 Anonymous Anonymous Anasema:
Uzuri ni kuwa hatujadiliana haya ana kwa ana maana naona tungeanza kurushiana viti na chupa. Hivi tuongeze "kamati ya usuluhishi"? Inaelekea tunavyokwenda tunahitahi tuwe na kamati hiyo. Labda iundwe na wazee, wawe wanatusuluhisha kwa busara zao. Katibu unasemaje? Tutafute wazee?
Luihamu na Mirium msirushiane vijembe!, Ndesanjo ushauri wako ni mzuri sana,sasa hao wasuluhishwaji wakigoma kusuluhishika tuwafanyaje?
Nadhani Babu wa blogu Ndesanjo alipaswa akemee haka katabia ka kurushiana vijembe wakati kila kitu hapa kinarushwa live.Kamwe lugha za dharau zisivumiliwe humu ndani.
Waungwana muombane radhi kuonyesha uungwana wenu.Katibu unasemaje?
  Tarehe: 23 August 2007 at 21:34 Anonymous Anonymous Anasema:
nani aliye anza mdomo na matusi? luihamu au miriam? nadhani jibu unalo.

bora twakutana ndani ya blogu, ingekuwa live mi ningeshambanjua mtu na kama bro dito vile. heshima ingetawala.
Leo ngoja niulize hii katiba iko wapi?kuandika katibu inachukuwa mienzi mitatu?je kuijadili na kuhakiki si nusu mwaka.Kama katiba iko tayari iwekeni mezani tuijadili maramoja tusonge mbele.Hivi kwanini wanablogu wengine hawaulizii kuhusu katiba yao au nikusema Rasta anahamu sana na hii katiba, kama tulivyoyaona matanzo ya MK GROUP nilitumai mngeuliza kwanini katiba haijawekwa mezani.

Ndugu wanablogu naelewa kabisa kwamba tunablogu kwa kujitolea,najuwa kabisa wengi tunamajukumu lakini nivizuri wanablogu tungekuwa tunaambiwa jamani Katiba bado au Katiba imekamilika au tunamsubiri mtu fulani na si kukaa kimya.

Ndugu wanablogu naomba tunzungumzie hili swala la Katiba,tuambiwe lini itatoka.
  Tarehe: 28 August 2007 at 20:48 Anonymous Anonymous Anasema:
Kwa kweli, mimi sijashirikiana sana kwa mambo haya ya jumuwata. Lakini, naomba tuwape nafasi ya kuendesha kazi yao. Kila mtu ana shuguli zake za kila siku.

Napendekeza viongozi watupe taarifa fupi fupi za kazi yao ya muda huu. Pia, naomba tujitahidi kuwapa tamaa pia. Kazi hii ya jumuwata ni kitu kipya kabisa. Si mchezo, tujitahidi kuwasaidia na mawazo yetu. Mambo yameanza hivi karibuni tu. Safari ni ndefu.
  Tarehe: 29 August 2007 at 16:38 Anonymous Anonymous Anasema:
Tunataka katiba, mtaendeshaje chama bila katiba zitakazo linda sheria na maadili ya chama!

Katiba mtupatie kwanza, kama kazi imewashinda achieni ngazi.

Ni demokrasia ya kujieleza naitumia.
Ndugu wanablogu na wanajumuwata,leo ni tarehe 3/9/2007 imetimia miezi mitatatu baada ya jumuiya yetu kupata viongozi.
Kabla ya yote si mlaumu yeyote bali nadhani we are out of time,we can not take 3good months and yet we have no Katiba until now.Nilitumai leo hii niikute katiba humu ndani.
Hapa simlaumu yeyote yule bali tujiulize nini kimetokea,kama tunasubiri utengenezaji wa aggregator basi tuendelee kuijadili katiba.Natumai kabla ya mwezi wa kumi 2007 katiba itakuwa imetoka we can not hold any more.
  Tarehe: 10 September 2007 at 00:27 Anonymous Anonymous Anasema:
Mbona mambo yameganda, ndo maana rasta anabwatukaga halafu anaambiwa kakosa heshima, katibu tuambieni kinachoendelea, toeni tamko fulani tujue, mkikaa kimya tutadhani ndo kifo cha mende kinaisubiri jumuiya, tuoindoeni hofu hii.