MATOKEO RASMI YA UCHAGUZI

Sunday 1 July 2007
Watanzania/Wanablog

Yafuatayo ni matokeo rasmi ya uchaguzi wa viongozi wa jumuia yetu. Lakini kwanza ni maelezo ya jinsi uchaguzi ulivyokwenda;

Jumla ya wagombea waliojitokeza kupiga kura ni 13. Kati ya hao mmoja kura yake iliharibika kabisa kwani alishindwa kabisa kupiga kura. Makosa mengine yaliyofanyika ni katika nafasi ya ukatibu ambapo baadhi ya wapiga kura aidha hawakukumbuka kabisa kuweka jina la waliyemtaka awe katibu au waliweka jina tofauti na mojawapo ya waliokuwa wagombea wa nafasi ya ukatibu ambao walikuwa ni Simon Kitururu, Miriam Kinunda na Yahya Poli. Kosa lingine ni kwamba wengi wa wapiga kura walisahau kupiga kura kuchagua nembo ya jumuiya. Wachache waliofanya hivyo ndio waliofanikiwa kutuchagulia nembo rasmi ya jumuiya.

Baada ya maelezo haya ndio matokeo

Nafasi ya Mwenyekiti

Ramadhani Msangi amepata kura 5

Luihamu Ringo amepata kura 4

Simon Mkina amepata kura 3

* Kosa lilikuwepo kwenye kura 1 iliyoharibika.


MSHINDI- RAMADHANI MSANGI

Nafasi ya Katibu

Simon Kitururu amepata kura 5

Miriam Kinunda (Malaquias) amepata kura 4

Yahya Poli amepata kura 1

* Makosa pamoja na kura iliyoharibika 3

MSHINDI – SIMON KITURURU


Nafasi ya Mweka Hazina

Mija Shija Sayi amepata kura 10

Egidio Ndabagoye amepata kura 2

* Kosa lilikuwa 1 tu kutokana na kura iliyoharibika

MSHINDI- MIJA SHIJA SAYI


Nembo ya Jumuiya

Kati ya watu 13 waliojitokeza kupiga kura watu 4 tu ndio waliopiga kura ya kuchagua nembo. Wote walichagua nembo namba 2. Kwa maana hiyo nembo namba 2 ndio nembo iliyoshinda.Inakuwa nembo rasmi ya jumuiya.

Kwa maana hiyo uongozi rasmi wa jumuiya yetu ni huu hapa;

MWENYEKITI- RAMADHANI MSANGI

KATIBU- SIMON KITURURU

MWEKA HAZINA- MIJA SHIJA SAYI

NEMBO NAMBA 2


Shukrani kwa nyote mliojitokeza kuchagua viongozi wa jumuiya yetu. Samahani nyingi kwa mliopata usumbufu au tatizo lolote wakati wa kupiga kura. Tuwape ushirikiano wa dhati viongozi wetu ili waliongoze vyema jahazi letu. Ahsanteni

Kwa niaba ya Kamati ya Muda

Jeff Msangi-Msimamizi mkuu wa uchaguzi.

 
© Blogu Tanzania | Tarehe: 7/01/2007 |

Maoni: 24

Nakubaliana na matokeo haya kwa 100%.Wanablogu woote tuko nyuma yenu katika kufanikisha maazimio ya kujenga jumiya yenye manufaa kwa umma woote wa watanzania.Pongezi kwa kamati ya uchaguzi

Ahsanteni sana.
  Tarehe: 2 July 2007 at 08:00 Blogger luihamu Anasema:
Nakumbuka ni jinsi gani nilikuwa nimejitolea katika maswala ya blog na kushiriki mijadala katika JUMUWATA.

Sina mengi ya kusema,naamini nivigumu katika dunia ya leo Rasta kuongoza au kuonekana anafaa katika jamii yoyote ile.

RASTA ANASEMA KWAHERINI.

JAH RASTAFARIAN.
  Tarehe: 2 July 2007 at 09:57 Blogger Kaka Poli Anasema:
Hongera kwa waliochaguliwa kuomgoza jumuia yetu. Wakati ni huu wa kuifanya Tanzania huru kwa kuleta mapinduzi ya kweli.

Hongereni sana!!
  Tarehe: 2 July 2007 at 11:36 Anonymous Anonymous Anasema:
Hongera kwa viongozi wachaguliwa wote.

Ninamwomba Luihamu kutulia, marasta wana heshima ya pekee katika dunia yetu. Avute subira, hawa wanapomaliza muda wao, naye aje apige kampeni kwa mbinu mpya. Hata hivyo, naona ameleta ushindani wa kutosha dhidi ya mteule. Kwa hiyo, anakubalika sana.

Pongezi nyingi kwa wapiga kura. Sasa ndiyo hasa mambo yanaanza, tusikunje mikono na kungoja tufanyiwe kazi na watu wengine.

Ciao
Nadhani kila mmoja kwa namna moja au nyingine alikuwa na sifa ya kushinda lakini kwa kuwa ni mtu mmoja kwa nafasi moja ndio maana wamepita waliopita,mmoja mmoja kila nafasi.
Ninawapongeza sana.Kazi kubwa ya kwanza mliyonayo ni ya kutuunganisha wanablogu wa bongo na kutuonyesha kuwa hii ni jumuiya yetu.
Blogu ya jumuiya iwe ina blogu zote za wana jumuiyana si za wateule wachache.Pawe na kanuni za kumuondoa anayezikiuka ili kudumisha nidhamu.
Naipongeza kamati ya muda kwa kazi nzuri waliyoifanya hadi kufanikisha uchaguzi.
Luihamu uchaguzi umekwisha tuwaunge mkono waliopita jumuiya isonge mbele.
Asanteni kwa wote walionipigia kura!

Naahidi kutekeleza shughuli za kiti nilichoteuliwa kwa uwezo wangu wote.Naahidi kushirikiana na viongozi wenzangu katika kutimiza wajibu wa kujenga jumuiya. Naahidi juu ya yote kushirikiana na wanajumuiya wote katika kujenga jumuiya yetu ambayo inahitaji ushiriki wa wana jumuiya wote katika ujenzi wake. Naamini si muda mrefu mikakati na hatua inayofuata katika ujenzi wa jumuiya tutaiweka wazi .
Nianze kwa kuwashukuru sana wale wote walioonyesha imani yao kwangu na kuniteua kwa nafasi ya uenyekiti. Asanteni sana. Kwa sasa najiandaa kupeleka nchini Uingereza oda ya suti moja maridadi sana kwa ajili ya kuapishwa rasmi, ila nina machache sana ya kusema kwa leo.

Kumalizika kwa uchaguzi huu ni kukamilika maana yake ni kuanza rasmi kwa ile safari ya kujenga jamii yenye fikra mbadala katika suala zima la ushiriki na ushirikishwaji katika maamuzi. Inawezekana kabisa kuwa viongozi tuliopatikana tukajivunia hilo, lakini ni vyema pia tukafahamu kuwa tumetegwa kupita maelezo.

Nasema tumetegwa kwasababu wanajumuiya wanategemea sisi kama viongozi waanzilishi kuweka historia ama ya kijinga kabisa kwa kushindwa kuinyanyua jumuiya, au ya kuvutia kabisa kwa kujenga jumuiya ambayo itakuja kuwa msingi imara wa Watanzania kubadilika. Hivyo si kazi ndogo tuliyonayo kama tunavyodhania.

Hata hivyo, naamini kabisa kuwa sote tulikuwa na tungali tuna malengo yaliyotusukuma kushiriki katika mchakato mzima wa kutufikisha hapa, na hii ikimaanisha kuwa tuna mawazo, nia, uwezo na ari ya kwenda mbele zaidi. Tusonge mbele jamii inatutegemea.

@LUIHAMU:
Ndugu yangu Luihamu naomba niwe wazi kwa kusema kuwa umenikwaza kidogo kusema kuwa marasta hawaaminiki kuongoza jumuiya. Imenisikitisha kwasababu wewe ni mpiganaji mzuri sana na mwenye kila silaha inayohitajika kushinda mapambano, inanisikitisha kuona umetoa kauli za namna hiyo.

Ni vyema nikakukumbusha kuwa, kupatikana kwa viongozi hawa sio kuwa ndio mwisho wa muundo wa jumuiya yetu. Tuna kamati, kurugenzi na vitengo mbalimbali vitavyoundwa kwa ajili ya jumuiya yetu, ambako kila mwana jumuiya ana nafasi ya kushiriki huko.

Daima nimekuwa nikiamini kuwa, kiongozi mzuri ni yule aliye nje ya uongozi ambaye anaweza kusoma makosa na ubora wa walioko ulingoni na kisha akaelekeza cha kufanya. Rubani ni mwongoza ndege tu, anayemwezesha kuiongoza ni yule aliye katika mnara wa kusomea mwenendo wa ndege yenyewe.

Nafsi yangu inaniambia kuwa maneno hayo uliyatamka kwa kejeli na kwamba nia yako ingali iko palepale kuhakikisha tunakuwa kioo cha jamii kwa ujumla.

TWENDE PAMOJA....ASANTENI SANA
  Tarehe: 3 July 2007 at 17:04 Blogger mwandani Anasema:
Hongereni kwa kupewa heshima ya kubeba dhamana ya uongozi. naamini mtapewa ushirikiano wa kuifikisha jumuiya inakotakiwa kwenda.
  Tarehe: 3 July 2007 at 17:26 Anonymous Anonymous Anasema:
Sasa Rasta ngoja nicheke kidogo,yaani ulivyokuwa unamudu kushiriki mijadala yote leo hii uongozi umeukosa hivi hivi,aisee kimbilia JEMBE RASTA nakumbuka ulivyokuwa unatetea KILIMO,ukaachana na kilimo ukaingia ndani zaidi ya tekinolojia,sasa umejionea mwenyewe.Pumzika Rasta.

101
  Tarehe: 3 July 2007 at 17:34 Anonymous Anonymous Anasema:
MOST OF US DONT KNOW HOW RASTA LUIHAMU FEELS,THE MAN HAD DESIRE TO TAKE US TO THE PROMISED LAND BUT THE MOJORITY VOTES COULDNT MAKE HIM THE WINNER.

RASTA YOU ARE DEVOTED TO HELP JUMUWATA SO DONT GIVE UP,A MAN HAS TO TAKE CHALLENGES AND AT THE END HE WILL WIN.

RASTA TAKE IT EASY MAN,THIS IS THE WAY IT GOES.
  Tarehe: 3 July 2007 at 17:40 Anonymous Anonymous Anasema:
Jamani kinachomuuma Rasta Luihamu,alikuwa wa kwanza kuingia na akawa wa kwanza kushindwa.

rasta naomba niwe mshauri wako.
rasta umeteleza haujaanguka.

LILI
  Tarehe: 3 July 2007 at 18:36 Anonymous Anonymous Anasema:
Rasta Luihamu Ringo,mmmmm dunia inamambo,KWAHERINImmmmmm.Rasta wewe mwenyewe ulipinga kwa mifano akina Anonymous wasishiriki katika zaozi la kupiga kura ukadhani walio na blogu utakupa kura sasa ungeungana nasi tungekupa kura kibao.

Rasta wenzako wanaula wewe umenuna mmmmmmmm.

RASTA unakubali watoto wamjini wakisema UTAISHIA KUNAWA KULA HULI?

mmmmmm.
  Tarehe: 3 July 2007 at 21:51 Anonymous Anonymous Anasema:
Mmmm Kitururu, yaani umenishinda kwa kura 1. I know you will do a good job my dear.

Sasa ukiitaji ku-redesign your blog to look like a blog for Katibu, send me email.

Contrats to all.
  Tarehe: 4 July 2007 at 06:52 Anonymous Anonymous Anasema:
Nasahihisha makosa hapo juu

Congratulations to all.
  Tarehe: 4 July 2007 at 09:24 Blogger Mkina Anasema:
Jamani hongereni wote kwa kuchaguliwa, nina imani kuwa mengi mazuri yatafanywa na jumuia yenyewe kwa pamoja. Ninawapa five na wote tuko pamoja. Walioshindwa, ikiwa ni pamoja na mimi ninasema hatujashindwa, bali tumekosa nafasi kwa sasa na baadaye tutazipata, tena wakati huo mambo yakiwa yamerahisishwa, katiba ipo, taratibu zipo na mambo mengine, hivyo itakuwa tumetafuniwa.
Ninaahidi ushirikiano kwa wote na Mungu awabariki kuimaridha Jumuwata.
@Miriam: Asante kwa hongera! Nimestukia kumbe kura moja ina nguvu kweli:-)

@Mkina:Umesema hapo!Hakuna aliyeshindwa.Tuko pamoja!
  Tarehe: 4 July 2007 at 17:15 Anonymous Anonymous Anasema:
Nawapongeza wote,walioshinda na waliojitahidi kwani na amini kabisa hakuna aliyeshindwa,naamini wato wameshinda kwa vishindo vya tembo kule serengeti.

Luihamu naomba jibu,
kama ungepewa nafasi hiyo then wengine wote wabehave the way you are behaving,ungejisikiaje?
ZEPHANIA.
  Tarehe: 5 July 2007 at 13:03 Anonymous Anonymous Anasema:
Wote mko pamoja na ninawaomba muwe sawa sawia. Mkina ameonyesha uungwana na anapaswa kugombea nafasi zingine za juu. Ninamfahamu na ana uwezo wa kuongoza, bali sfari hii hakupata nafasi. Tuko pamoja.
Ninashauri kuwa wakati mwingine panapotokea uchaguzi, endapo kuna mtu ndugu yake wa damu anasimamia uchaguzi, basi asigombee au huyo ndugu yake wa damu asiwe msimamizi mkuu, kwani kwa taratibu za uchaguzi wa online anaweza kuwa pekee mwenyewe mwenye password na hivyo kuwa na mamlaka makubwa yanayoweza kutia shaka matokeo halisi.
Zaidi ya hapo naomba majina ya waliopiga kura na kura zao ziwekwe kwenye blogu hii kuepusha hisia za watu kama Rastaman wangu.
@kwa Laihumu namuomba asiwe na hasira, atapata nafasi zingine za juu zaidi tena zenye heshima ambazo zitamjadili hata huyo mwenyekiti mwenyewe.
Tunashukuru kuwapata viongozi. Hii kitu (Jumuiya) inaanza kuwa ya ukweli sasa. UHURU!
Hongereni wote jamani. Kazi ndio hiyo mmekabidhiwa tushiriiane uifanya kwa pamoja
  Tarehe: 13 July 2007 at 19:14 Anonymous Anonymous Anasema:
Nawapongeza wote.
Damija uko wapi mama?,tumeku miss hapa jumuiyani.Sema japo kidooooooooooooogo!
Hongereni washindi na tusonge mbele.
Anonymous hapo juu miye nipo usihofu, tumebanwa kidogo na mikakati mipya ya JUMUWATA. Punde si punde tutarudi kwa moto mkali.
  Tarehe: 17 July 2007 at 22:32 Anonymous Anonymous Anasema:
hongereni kwa viongozi! Nawatakia kila ya heri ya kuendesha mambo ya blogu hapa tanzania