Dondoo ya Katiba!

Tuesday, 11 September 2007
Tafadhali soma dondoo ya katiba upate muelekeo wa nini kitafanyika.
Maoni yako yatasaidia kukamilisha katiba hii.

Kwa kifupi katiba iko kwa lugha mbili; Kiwahili na Kiingereza.
Kumbuka kuwa inatakiwa kugusa wanablogu wote popote duniani.

Ni muhimu kukumbuka umuhimu katiba kuchukua sura za kijamii na sheria za kimataifa. Kwa maana hiyo tunaiandika katika jinsi ambavyo ndani kwa ndani zitaweza kutatua aina
zozote za migogoro itakayoweza kujitokeza.


Lakini, kimsingi kama tutaamua kuisajili rasmi jumuiya yetu basi itachukua sheria za nchi ambayo itasajiliwa ndani yake. Tanzania ni nchi muafaka ingawa wanablogu wametawanyika dunia yote.

Kumbuka kuwa miradi ya JUMUWATA kamaitakubalika hapo baadaye itafanyika zaidi Tanzania.

Katiba kamili itapandishwa baada ya kukubaliana wote kuwa imegusa mambo yote.
Tazama dondoo hapa chini na changia, kosoa, jazia kwa kutoa maoni .

DONDOOyaKATIBAyaJUMUIYA
 
© Blogu Tanzania | Tarehe: 9/11/2007 |

Maoni: 6

  Tarehe: 12 September 2007 at 17:46 Anonymous Anonymous Anasema:
Nitachangia ila nikitulia vizuri, baada ya hii mikutano. Ila shukrani kwa kazi ya kutuletea katiba hii (tena kwa lugha mbili).
Kazi imeanza.
Naomba turekebishe sehemu ya kwanza kifungu namba 24.
kifungu hiki kinaeleza ya kwamba mwenyekiti hatakiwi kuigeuka JUMUWATA akiwa ofisini,

Sehemu ya pili,kifungu namba 33(masharti ya ukatibu)
inaeleza katibu hatakiwi kuigeuka JUMUWATA akiwa ofisini.

Sehemu ya tatu,kifungu namba 36(kazi za mamlaka yake katika JUMUWATA)
inaeleza hivi,mweka hazina anahakikisha kuwa mwenyekiti anajua hali ya kifedha ya JUMUWATA mara kwa mara.
pia kifungu namba 42(masharti ya kazi ya uweka hazina)
inaeleza hivi hatakiwi kuigeuka JUMUWATA akiwa ofisini.

sehemu ya 4,kifungu namba 45(uteuzi wa wanakamati)
inaeleza hivi,pia wanakamati wanaweza kupendekezwa na wanajumuwata waaminio wuwezo wao ....
pia kifungu namba 48(mashrti ya kazi za wanajumuwata
inaeleza hivi mwanakamati hatakiwi kuigeuka jumuwata wakiwa ofisini.

Ndugu wanajumuwata,kwa mtazamo wangu naona katiba inataka kuwa na mfumo wa usiri,usiri huu unatokana na wao(mwenyekiti,katibu,mwekahazina na wanakati)kubanwa kuto kuigeuka jumuwata hata kama kuna maovu yanatendeka ndani ya jumuwata.Kwa mtizamo wangu napendekeza hivi vipengele virekebishwe,kwasababu endapo itatokea kuna ufisadi au ajenda za siri basi wao watakaa kimya.

Ndugu wanajumuwata,kwanini wengine wapigiwe kura na wengine wapendekezwe na wanajumuwata?hapa nazungumzia wanakati,tukisema wakupendekezwa nadhani watatokea watu kwa ajili ya maslahi ya watu fulani.Naomba tuwe makini sana.Napendekeza hiki kifungu kibadlishwe na wanakamati wote wapigiwe kura tu.

Ndugu wanajumuwata sioni kama kunasababu yoyote ya mweka hazina kutoa taarifa tu kwa mwenyekiti,napendekeza kuwe na taratibu fulani ambapo wanajumuwata watapitia kurasa itakayo orodheshwa mahesabu yote.

licha ya muda kubana,najitahidi kupitia katiba yetu.

AMANI.
Mie nimeshindwa kuifungua(download) hii katiba.
@Ndabuli:Sijui tatizo liko wapi .Mimi naifungua kwa kutumia Microsoft Word na inafunguka.
  Tarehe: 13 September 2007 at 15:11 Anonymous Anonymous Anasema:
Sehemu ya 56; Zawadi kwa bloggers.

Ninapendekeza kiongezwe kipengele cha Blogu bora ya michezo.

Naomba kuwasilisha
  Tarehe: 13 September 2007 at 20:57 Anonymous Anonymous Anasema:
na mimi pia, nimeshindwa kuifungua.