Kuhusu Aggregator!

Monday 29 October 2007
Aggregator itakuja!

Funzo kutoka kwenye jumuiya zenye aggregator kama ya Wakenya; www.kenyaunlimited.com ; maswala haya kadhaa yanatakiwa kuwekwa sawa.


Kuwa kujenga aggregator bomba kunahitajika umiliki webhosting account yako. Kwa mfano baadhi hutumia A Small Orange, http://asmallorange.com/services/hosting/ , hasa hapa maarufu ni medium account ambayo huwa na gharama za USD 100.00 kwa mwaka.

Unahitaji kununua domain name.
Wengi wanashauri domain name inunuliwe tofauti na web hosting hasa kama unaweza kuamua kubadilisha web hosts baadaye.

Baadhii wameonekana kutumia zaidi huduma za kusajili domain names kupitia Name Cheap http://namecheap.com/ ambao wanagharimu USD 9.00 kwa a .com or .org name.

Katika ujenzi wa aggregator baadhi wamekuwa wanatumia software iitwayo Gregarius http://gregarius.net/ ambayo ni open source.


Hii ni katika kutoa mwangaza kidogo wa nini kinatarajiwa katika hili.
Wataalamu wa computer katika umati wetu mnakaribishwa kutoa hoja au hata msaada wa kimawazo au mwingine wowote!
Tunaamini wako wanajumuiya wenye mchango au mwanga zaidi katika swala.

Karibu kuchangia , kuuliza au hata kukosoa!
Tuko Pamoja!
 
© Blogu Tanzania | Tarehe: 10/29/2007 |

Maoni: 3

  Tarehe: 23 November 2007 at 11:51 Anonymous Anonymous Anasema:
hapa nadhani tutaikumbuka kazi ya ndugu MK.
  Tarehe: 12 December 2007 at 15:35 Anonymous Anonymous Anasema:
wabongo bwana kwa kupenda makampuni ya nje mi nashangaa sana wakati bongo kuna makampuni kibao ya web hosting kama:

1 E-XTREMETECH.NET
2 SIMBAHOST.COM
3 RAHA.COM
4 DARCITY.NET
5 BOL.CO.TZ

Lakini wapo sawa kupeleka pesa kwa wazungu kuliko kwa watanzania wenzao. Tutafika wakati mnashangaa eti miaka 46 na bado tupo masikini wa akili, kimawazo, ata kipesa. Haibu tupu na hapo nimetaja machache tu.
anonymous wa pili,
asante kwa mawazo yako lakini napenda kukutaarifu MK ni mtanzania mzalendo na yeye anaweza kutusaidia kwa sababu ni mwanajumuwata.

pia kama bei ya kuhost ni nafuu kutoka ughaibuni basi itabidi tufanye nao kazi.

amani.

TUENDELEE JAMANI.

SIMON HONGERA.