KATIKA KUFUFUA WAZO ZURI la JUMUWATA , baadhi ya maoni kutoka kwa BWAYA!

Thursday, 12 March 2009
Nasikitika kukubali kuwa JUMUWATA ilibakia jina kinamna kwa wengi.

Chakutia moyo ni kwamba wenye uchungu wapo na naamini JUMUWATA imefufuka na tuipe punzi tu .

Kabla sijaongea sana!

Pata baadhi ya maoni ya watu kutoka katika mjadala ulioanzishwa na Bwaya na Rasta Ringo Jr Luihamu.

Ukimaliza kama wewe ni mgeni na JUMUWATA basi soma tuliyokuwa(YALIYOPITA) tunafikiria tufanye na JUMUWATA ili tusirudie kosa na endelea kukosoa na kuchangia nini kiendelee kutokea hapa.

Simon Kitururu.G.shayo said...

Bwaya hapo umenena,mimi nilishaliuliza swali hilo mara nyingi sana lkn mimi sikupata jibu,kwa kifupi mimi hilo jambo linaniumiza sana.hebu mwenyekiti/katibu watujibu.
7/3/09 8:02 AM

Fadhy Mtanga said...

Kaka Bwaya hapo nakuangushia gwala. Umenena kitu chenye. Wakubwa inakuwaje? Si hatuyataki mambo ya alfu tisa mia sabin' na saba. Jumuiya yetu haipaswi kutokomea.
Tunapaswa kuifanyia kitu.
7/3/09 9:14 AM

Anonymous said...

Kaka Bwaya umenene,

hili jambo tulivalie njuga.asante sana kwa kujituma.

amani rasta hapa.
8/3/09 11:35 PM


Mtingwa said...

Mjadala mzuri. Kumbe mnayo organization? How do you go about it? Kwani hatuisikii!
9/3/09 4:36 AM


kamala J Lutatinisibwa said...

tumsubiri ndg kitururu atupeyake majibu kwanza
9/3/09 5:44 AM


kamala J Lutatinisibwa said...

tumsubiri ndg kitururu atupeyake majibu kwanza
9/3/09 5:44 AM


SIMON KITURURU said...

Nimesoma msuto na nitajibu!
9/3/09 7:48 AM


Bwaya said...

Nafikiri uwe ni mjadala wetu wote. Wale wapya ambao hatukuwepo wakati jumuiya inazaliwa, nao wanakaribishwa. Tuulize maswali ikibidi. Na Katibu wetu (kwa niaba ya viongozi wengine wasiojulikana walipo hivi sasa) atajaribu kujibu, kuelekeza na kuweka mambo vizuri.

Nia si kushutumu bali kujaribu kuangalia wapi tulikojikwaa ili tujisahihishe.

Labda tuanzie hapa. Kwamba jumuiya yetu imelala. Hilo halina mjadala. Sasa tujadili kipi kinakosekana na cha kufanya ili kuifufua ni kipi.

Tafadhali tusiogope mjadala.
9/3/09 1:33 PM


Koero Mkundi said...

Hivi kumbe kulikuwa na Jumuiya?
Ndio kwanza nasikia hizi habari.
Haya wale walioaminiwa na kupewa dhamana ya kuongoza mashua hiyo wajitokeze wenyewe hadharani tuwaweke kiti moto na kama wamechemsha basi wajitoe wenyewe wasisubiri kustaafishwa kwa manuafaa ya jumuiya.
9/3/09 9:11 PM


Kissima said...

Da! Kumbe kuna jumuia ya wanablog,? Ni hatua nzuri iliyokwisha kupigwa.
Hivi malengo hasa ya jumuia hii ni yapi?
Viongozi wa jumuia hii wako wapi? Namfahamu Kaka Kitururu basi.
Kuna malengo gani ya baadae kuhusu jumuia hii?
Mpaka sasa jumuia hii imeshapata mafanikio gani?
Ni vigezo gani vinazingatiwa ili mtu kuwa mwanachama?
Kuna kauli mbiu yoyote ya jumuia?
9/3/09 11:07 PM


luihamu said...

samahani fungua kurasa ya kuchangia mawazo kuhusu jumuiya ya wanablogu tanzania.

http://blogutanzania.blogspot.com/

www.ringojr.wordpress.com

N.B nimejaribu kuweka au kusambaza ujumbe huu takribani blogu 15.Naomba tusaidiane katika hili,tuhamasishe ili wengi waelewe umuhimu wa blogging na kuwa na jumuiya.

Bwaya kwa pamoja tunaweza.

amani.
10/3/09 12:59 AM


Anonymous said...

Hivi mwili unaweza kufanya kitu kinachoeleweka kama kichwa kina matatizo? Niambieni. How can it be?
10/3/09 2:37 AM


kamala J Lutatinisibwa said...

tufanye kitu kimoja muhimu. sisi wenye blog fualni zinazojikita kwenye kutafuta majibu ya changamoto tulizo nazo, tuunde jumuiya yetu ya kujitegemea

ni wazo langu tafadhalini
10/3/09 2:47 AM


Bwaya said...

Ringo, asante kwa hamasa. Ni kiu yetu sote kwamba wazo lililozaliwa mwaka 2006 lisife bila sababu.

Uhai wa Jumuiya yetu unatutegemea sisi sote. Si jukumu la watu fulani pekeyao ambao kimsingi hawatastahili lawama yoyote ikiwa mambo hayatakuwa kama inavyotarajiwa.

Tuifufue jumuiya yetu kwa pamoja.
10/3/09 2:50 AM


Bwaya said...

Kamala, sijakupata vizuri. Naomba ufafanue vizuri kwa sababu jumuiya tayari ipo na kinachofanyika ni kuifufua.
10/3/09 3:03 AM


kamala J Lutatinisibwa said...

basi tufanye juhudi za makusudi za kuifufua ili na sisi tusiokuwemo tuwemo. vinginevyo tujadili kwa mkabala mwingine. ni vyema tukawa na chombo chetu imara. basi tuunde kamati maalumu ya kuifufua kamati hiyo iwe chini ya uenyekiti wako ndugu bwaya, amina
11/3/09 12:35 AM


Bwaya said...

Kamala, nadhani tunachokifanya sasa hivi ni juhudi hizo hizo za kuifufua Jumuiya yetu. Ufufuzi huu unapofanyika kwa njia ya mijadala ya wazi inapendeza zaidi badala ya kuunda kamati kama wanavyofanya wanasiasa. [Manake tunaweza kuunda kamati ikaja na mapendekezo ambayo tunayaundia kamati ili kuja na hatua zitakazotekelezwa na kamati nyingine!]

Nadhani (kwa maoni yangu) kuwa kujadiliana kama tunavyofanya kunaweza kabisa kuifufua jumuiya hii.

Halafu Kamala ukiisha kuwa mwanablogu tu ni 'automatiki' kwamba unakuwa mwanachama wa Jumuiya hiyo (Labda taratibu zikibadilishwa). Kwa msingi huo, nawe umo japo hukuwaunablogu wakati inazaliwa mwaka 2006.

Narudia tena kwamba haipendezi tunapoanzisha vitu halafu tunaviacha vinaelea elea hivi na hatimaye vinajifia bila sababu.

Hata kama ni kweli kwamba wengi waliokuwepo enzi za 'vuguvugu' la Jumuiya hawaonekani lakini hiyo haitufanyi tuogope kushiriki ufufuzi huu kwa pamoja.

Unaonaje hapo?
11/3/09 4:08 AM


Mtingwa said...

Nimeipitia ile blogu ya Jumuiya. Iko kimya tangu mwaka juzi. Mimi nimwulize Katibu, nani mwenye access na blogu ile?
11/3/09 5:11 AM


Anonymous said...

Bwaya ni lazima tupate access ya ile blogu ili mijadala ianze au
tutumia hata hii blogu yako kuendesha mijadala.

jamani naomba tuchangie.

ringojr.
11/3/09 8:01 AM


Anonymous said...

Ringojr tupe maoni yako nini kifanyike
11/3/09 11:04 AM


Nalilia haki said...

Nakubaliana na anon wa 10/3/09 2:37AM. Tatizo linaloimaliza jumuiya yetu ni la kiuongozi zaidi. Mwenyekiti mbali na kutokufahamika kwa 'wananchi' lakini inaelekea kuna mazingira yasiyoeleweka yaliyomweka madarakani. Kwa mfano nilipokuwa nafuatilia kumbukumbu za mwenendo mzima wa uchaguzi kwenye blogu ya blogtanzania, nilibaini hitilafu kubwa. Uchaguzi ule ulifanyika kwa mizengwe ya kimaslahi ambapo nahisi msimamizi wa uchaguzi huo alizidiwa na damu.
Pamoja na malalamiko mazito yaliyotolea baada ya 'upishi' wa matokeo hayo, bado jamaa walibaki yakichekelea na kukejeli.

Ndugu zangu kinachotokea sasahivi ni matokeo ya kuchezewa kwa uchaguzi ule. Msilalamike
12/3/09 7:09 AM


kamala J Lutatinisibwa said...

nimekuelewa bwaya. japo umekosea nilianza kublog toka 2006.

sawa, tuendeleze mjadala
12/3/09 7:12 AM


Yasinta Ngonyani said...

Mimi ni mgeni kabisa sikujua kama kuna jumuiya ya wanablog. Na sijui mlikuwa mnajadili nini na kama kumekuwa kimya hivi basi inapaswa tufanye kitu nini sijui wenyeji watuambie.
12/3/09 9:09 AM

Mzee wa Changamoto said...

Amani, Heshima na Upendo kwenu nyote.
Nashukuru kaka Bwaya kwa changamoto hii. Kwangu naweza sema machache. Kwanza ni kwamba tutahitaji kujua mipaka ya nani anaweza kujiunga na jumuiya. Ninalomaanisha ni kuwa kwa kuwa nina imani kuwa wanajumuiya tutakuwa na orodha mahala fulani, tunahitaji kujua kama kutakuwa na "ratings" za blogs zetu. ni kwa kuwa kuna wenye habari za kiutambuzi, kiuchanganuzi, kijamii, misaada ya kielimu, misaada ya kijamii kwa ujumla, taswira na hata wapo ambao wao ni "strictly" ngono. Kwa hiyo kujua ni vipi tutaweza kuwa na mipaka ya nani atakuwepo kwenye jumuiya na ambaye hatakuwepo ni kwanini asiwepo. Na hapo ndipo linapokuja suala alilosema ndugu Kamala hapo juu kuwa na vi-branch vya jumuiya ambavyo vuinaendana na yale muandikayo. Na hili lina ukweli maana sisi wa changamoto, utambuzi na mijadala hatuna utendaji sawa na wale wa taswira pekee. Naamini umeliona hili. Lakini pia hata namna tunavyoshirikiana (baina ya bloggers) utagundua kuwa ni tofauti. Na kuendelea kung'ang'ania jumuiya kubwa isiyo na watu wa mtazamo mmoja ni afadhali kutengeneza ndogo itakayokuwa mfano kwa wengine na namna ambavyo tutaweza kutumia uzoefu wa hii kuendeleza hiyo KUBWA.
Nawakilisha na ntarejea kuendeleza mjadala kwa manufaa yetu sote.
12/3/09 9:25 AM

Bwaya said...

Asante Mube bila shaka Katibu atalichukua hili kama changamoto.
 
© Blogu Tanzania | Tarehe: 3/12/2009 |

Maoni: 3

Mpaka hapa naamini Jumuiya imefufuka.
Kufunguka kwa ukurasa huu ni dalili nzuri.
Shukrani za pekee kwa juhudi za Katibu wetu, Simon Kitururu.
Tutakuwa tumefanya jambo la maana sana ikiwa tutamwuunga mkono kwa hatua hii iliyofikiwa.
Hakuna kurudi nyuma!
Kesho Jumapili napandisha hitimisho na tuendelee mbele
kwa mbele kwa tuwezacho!
Kitururu
Mimi nadhani suala la JUMUWATA linawezekana endapo tutaweka ubinafsi pembeni. Zipo changamoto zingine kama vile hii JUMUWATA itakuwa ikisimamiwa na nani mbali na wanachama wake mf. Baraza la udhamini/Ushauri, suala la kuwa na katiba, kuwa na utaratibu wa kuwatambua wanachama, Utaratibu wa kisheria, masuala ya michango pamoja na namna tunavyoweza kushirikishana katika tasnia ya habari.

Tofauti kubwa niliyoiona ni kuwa kwa sasa kuna kundi fulani ambalo linaonekana kutawala katika tasnia hii pengine ni kutokana na umaarufu wao ama system kuwalinda. Mfano suala la vigezo na wapi ilipotoka wazo la tuzo za blog na mdhamini alikuwa nani? Bado linaacha maswali mengi na ufa mkubwa. Kikubwa hapa ni kuondoa tofauti na kuunganisha nguvu kwa pamoja ili baadae kusije kukawa na migongano ya kimaslahi, kisheria, mtazamo,itikadi kutoka kwa kundi moja lenye nguvu ya pesa na umaarufu dhidi ya lingine.

Suala lingine ni kuwa na jukwaa huru kwa wanablogu kama ilivyo kwa majukwaa mengine ambayo yatatuwezesha kushirikishana changamoto zetu na namna ya kuweza kupashana habari , elimu na ujasiriamali. Hivi sasa kila mtu anajifanyia chake. Nashauri kuanzishwe hata facebook page itakayoweza kutembelewa na watu wengi.

Mwisho ni lazima tuwe na miiko ambayo kila mwanachama ni lazima aitii na kuiheshimu. Yaani nidhamu ya kila kitu. Naamini suala la JUMUWATA linawezekana endapo tukidhamiria kwa nguvu zetu.